Uoga: Kongamano la Katiba lazua balaa Mwanza. RPC aanza kumung'unya maneno, amsingizia Rais

Uoga: Kongamano la Katiba lazua balaa Mwanza. RPC aanza kumung'unya maneno, amsingizia Rais

Acheni ujinga, kongamano la katiba litatusaidia nini kwa wakati huu?

Shida zetu wenyewe ni kongamano tosha.
Wote ni wachumia tumbo, sijaona wa kumtetea mwananchi hapo, shida ni kutaka kutawala tu ,hawana jipya.
 
Ni sawa katiba mpya Ila Nina kaswali ka kizushi.
Je , hao wanaoandaa wangekuwa madarakani kweli wangekomaa kuidai katiba

..Ni nadra kwa aliyeko madarakani kudai katiba mpya.

..Lakini inategemewa kuwa ataiheshimu katiba iliyomuweka madarakani.

..vilevile inategemewa hatavunja sheria kwa kuwabugudhi wananchi, wanasiasa, na wanaharakati, wanaodai HAKI zao kwa njia ya amani na kwa mujibu wa katiba.
 
Sahivi chadema ndo wamegeuka wavunja miongozo ya kujikinga na Corona yani pamoja na kwamba kandabya ziwa ndo inaongoza kwa maambukizi bado mnakutana tu
 
..Ni nadra kwa aliyeko madarakani kudai katiba mpya.

..Lakini inategemewa kuwa ataiheshimu katiba iliyomuweka madarakani.

..vilevile inategemewa hatavunja sheria kwa kuwabugudhi wananchi, wanasiasa, na wanaharakati, wanaodai HAKI zao kwa njia ya amani na kwa mujibu wa katiba.
Ni ngumu sana kwa pande zote mbili kuyatimiza haya uliyoandika hapa.

Ni lazima mmoja au wote wawili kwa pamoja wayakiuke yote au baadhi ya hayo matatu kwa nyakati mbalimbali.

Isipotokea hivyo, basi sheria na Katiba yetu havitahitaji kufanyiwa marekebisho..
 
Hii ndio taarifa ya usiku huu kutoka Mwanza kwa hisani ya Maranja Masese

View attachment 1856391
Polisi wa Tanzania wamekosa weledi, hawajiamini, wanafanya kazi zao sio kwa kufuata maadili yantaaluma zao ila matakwa ya CCM.
Polisi hawajui kwamba katiba mpya ni takwa na haki ya raia wote, wanadhani KATIBA MPYA NI KITABU CHA MATUSI CHA KUITUKANA CCM
 
Katiba mpya naimani itapatikana,ila haitapatikana kwenye sahani ya dhahabu,lazima ipatikane kwa staili yake.Ni ngumu Sana Afrika kupata haki kwa mseleleko,mpaka jasho na damu vionekane.viongozi wetu mnapokosa busara ndogo mtalazimishwa kuokota busara hizo.
 
Ila mwanza kuna corona serious naomba chadema acheni kufanya mambo ambayo yanafanywa na ccm pls don't

Corona imetoka kumchukua kaka yake na mbowe lakini hamjaridhika tu mnaenda kwenye risk

Sikubaliani na kauli ya kamanda ila pia sikubaliani na mikutano ya chadema kukusanya watu.

Media zipo wazi sasahivi nendeni uko mkatoe elimu

Juzi Mbowe aliitwa clouds alienda? Nchi ina taharuki ya Miamala, corona sijui sadala yaani upuuzi mtupu

Hebu niacheni Mimi nipige pombe aisee Leo weekend!

"Katiba mpya ni kipaumbele sana kuliko vyote, ila siyo kuzidi kujihami dhidi ya Corona," -- mzee Warioba.

 
Back
Top Bottom