Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

🤣Au dragon wa Dan baker
 
Argument from inconsistent revelations... 🥺 kila mtu anasema dini yake ndo ufunuo kutoka kwa muumba na wengine wote ni waongo...🤣bac hizi dini zituendeleze Sasa mbona nchi ambazo Zina udini mchache zinaendelea
 
Huyo Allah kajiumba
 
Kuongelea kwako dhana ya Mungu kwa ujumla no ujinga na uvivu wa kufikiri sababu lazima ukosee kama ulivyo kosea hapa. Huwezi kumuongelea Ng'ombe kuwa ni Mungu wakati Mungu ili awe Mungu lazima awe na sifa zake anuani.

Hapo ulitakiwa ujue unajadiliana na mtu wa aina gani kisha ujenge hoja kwa mtizamo wake. Ulipaswa ujadiliane na Mimi kwa mujibu wa Mungu ninae muamini Mimi, na ukijadliana na Mhindu hali kadhalika.

Amemkubalia sababu amemuomba, na angetaka asinge mkubalia bali amefanya hivyo kwa hekima na kuwatahini waja wake. Lakini hakutuacha hivi hivi alitutahadharisha juu ya Shetani, maana ukishawishiwa na Shetani ujue hiyo ni hiari yako. Kwa maana hiyo chochote utakacho kihoji hapo hakiwezi kuwa na nguvu, sababu ya uwepo wa Uhuru wa kuchagua.

Naam, lakini Adamu na Hawa walipewa onyo na ndio maana Allah akawatoa, maana yake walizembea wenyewe. Duniani unapata vyote, huwezi kuishi katika huzuni maisha yako yote au katika raha, bali duniani ni mapito ndio maana Kuna kufa, Kuna kufufuliwa na kuna kulipwa.

Aya zako za mwisho hakuna hoja uliyo iweka hapo zaidi ya malalamiko, hata wakiwa zaidi ya hizo asilimia ulizo zitaja, ukweli unabaki pale pale ya kuwa wamepotezwa kwa kutaka wenyewe kupotezwa.
 
Mnyiramba wakwanza wa hovyo sana.
Hujui kitu na huna akili hata moja

Huamini kuhusu Mungu ila unaamini uchawi bogus wewe
Kama huyu jamaa ni mnyiramba ameaibisha sana kabila letu
 
Argument from inconsistent revelations... 🥺 kila mtu anasema dini yake ndo ufunuo kutoka kwa muumba na wengine wote ni waongo...🤣bac hizi dini zituendeleze Sasa mbona nchi ambazo Zina udini mchache zinaendelea
Sahihi kabisa, baada ya kuona hilo, huwa tunaenda mbali na kujadili ukweli wa hicho kinachodaiwa au kusemwa.

Mfano katika hayo maswali niliyo yaweka, Kuna uongo gani ? Jifunzeni kujadili hoja na si kukimbia hoja.

Kwamba je Dunia imeumbwa na sisi ? Au Dunia imetokana pasi na chochote ? Kumbuka haya yamenukuliwa natu ambaye hajui kusoma Wala kuandika. Kwa mwenye akili lazima atakiri ya kuwa hili si la kawaida.

Kujibu kwako maswali hayo na kutokujibu kwake kunaonyesha ya kuwa Mola yupo na Dunia hii imeumbwa.

Kuendelea kwa nchi sio lengo la sisi kuumbwa na hakimfanyi mtu awe sahihi, sababu Mola wetu huwa anawaruzuku mpaka watu waovu bali mpaka wanao mtukana na kumkana.

Jaribu kujenga hoja kijana.
 
Bado tunazunguka pale pale kama Allah hayupo basi hata hayo maagizo hayakushuka

Allah HAYUPO
Unazunguka wewe ambaye unaandika mambo ambayo unashindwa kuyajengea hoja,vukiulizwa unakimbia. Wewe thibitisha ukweli wa unayo yaandika.

Thibitisha Allah hayupo. Mpaka unakufa huwezi kufanya hivyo.
 
Haya ni mawazo yu yaliyojengeka katika falsafa.

Leta uhalisia usilete stori. Sharti sio kuamini au kutoamini, usahihi wa mambo unatakiwa ujue unachokiamini na kukikanusha, kinyume na hapo hutakiwi kupinga wala kukiri. Bado upo katika makosa tu.
 
