Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Hii kanuni huwezi kuikosoa ndio maana hata hapa umeshindwa pia. Kanuni imemtoa Allah Japo na yeye ni kitu.

Kanuni inasema kila kitu isipokuwa Allah, hapo tayari imeshamtoa Allah, Sasa uongo uko wapi na kanuni Iko wazi ? Uwe unasomwa kwa kuelewa usisome ilimradi.

Nilikupa kazi hapa uje uthibitishe ukweli wa "Infinity" naona unaruka ruka tu.
 
Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu wenye kuruhusu mabaya(uovu+Majanga n. K)

Ni contradiction ama siyo contradiction?
Hii si Contradictions sababu yeye ni muweza wa yote. Hivi hiki mnachokoandika huwa mnakofikiria ?

Yaani anafanya Yale ambayo akili yako haiwezi kuyadiriki.

Onyesha Contradictions Iko wapi hapo ?
 
Aibu ya dini yako hii ambayo bado inafundisha jua linazama kwenye matope. (Quran 18:86)

Mara sperm zinatoka kwenye uti wa mgongo.

Kwamba jua linaenda kusujudu, mara mpaka liruhusiwe na Allah ndo lichomoze.

Kwamba milima imewekwa ili kufanya dunia iliyoflat isiyumbe yumbe.(21:31)

Kwamba kuna sehemu jua huwa linachomoza na huko Mungu hajawawekea hata pazia la kuwakinga nalo (18:90)

Katika karne hii, kung'ang'ania haya ni Upumbavu na si ujinga
 
Ameweza vipi kuwepo bila kuumbwa?

Nkikwambia dunia na watu hawajaumbwa bali wapo utasemaje!?

Kwanini unaongea as if tushakubaliana kuwa yupo kweli!?

Umethibitisha uwepo wa huyo Allah!?
Nani alikwambia kila kilichopo lazima kiwe kimeumbwa ?

Nilikuuliza swali, nipe sababu tatu au mbili zinazo onyesha ulazima wa kuumbwa yule ambaye ni chanzo Cha kila kitu ?

Sasa unashindwa nini kuthibitisha ya kuwa hayupo ?
 
Hii si Contradictions sababu yeye ni muweza wa yote. Hivi hiki mnachokoandika huwa mnakofikiria ?

Yaani anafanya Yale ambayo akili yako haiwezi kuyadiriki.

Onyesha Contradictions Iko wapi hapo ?
Uweza wake wote ungemfanya aumbe ulimwengu usio na mabaya.

Kama Mungu ni mwenye upendo wote kwanini anaruhusu tetemeko liue watu!?
 
Sasa kosoa hayo ili tukuone wewe ni mkweli ?

Usiruke ruke, nipo hapa nataka ianze kukosoa nukta baada ya nukta.
 
Uweza wake wote ungemfanya aumbe ulimwengu usio na mabaya.

Kama Mungu ni mwenye upendo wote kwanini anaruhusu tetemeko liue watu!?
Huo ni udhaifu, sababu anakuwa na uwezo wenye ukomo.

Ushawahi kufikiria hiki kitu ?

Sababu anataka liwe na ndio maana anaruhusu tetemeko litokee, na linatokea kwa sababu ya kuwapa adhabu au kuwakumbusha.

Ukifatilia katika haya majanga, yanayo tokea utakuta watu husika Kuna makosa wanayafanya, kwahiyo inakuja kama adhabu au uzinduo kwa yale wanayo yafanya, na huu ndio utaratibu alio uweka Allah na haubadiliki.
 
Hili nimeshalielezea Jana rejea nilicho kiandika. Nilimaliza kila kitu kuhusu hili.
 
Uweza wake wote ungemfanya aumbe ulimwengu usio na mabaya.

Kama Mungu ni mwenye upendo wote kwanini anaruhusu tetemeko liue watu!?
Hii Ni ukweli ambao ni mchungu kwa Watu kuupokea Wakasome problem of evil
 
Nani alikwambia kila kilichopo lazima kiwe kimeumbwa ?

Nilikuuliza swali, nipe sababu tatu au mbili zinazo onyesha ulazima wa kuumbwa yule ambaye ni chanzo Cha kila kitu ?

Sasa unashindwa nini kuthibitisha ya kuwa hayupo ?
Kuna ambae ni chanzo cha kila kitu!?
 
😂😂Yanatokea majanga wengine wanakufa ni njia tu ya kifo ,ila hata ukiumwa utakufa hata bila ya majnga na magonjwa utakufa.


Mungu huyo kapendelea Tanzania isipate hayo majanga makubwa mbona husemi kwamba kapendelea.

