Uongo gani mkubwa uliwahi kuongopewa na mwenza wako ukaja kujua ukweli?

Uongo gani mkubwa uliwahi kuongopewa na mwenza wako ukaja kujua ukweli?

Habari wakuuu,

Kama tunavyojua kwenye harakati au maisha ya kimapenzi tunakutana na misuko suko ya hapa na pale, misuko suko ambayo inatufanya tuyachukie mapenzi au mahusiano.

Moja ya mambo yaliyoshamiri kwenye ndoa na mahusiano ya nyakati hizi ni UONGO uliokithiri.

Mimi binafsi niliwahi kuongopewa ujauzito na binti mmoja miaka ya nyuma kwa kuwa tulikuwa tukiishi mikoa tofauti na nilikuwa namuamini sikumtilia shaka.

Pia soma: Jambo gani baya umewahi kumfanyia mpenzi wako na utajutia milele?

Nililea mimba mpaka miezi mitano ndipo dada yake alipokuja kuniambia baada ya kuwa na yeye alikuwa anakereka na jambo alilokuwa akinifanyia mdogo wake, baadae alikuja kukiri na kuniomba msamaha, Sikumsamehe.

Rafiki yangu na yeye ilimkuta kwa binti mmoja wa Kihehe mpaka mimba ikazaliwa baadae akasema mtoto amekufa.

Je, wewe ndugu uliwahi kukutana na uongo upi kwenye ulimwengu wetu wa mapenzi?
Anafanya kazi usalama wataifa nikaja kujua ni usalama wamapenzi hana hata nyumba kapanga gari na kila kitu niuongo
 
Aliniambia ana miezi mitano hajaingia period na kwao huko ni kawaida eti...

kumbe ana mimba ya miezi minne

mimi nilikuwa namchora kama sielewi vile, nilishaiba mkojo nikaenda pima UPT nikakuta tayari ni mjamzito kutoka kwa ex wake

huyu dem alitoroka kwao na kunifuata huku town anafos kuolewa kumbe anakimbia timbwili kwa wazazi...

Fak-ha
 
Back
Top Bottom