Mosi, Wajibu wa kuthibitisha anao aliyedai uwepo wa kitu

Pili, Mtu akikwambia habari za mashaka mwitikio wa kwanza ni kutokuamini na sio kuamini
Kwahiyo kutokuamini ni msingi wa kwanza hadi kuwepo uthibitisho

PROVE IT
Hii sio kweli, bali hiki ni kichaka ambacho huwa mnajifichia wakana Mungu na hii inaonyesha ya kuwa mnapinga mambo ambayo hamna elimu nayo.

Mara nyingi anae kanusha ndio hutangulizwa sababu hudhaniwa ya kuwa ana elimu zaidi juu ya jambo hilo, na mara chache anaye kiri hutangulizwa.

Sisi tunakiri ya kuwa Mola yupo kwa sababu nyingi sana, zipo sababu za kiakili, za kimazongira na ufunuo. Sasa wewe ambaye unakuja na kusema ya kuwa "Mungu hayupo" unapewa nafasi kubwa ya kuthibitisha sababu unakuwa unaenda kinyume na Uhalisia, yaani unapingana na akili, unapingana na mazingira na unapingana na ufunuo.

Sasa hakuna mlango wa nyinyi kutoka katika kuwajibika kuthibitisha juu ya kutokuwepo kwa Mola.

Twende kazi.
 

Walau nusu ya swali ulipouliza umelijibu kuwa pamoja na kupewa manual si manual yote wanadamu wanaielewa. Na kutoielewa kwenye haini ni uthibitisho wa kutokuwapo kwa Muumba wa kila kitu.

Pili ngoja nikupe kisa kimoja cha wakati wa mtume.

Mtume ktk siku zake za mwisho wa uhai wake alikaa na baadhi ya wanafunzi wake na kuwauliza maswali matatu.

Mmoja wa wanafunzi wake alifahamaika ABU DHAR AL GIFARIY:

Alipoulizwa wewe unapenda nini ktk hii dunia.
Alisema Ninapenda vitu vitatu hapa duniani.

a. Njaa,
b. Ugonjwa,
c. Na kifo

Alipoulizwa kwann, Abu Dharr akajibu:👇🏼 a. Ninapenda njaa ili kulainisha moyo wangu.
b. Ninapenda magonjwa ili kupunguza dhambi yangu.
c. Na mimi napenda mauti kwa kuwa nimejiandaa kukutana na Mola wangu Mlezi.

Angalia hii falsafa na ndio spirit tunayoishi sisi waislam.

Kwamba pamoja na kuwa tetemeko limeua watu wema na wabaya lkn wale wema wana spirit ya kuamini amerudi kwa mola wake hali ya kuwa yuko na amani ktk nafsi na moyo wake.

Wakati ninyi kwa upande wenu mnaona ni mateso.

Same case kwa magonjwa haya dume kama canser kwa watoto
 

Nasubiri mazingira na akili mkuu
 
Unazunguka wewe ambaye unaandika mambo ambayo unashindwa kuyajengea hoja,vukiulizwa unakimbia. Wewe thibitisha ukweli wa unayo yaandika.

Thibitisha Allah hayupo. Mpaka unakufa huwezi kufanya hivyo.

Kwahiyo wewe unakubaliana kwamba kuna kibuyu cha kinyiramba kinazunguka kwenye orbit ya jua?

By default huwezi kuamini hadi uthibitishiwe

Siamini Mungu by default hadi nithibitishiwe

Kwanini unalazimisha uwepo wake kwasababu siwezi kuthibitisha uwepo wake?

MIMI SIWEZI KUTHIBITISHA KUTU AMBACHO HAKIONEKANI, HAKIHISIKI, HAKITHIBITIKI, HAKINUSIKI yaani HAKIPO
Kinasemwa tu kwenye vitabu kuna Mungu
 

Mkuu Abu Dharr alijibu vile kulingana na level yake kwa namna alivyokuwa brainwashed na Mohammed(saw)

Kuna mjinga mmoja aliwashindisha njaa waumini wake hadi kufa achilia mbali aliye wanywesha sumu na wanao jivika mabomu
 
Japo mie ninaamini mungu yupo,lkn nikiri wazi kabisa kuwa wewe ni mtu mwenye akili sana,una uweze mkubwa sana wa kujenga hoja na kushawishi.
Nashukuru sana mkuu kwa kutambua hilo, Na umekuwa muelewa.

Watu wengine huwa hawawezi kukubali ila wanataka ubishi tu.

