Uonevu dhidi ya Mbowe: Viongozi wa dini toeni kauli ya kitume

Uonevu dhidi ya Mbowe: Viongozi wa dini toeni kauli ya kitume

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Posts
13,203
Reaction score
23,027
Uzi huu ni mahsusi kwa viongozi wetu wa kiroho (maaskofu na mashehe)

Hakuna Mtanzania (wakiwemo viongozi wa serekali wenyewe) asiyejua kuwa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubambikwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe ni nia ovu ya kutaka kumkata makali katika adhma yake ya kupigania haki kwa watu wote hapa nchini kwetu.

Kwa ajili ya muktadha tu.

Mbowe ni mzazi.

Mbowe ni kiongozi wa siasa anayeheshimika barani kote Africa and beyond.

Mbowe ni mfanyabiashara mwadilifu - vinginevyo angekuwa tayari amebambikiwa makosa ya uhujumu uchumi siku nyingi

Baba yake Mbowe alipigania uhuru wa nchi hii, hivyo Freeman ni mtu ambaye damu yake imeshikamanishwa moja kwa moja na uhuru wa Tanganyika / Tanzania

Mbowe ni mtoto wa kiroho wa baba wa taifa Mwalimu JKN (Mungu amrehemu)

Viongozi wetu wa kiroho simameni mhesabike. Tunajua mnajua tunajua mnajua tunajua kwamba Mbowe anaonewa na serekali. Sababu za kuonewa kwake sihitaji kuzirudia hapa kwani zipo well documented.

Haya mambo ya kuonewa na kunyanyaswa chini ya serekali ya CCM ni suala la zamu. Usiponyanyaswa leo, ipo siku yako huko mbeleni inakuja - bila kujali wewe ni mtumishi wa Mungu au la. Anaweza kuja kutokea kiongozi mwingine wa hovyo zaidi kuliko hawa waliopo sasa kwa utashi wake tu akaitumia katiba hii kuwasulubu ninyi viongozi wa kiroho. Hahitajiki nabii kuliona hili likija huko mbeleni.

Kwa sababu sasa wamejitokeza watu jasiri walioamua kusimama kwa niaba yetu, hakuna wakati muafaka mwingine zaidi kwenu viongozi wa kiroho kupaza sauti zenu ili Mungu akapate kutenda kupitia kwenu haki ipate kutamalaki katika taifa letu alilotupa Mungu mwenyewe, sawasawa na maandiko matakatifu katika Biblia (Zaburi 7:11)


1627021213091.png
 
Labda hao maaskofu lakini hakuna shehe mwenye kauli ya kitume, mitume ni mitume na mashehe ni mashehe darja tofauti. Alafu shehe na siasa wapi na wapi labda shehena
 
Sadaka iko wapi yaani amegaidi huko alafu sisi viongozi wa dini ndiyo mtusumbue, kwani Mamakula hayupo.

Alafu Afrika bado sana hivi wewe hao viongozi wa dini unawatambua kiimani au kisiasa na imani ipi? Kutoka wapi?
 
Mimi na wewe tuendelee kuwakumbusha wajibu wao wa kiroho katika jamii yenye mtindio wa haki
Jaribu tu taratibu kuwalist viongozi wote wa dini kichwani kwako, tafakari wale viongozi wote wa mabaraza ya dini ukristo, uislamu na wengineo...

Halafu niambie ni nani atayeweza kuendana na unachokishauri?

Wakati wale viongozi ndio huwa waalikwa wakubwa wa CCM kwenye hadhira kubwa, au mikutano ya kufunga na kufungua kampeni za CCM n.k
 
Jaribu tu taratibu kuwalist viongozi wote wa dini kichwani kwako, tafakari wale viongozi wote wa mabaraza ya dini ukristo, uislamu na wengineo...

Halafu niambie ni nani atayeweza kuendana na unachokishauri?

Wakati wale viongozi ndio huwa waalikwa wakubwa wa CCM kwenye hadhira kubwa, au mikutano ya kufunga na kufungua kampeni za CCM n.k
Sawa. Lakini hilo halituzuii kuwakumbusha wajibu wao kama viongozi wa roho za watu. Najua uamuzi ni wao lakini wacha siye wengine tutimize wajibu wetu!
 
Alikuwa hajajua kama ni gaidi, gaidi ni gaidi tu. Kwamwulizeni zitto na Dr Slaa wanamjua.
 
Back
Top Bottom