Unywaji wa pombe una athari mbaya kwenye ubongo, utafiti wabaini

Unywaji wa pombe una athari mbaya kwenye ubongo, utafiti wabaini

Hawa wazungu wanataka tufe na stress, pombe angalau inasahaulisha matatizo kwa muda...sasa ukae mkavu tu siku zote haki ubongo wenyewe lazima ukutume relaxers

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Hata kiroho pia
Kiroho ndio mbaya zaidi. Nawaonea huruma wanywaji wa pombe ninaposoma maneno haya ya Biblia:
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi…"(1Kor 6:9-11)
 
Mh!! Ebu kuwa muungwana kidogo, acha kufananisha pombe/ Bia/UGIMBI na vitu vya kijinga kama Corona
Unaithamini sana pombe. Hujasoma maneno haya ya mfalme Suleiman?
"Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima."(Mit 20:1).

Wine is a mocker, and beer is a brawler. Whoever is led astray by them is not wise.
 
Hebu nipishe
Kweli kabisa, mwambie tena shetani akupishe, upite, asije akakufanya ushindwe kuiona mbingu kwa sababu ya pombe, bia au ugimbi. Shetani yeye ameishahukumiwa; anachofanya sasa ni kuwavuta wanadamu kwenye anasa za dhambi ili siku ile ya mwisho waangamie wote jehanum ya moto.
 
Kwenye amri za mungu hakuna sehemu wamesema pombe ni dhambi. Yaani ninywe glass ya wine nilale zangu halafu mungu aje kunichoma moto baadae? You are not serious mkuu. Yesu mwenyewe kwenye harusi ya Kana alitengeneza pombe watu wakanywa na kusaza.
 
Kiroho ndio mbaya zaidi. Nawaonea huruma wanywaji wa pombe ninaposoma maneno haya ya Biblia:
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi…"(1Kor 6:9-11)

Ameen Ameen Ameen Mkuu..

Ahsante Mkuu kwa kuongezea nyama,haswa uzinzi tena ndo kaa la moto kabisa.

Ndio maana kwa mkristo itapendeza after 6hrs/3hrs aombe toba kwa Mungu.

Kwa sabbu ya dhambi ya matamanio + kuwazia
 
Kwenye amri za mungu hakuna sehemu wamesema pombe ni dhambi. Yaani ninywe glass ya wine nilale zangu halafu mungu aje kunichoma moto baadae? You are not serious mkuu. Yesu mwenyewe kwenye harusi ya Kana alitengeneza pombe watu wakanywa na kusaza.
Hiyo Biblia yako kama inasema Yesu alitengeneza pombe, ni feki. Tafuta Biblia og.
Yesu alitengeneza divai njema(isiyolewesha)
 
Utafiti huo unathibitisha pasina shaka kuwa Biblia ni kitabu cha kweli. Watafiti wanagundua leo madhara ya pombe; yenyewe Biblia ilishaona madhara mengi miaka mingi iliyopita. Look how it says in the Book of Proverbs:
"Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye,Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? …Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; mwisho wake huuma kama nyoka.Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; na moyo wako utatoa yaliyopotoka.Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti. Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; wamenipiga wala sina habari…" That was written thousands of years ago!
Mbona inaruhusu kunywa divai sio pombe
 
Wasomi wasikuhizi wepesi sana nilijua bongo tu kumbe in TATIZO La DUNiA
 
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Oxford wanasema hata unywaji kiasi wa pombe unahusishwa na kuenea zaidi kwa athari mbaya kwenye ubongo kuliko ilivyotambuliwa awali. Utafiti huo umebaini kwamba kiasi chochote cha unywaji wa pombe kinaweza kukuletea madhara kwenye ubongo wako.

Utafi huo uliofanyika kwa kutumia hazina ya sampuli za Ulaya unasema : "Hakuna kiasi salama cha pombe kwa ubongo kilichobainika. Unywaji wa kiasi wa pombe unahusishwa zaidi na kusambaa kwa athari mbaya kwenye ubongo kuliko ilivyotambuliwa awali."

Utafiti huo uliwahusisha washiriki 25,378 kwa kutumia data kama vile umri, jinsia, elimu , ripoti binafsi ya kiwango cha unywaji wa pombe, ukubwa wa ubongo na afya kwa kutumia scan za MRI, taarifa kuhusu hospitali na matibabu ya bila kulazwa, pamoja na vipimo vya kumbukumbu. Pia ulibaini kuwa unywaji wa pombe ulichangia kwa kiasi kikubwa athari nyingine zilizosababishwa na mambo mengine, ikiwa ni pamoja na uvutaji wa sigara.

Walibaini kuwa hapakuwa na kiwango "salama" cha unywaji wa pombe, ikimaanisha kuwa unywaji au kiasi chochote cha pombe ni kibaya kuliko kutokunywa kabisa pombe. Walibaini pia kwamba haijalishi unakunywa aina gani ya pombe. Na kwamba hali fulani alizonazo mtu kama vile shinikizo la juu la damu, unene wa kupindukia wa mwili, vinaweza kuwaweka watu katika hatari ya juu. Watafiti waliongeza.

Wataalamu wa magonjwa ya ubongo wanasema wakati bado hatujapata dawa za tiba kwa magonjwa yanayoathiri ubongo kama dementia, kufahamu juu ya mambo yanayoweza kuzuia madhara ya ubongo ni muhimu kwa afya ya umma.

Source: BBC

Utakua mzinzi na msengenyaji sana
 
Hiyo Biblia yako kama inasema Yesu alitengeneza pombe, ni feki. Tafuta Biblia og.
Yesu alitengeneza divai njema(isiyolewesha)
Nionyeshe waliposema divai njema. Walisema alitengeneza divai hawakuspecify
 
Back
Top Bottom