Unyanyasaji wa wapinzani: Namuomba Mungu anaetoa maagizo atangulie mbele za haki atuachie nchi yetu

kwakua hii imeenda tayari,

wakati mwingine muafaka kama huu tukijaaliwa Neema na Baraka ya uhai kadiri ya mapenzi ya Mungu,

Tuwaombee Hekima na Busara wagombeaji uongozi wa upinzani kujaza fomu za kugombea uongozi vizuri kwa utulivu bila mihemko, makasiriko, ghadhabu wala mchecheto ili wasikosee tena.

Inafaa vyama vya siasa kujiamini na kua na uhakika na mchakato mzima wa uchaguzi na malengo yao.

Wajiepushe na mawenge ya mara hatushiriki mara tunashiriki uchaguzi . Ooh mara hakuna haja ya kujiandikisha mara tukajiandikishe huku muda unakwenda n.k

Kusitasita, Staki na taka ndiyo imewafikisha hapa walipofikia wapinzani nchini.

Mengineyo ni porojo na story za pata potea tu 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…