Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Mkuu hata kapicha hakuna?[emoji848]
 
Jehanamu (bonde la Hinom/Gehenna) ni eneo lililo nje kidogo ya Jerusalem ambalo hapo zamani lilitumika kuchoma miili ya wafu.

Jehanamu was a metaphor.

Kwanini Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kaumba ulimwengu huu wenye kuruhusu mabaya!?
 
Akakuletea manabii na vitabu Ili vikupe muongozo jinsi gani uishi Dunia na Baada ya kuondoka duniani

Sasa wewe kama umesoma vitu vyote Yani
TAURATI
ZABURI
INJILI
QURANI
Kwanini Mungu huyo kwa uwezo wote alionao anatuma watu kuhubiri na sio malaika?

Nlitegemea huko makanisani na miskitini wangekuwa wanahubiri malaika.

Sisi ni binadamu na hatutegemei uwepo wa mungu ili tuwepo.

Lakini Mungu hawezi kuwepo bila binadamu. Mungu huyo anategemea uwepo wa watu kwamaana tumemuumba sisi aishi kama wazo, ili atusaidie kujibu maswali magumu yaliyotukabili hapo awali.

kwasasa mambo mengi tumeweza kuyaelewa na kuyaelezea bila haja ya kuweka dhana ya Miungu.

Wewe uliyeshikilia mambo ya miungu, ni kwamba umeshikwa kwenye uzamani tu na hutaki kubadilika.

Yaani kama ni nguo umevalia fashion ya mwaka 1653.

Kwa miaka yote hyo kwanini Mungu huyo kajificha!?

Kwanini tunahitaji vitabu hivyo ulivyovitaja ama wahubiri na manabii kumhubiri na asijihubiri mwenyewe!?

Ukweli kwamba Mungu hawezi kufanya jambo hili yeye mwenyewe ni ushahidi mzuri ambao unakuonesha Mungu huyo hayupo.
 
Kisichokuwepo hakipo...!! hata kukitamka au kukifikiria haiwezekani maana hakipo...huwezi ukasema Mungu halafu ukasema hayupo....umejuaje Hayupo halafu ukamtamka....!
Kwahyo spiderman (Buibui mtu) yupo?
 
Si kila maji ni ya kunywa na si kila dini ni ya kihuni, usipite kwenye njia za mkato katika kuhukumu kitu, kwanza pata maarifa ya kina kuhusu jambo halafu ndiyo uweze kutetea msimamo wako. Tofautisha kati ya dini na wafuasi wa dini. Wazungu walitudharau waafrika kutokana na mafundisho ya Biblia kuwa Ham mtoto wa Noah alilaaniwa na baba yake kwa kuwa alimcheka pindi alipolewa na kuwa uchi (soma Genesis 9:20-27), na Ham ndiyo baba wa waafrika, na ndiyo miongoni mwa sababu waliyoipata hao wazungu kutufanya watumwa na kututawala. Waarabu wamesambaza dini si kwa ajili ya kiuchumi bali ni kwa ajili ya kuwalingania wanadamu katika kumuabudu Mungu Mmoja. Hakuna hata nchi moja ya kiarabu yenye kutegemea uchumi wake kutoka nchi za Afrika. Na hakuna imamu mwenye msikiti wake, misikiti si mali ya watu, mtu anaweza akajenga msikiti na akauendesha kwa pesa zake au kwa michango ya waumini. Dini ni neno lenye tafsiri pana sana, itabidi ufanye utafiti ili kujua kwanza nini maana ya dini.
 
😂Basi toa ubongo wako tuone Kama utaishi...si una roho..mbona mnakuwa Kama mmeishia la pili
Kwa nni mtu ajidhuru mwenyewe ?

hata ukikatwa kichwa hautoishi kila kiumbe kina nafsi chenye kuhisi maumivu .. Ukizungumzia nadharia ya Mungu mpaka mimea na wanyama sasa kaangalie kama viumbe wote wana ubongo.
 
Tunazungumzia uwepo wa Mungu kiakili sio vitabu vilivyoandikwa na wanadamu.
 
😂😂😂Wewe unamjua na aliyetengeneza aliambiwa je ina usalama kiasi gani je alijibu vip?

Yule zombie wenu stephen hawking na uongo wake mbona kateseka kama zombie na alikuwa mzima mpaka akafa😂😂😂.

Yaani tatizo lake la kuparalyse kalishindwa mpaka kawa kama zombie ,wew unamuamini kwa kusema hamna Mungu.
 
Machafuko hayawezi yakaletwa na uislamu hata kidogo, waislamu hawawezi kufanya machafuko kwani si katika mafundisho yao. Mungu ametukataza kutoa uhai usiyokuwa na hatia, lakini ikiwa nafsi itatenda maovu yapasayo kufa basi sheria itafuata mkondo wake. Hakuna kulazimashana katika dini ya kiislamu ikiwa huiamini basi ni wewe mwenyewe unaweza usiifuate, lakini usije ukaleta fitina kwa kufanya propaganda za kuihujumu dini na wenye dini, hapo hutoeleweka. Nchi zinazofuata dini za kiislamu tunaziona zilivyo na nchi zinazofuata ukristo na dini zao tunaziona jinsi ustawi wa jamii zao. Billy Graham alipata kuandika "Ikiwa Mungu hataiadhibu Amerika, basi itabidi awaombe radhi watu wa Sodoma na Gomora" Billy Graham: 'My Heart Aches for America'
Tanzania haiendeshwi na dini lakini raia zake wana dini zao na ni kweli tunaishi vizuri tu, ila wakati mwingine wanasiasa wanawapoteza hawa waumini maboya. Taliban ni zao la amerika
View: https://www.youtube.com/watch?v=AwpR6ngoSjQ
 
Huwa nashangaa sana wanaoshupaza shingo kukataa nguvu ya uponyoji huku wakiitetea nguvu ya uharibifu kiimani,kwanini msizikatae imani zote?
 
Unaelewa roho ni nn? 😂😂 Wewe sayansi uliyosoma ni ile iliyoandikwa sio uhalisia ...Kiumbe kilichokuww hai kina roho na ndip inafanya kihisia maumivu na mambo mengine .

Kweny sayansi unaambiwa kwa binadamu ubongo ndio unatafsiri kila kitu ila bado utaambiwa ubongo ndio kila kitu ila kuna kitu kinaitwa kupumua(pumzi) 😂😂
 



Huyu alikuwa mzima😂😂na alisema hamna Mungu ,hajui kesho yake hatimae kawa zombie mpaka anakufa😂.

Mungu yupo hata wewe hujui kesho yako ..Hujafa hajaumbika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…