Uonevu dhidi ya Mbowe: Viongozi wa dini toeni kauli ya kitume

Dah, eti gaidi.. magaidi wa kweli mmewaachia last month.. leo mnamdondoshea zigo Bwana AIKAELI..!!
 
Viongozi wa kiroho waliunga mkono kwa dhati rasimu ya katiba mpya ya Tume ya Warioba. Haya ya ugaidi dhidi ya Mbowe ni mbinu ya kuzima moto mpya wa katiba mpya. Njia mojawapo ya viongozi wa kiroho kunusuru taifa letu sasa ni kuonyesha kuwa bado wanaunga mkono rasimu Tume ya Warioba ya katiba mpya. Watanzania wengi walitarajia kasikia kauli za viongozi wa kiroho kuhusu uchaguzi mkuu wa 2020 lakini mpaka sasa kimya. Kwa hali ilivyo sasa viongozi wetu wa kiroho wakiendelea kuwa kimya sijui watakuja kukemea maovu gani katika jamii na taifa letu wakasikilizwa.
 
Hata hao viongozi wa dini kutolea tamko huu utoto unaiofanywa na serikali ni kupoteza muda. Yaani ni utoto wa hali ya juu kufanywa na vyombo vya dola.
Mtoto akikosea pamoja na kufanya utoto lazima akemewe
 
Mtoto akikosea pamoja na kufanya utoto lazima akemewe

Kama ingekuwa ni watoto sawa, sio hayo majitu mazima na mengine mazee yanafanya huo upuuzi. Wameshindwa hata kumkamata aliyejiunganishia bomba la mafuta wamebaki kufanya sinema za kitoto. Hao ni kuwapuuza tu.
 
Mmoja wa wachache sana wanaojitambua huyu hapa...

Kwani mwamakula hajatoa kauli?
 
Hata hao viongozi wa dini kutolea tamko huu utoto unaiofanywa na serikali ni kupoteza muda. Yaani ni utoto wa hali ya juu kufanywa na vyombo vya dola.
Kweli. Viongozi wa kiroho hawahitaji kutolea kauli maigizo ya wanasiasa kama haya. Badala yake wanastahili kutolea matamko mambo ya msingi yanayotatiza taifa kwa kipindi hiki. Ukweli ni haya maigizo ni mkakati wa watawala wetu kuzima madai ya katiba mpya. Tunajua kuwa viongozi wa kiroho waliunga mkono kwa dhati rasimu ya katiba mpya ya Tume. Hoja kubwa ya kisiasa inayotugombanisha sasa hivi kama taifa ni katiba mpya. Viongozi wa kiroho wanayo nafasi kubwa kunusuru taifa kwa kuliwezesha kuvuka kiunzi hiki cha katiba mpya.
 
Tuwaachie jeshi la polisi wakamilishe upelelezi na kisha mahakama ifanye kazi yake mbivu na mbichi zitajulikana. viongozi wa dini waendelee kuhubiri amani.
 
Bagonza na Mwamakula si mnao huko? Waambie watoe matamko
 
Tuwaachie jeshi la polisi wakamilishe upelelezi na kisha mahakama ifanye kazi yake mbivu na mbichi zitajulikana. viongozi wa dini waendelee kuhubiri amani.
Magufuli naye alikuwa anawataka viongozi wahubiri amani hivi hivi. Kilichompata March 17 anakijua mwenyewe!
 
Kwani Bagonza, Mwamakula na Ponda wanasemaje wao?
 
Mnafanya ugaidi alafu mnakimbilia kwa wakuu wa dini, hapa mtawapa wale mnaowatumiaga miamala na wanatumia jina la dini kama kivuli tu
We ombea tu ugaidi siku ugaidi ukikuathiri ndo utapata akili
 
Viongozi wa dini si ndiyo hawa mnawatukana kila siku? Kauli ya Mwamakula (whatever his name is) inawatosha
 
Tuwaachie jeshi la polisi wakamilishe upelelezi na kisha mahakama ifanye kazi yake mbivu na mbichi zitajulikana. viongozi wa dini waendelee kuhubiri amani.

Jeshi la polisi linaendekeza siasa za kitoto, wameshindwa kumkata aliyejiunganishia bomba la mafuta, wamebaki kutumiwa kwenye siasa za kichovu. Watu tunataka katiba mpya, sio huu utoto wa polisi.
 
Ile kamati ya amani iliyokuwa inapiga marufuku matumizi ya neno mwendazake sijui ipo wapi wakati huu.
 
Hawa Viongozi wa dini wazee wa legacy ya mwendazake!!

Hii nchi wanafiki ni wengi mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…