VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Mambo sasa yanaanza kujianika kwenye mkeka wa uhakika. Ukweli unauzidi nguvu uongo kama mbegu inapochomoza kwenye udongo. Ukweli unaanza kutamalaki kama mashabiki kindakindaki au mwalimu na chaki. Tumedanganywa sana na kwa muda mrefu.
CAG amemwambia Mhe. Rais kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa hasara ya mabilioni ya shilingi za kitanzania kwa miaka mitano sasa. Lakini Mwendazake na wenzake wamekuwa wakituamisha kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa faida. Katika kuchagiza hilo, ATCL imekuwa ikitoa hadi gawio kwa Serikali. Tulikuwa tukidanganywa.
Serikali ya Mwendazake ilijaa propaganda na uongo mkubwa. Tumeanza kuona upande wa pili wa tulichokuwa tukiambiwa. Ukweli unaupiga kumbo uongo uliotaka kudumu kwa muongo mzima. Amini nawaambia, hilo ni tone tu kwenye bahari ya propaganda zilizokuwa zikiendelea wakati wa uongozi wa Mwendazake. Mengi yanafuata baada ya tuta.
Ndugu yangu Kichere, angekuwepo Mwendazake ungeiwasilisha Ripoti ile inayoanika ATCL na hasara zake?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)