Na waki ishiwa hoja huanza kutumia matusi, kejeli na kuni shambulia kwa lugha zisizofaa.

Siku zote, Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika,

Na kitu kikisha fahamika na kuthibitishika kipo, Hakuna haja tena ya imani kutambua uwepo wa kitu hicho.

Nikupe mfano mdogo,
Mwanafunzi anaye fanya mtihani, kabla ya matokeo kutoka anakuwa hana uhakika wa ufaulu wake utakuwaje, ila anakuwa Ana "imani" ya kwamba atafaulu, Lakini kwa vile hana uhakika vizuri hajui atafaulu kwa kiwango kipi, Pia vile vile anaweza akafeli au akafaulu kwa kiwango tofauti na matarajio ya "Imani" yake kwa vile Hana uhakika.
(Ni imani yake tu)

Lakini matokeo ya mtihani yakishatoka, Imani hiyo ya kuamini kwamba "Atafaulu au atafeli" ina ondoka na kuwa ukweli na uthibitisho wa kwamba mwanafunzi huyu "Amefaulu au Amefeli" kwa uthibitisho wa kuonekana kwenye cheti chake cha matokeo au karatasi ya mtihani aliyo jibia.

Na hapa mwanafunzi huyu anakuwa Hana "imani" tena ya kwamba "amefaulu au amefeli" kwa vile ana uthibitisho wa uhakika wa jibu moja tu, kwamba kweli amefaulu au amefeli kwa kuangalia vyeti vyake au matokeo yake ya mtihani yaliyo toka.

Imani ile ya kusema kwamba nitafaulu au nitafeli inakuwa haipo.

Hivyo msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika juu ya jambo fulani,

Ukweli Hauendani na imani.
ukweli una endana na kujua, uwepo wa uthibitisho, facts, evidences na Logic.

Yani kwenye imani hata 1+1 jibu linaweza kuwa tisa kwa imani, kwa vile ni imani tu.

Ila kwenye ukweli 1+1 jibu lazima liwe 2.
 

Kwel umeongea neno kwaiyo kbla ya wazungu na warabu kuja babu zetu walikua wakifa wanaenda motoni moja kwa moja ila baada ya wazungu na warabu kufika bas wakaja na upako na uponyaji
 
Epicurean paradox
 
@Kisai nakuuliza hivi,[emoji116]

Kwa nini Mungu wenu huyo "Allah" ana Zungumza kwa kiarabu tu?

Duniani kuna Lugha nyingi sana kijapani,kichina, kijerumani, kiingereza,kifilipino, kigiriki, kiswahili, n.k

Kuna lugha mbalimbali za makabila mengi sana ulimwenguni kote.

Sasa kwa nini Mungu wenu huyo "Allah" ana eleweka kwa kiarabu tu?

Na unadai Mungu wenu huyo "Allah" wa ninyi waislamu ndio Mungu wa kweli duniani kote.

Kama Mungu wenu Allah ndio wa ukweli kwa nini aeleweke kwa lugha moja tu ya kiarabu?

Yani kumjua Mungu huyo lazima umjue kwa kiarabu?

Mungu wenu huyo Allah, Alishindwaje kujidhihirisha kwa binadamu wote wa Lugha zote duniani aka eleweka?

Fafanua kinaga ubaga [emoji3516][emoji3516]
 
Mkuu Abu Dharr alijibu vile kulingana na level yake kwa namna alivyokuwa brainwashed na Mohammed(saw)

Kuna mjinga mmoja aliwashindisha njaa waumini wake hadi kufa achilia mbali aliye wanywesha sumu na wanao jivika mabomu
Sawa. Manual kwa maana ya Mtaala wowote kazi yake ni kukuchonga. Kukutengeneza.

Ni suala la hisia zako iwapo unakubaliana nacho au laa. Kama ninyi mulivyochongwa na kuamua kupinga manual ya maumbile ya yule aliyesababisha tuwepo na viwepo vingine.

Moja ya falsafa ya Uislam ni kutoogopa kifo iwapo unajiamini kuishi kwa kupita kwe njia ya Mungu.

Na kitu kibaya zaidi kuliko vyote ni Fitna.

Na mifumo yote iliyotungwa na wanadamu ni fitna ktk ardhi. Na universal law (uislam) umekuja kupingana na hizo fitna.

Sasa tunapigania ni kutengezwa kwa njia ya Mungu au kukumbatia fitna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…