stakehigh
JF-Expert Member
- Aug 9, 2019
- 7,134
- 4,556
Hapo kwenye ATCL, Mama Samia kaangushiwa jumba bovu. Hana budi kuchukua hatua za haraka kutafuta mbia/wabia toka sekta binafsi nchini na hata nje kuliendesha shirika hilo. Na huo ni mtihani mkubwa sana hasa nyakati hizi za janga la covid-19. Kupata mbia makini ni kazi ngumu sana sasa hivi. Aidha, usimamizi wa hali ya juu unahitajika katika mchakato mzima hadi utendaji wake.
Akichelewa ni mwendo wa kuendelea kumimina mabilioni kuhakikisha ndege zinaendelea "kuremba" viwanja na anga la Tanzania kuwafurahisha wanaofikiri ndege ni toys za kujivunia kwa majirani! Na serikali ndio ina zigo hilo la ndege kama mmiliki. ATCL wao wanasubiri tu kukabidhiwa hela ya kula (operating funds) waendelee "kuzitembeza" popote. Sijui Watanzania wangapi wanajua kwamba ukiirusha Dreamliner toka Dar es Salaam hadi Mwanza (459 nautical miles) kwa nauli za ushindani ni hasara hata ikiwa imejaa kabisa. Hata zisiporuka, pesa ya uhakika lazima itoke.
Rwandair iliwatoa jasho hadi ikabidi wawakabidhi Qatar Airways 49% ya hisa na jukumu la uendeshaji. Hiyo ilikuwa kabla ya corona. Kabla ya hapo walijaribu kulibinafsisha shirika lakini hakuna aliyekuwa akitoa bei inayoeleweka. Hii sio biashara inayochangamkiwa duniani na sasa corona ndio imeharibu kabisa. Kuna mashirika kadhaa yaliyokuwa yakienda vizuri kama Air Mauritius, sasa hivi linaelekea kufilisika.
I wish Her all the best. She'll certainly solve the problem, I believe.
privatisation waulize rwanda nn kinaendelea, na kama hujamaliza rwwanda fuatilia kenya airways! mind you kenya ways ilikua privatised way before covid ni miaka mingi nyuma results zake umeziona lakini?