Mungu sio kwamb hawezi kuzuia ila yeye ndio kapanga hta katika hayo mafuriko sio wote wamekufa ni baadhi, majanha kama hayo yapo nje ya uwezo wetu hakuna anayependa yatokeee ila ni Mungu muweza na hakuna jinsi unaweza kuzuia.

Mungu huyo kakupendelea wewe usiwe mlemavu na kakupa akili ni neema jaribu kushuruku ,huwezi kuonq neema mpaka yakufike..

Huoni hapo umeona umuhimu wa uhai basi unapumua bure mpaka uumwe ukapewe mtungi wa oxygen uanze kulipia ndio utajua kwambq kupumua tu ni upendeleo.


Neema za Mungu ni countless na huwezi kuzijua mpaka ziondoke na ni nyingi kuliko mjanga.
 
Je unapenda kumuona mwanao unayempenda sana akiwa anataabika na magonjwa, akiwa anapatwa na ajali hadi kuwa kilema,

Unapenda wale uwapendao wafe!?
 
Je unapenda kumuona mwanao unayempenda sana akiwa anataabika na magonjwa, akiwa anapatwa na ajali hadi kuwa kilema,

Unapenda wale uwapendao wafe!?
Wewe ulitaka apate mtoto wa jirani tu sio wako.!!

Katika Dunia hii Mungu anaweza kuleta janga kwa yeyote yule na mda wowote ,mimi na wewe wote ni sawa tu ..
 
1.Radi
2.Kutokea kwa Usiku na mchana
3.Mechanism za mwili (ikiwemo sperm zinapotoka)
4.Tetemeko la ardhi
5. Sayari kuzunguka jua

We bro unachekesha sana Yani hayo ndio mamba ambayo binadamu ameweza kuyafahamu na kuyaelezea pasipo dhana ya uwezo wangu ? Nani aliyekudanganya? Wewe Wala haujasoma Sayansi hayo mambo uliyoyataja hapo yote wanasayansi wamechemka

1) RADI
Radi inatokana na mvutano wa electron zenye chaji zinazofana either zote ni +ve au zote ni -ve

Nani aliyetengeneza hizo electron wanasayansi hawana majibu

Nani amezifanya hizo electron zibebe change wanasayansi hawana majibu

Umeme wa radi wanasayansi wameshindwa kuuchukua na kutumia pia Wanashangaa jinsi ulivyo na mamilioni ya voltage

Katika hili Mungu amebaki kuwa Mungu

2) KUTOKEA USIKU NA MCHANA
Usiku na mchana unatokea Kwa sababu Dunia inajizungusha yenyewe

Wanasayansi wanasema Ili kitu kimuvu lazima kuwe na external force
External force inayoifanya Dunia uzunguke ni ipi Hadi Leo wanasayansi hawana majibu na kwanini rotation speed ya Dunia ipo constant pia wanasayansi hawana majibu

3) MECHANISM ZA MWILI
Mechanism zote za mwili zinatumia umeme Hadi Leo hii wanasayansi hawajui source ya huo umeme Nini

4) TETEMEKO LA ARIDHI
Hadi Sasa wanachujua wanasayansi ni kupima ukubwa wa tetemeko yaliyobakia yote wanabahatisha na ndio maana nchi kama Uturuki Wana wanasayansi wengi lakini walishindwa kujua tetemeko litatokea LIni , saa ngapi na Lina ukubwa gani

5) SAYARI KUZUNGUKA JUA
Ingia katika website ya NASA Kila siku wanagundua vitu vipya maana yake ni kwamba hawana majibu sahihi kuhusu mfumo wa ulimwengu

Yani kama Kuna mtu amekuambia wanasayansi wanajua Kila kitu kuhusu huu ulimwengu na viumbe wake basi amekudanganya

We endelea tu kukaa na ujinga wako kuwa hakuna Mungu

Mbona hazizuki Sayari nyingine na viumbe vingine vipya kama Kila kitu kimezuka
 
Kapendelea Tanzania isipate majanga au sio [emoji23][emoji23] maana yake nifurahi majanga yamepelekwa nchi zingine kwa wanadamu wengine ambao sio mimi si ndio?

Kapanga mafuriko ambayo yataua hadi watoto, majengo yatabomoka yatadondokea wamama wajawazito yataua watoto ambao hawajazaliwa ila anatupenda sana na ana huruma na sisi [emoji1787][emoji1787].

Kanipendelea mimi sio mlemavu; kwanini hata yule mlemavu asingempendelea kama mimi? kinachomshinda nini? au atapungukiwa nini binadamu wote akiwafanya wazima bila ulemavu?

Conclusion rahisi tu hapa yaani huyu mungu katuumba sisi kama vifaa vya kuonyeshea uwezo wake anaumiza wengine Ili wengine tuone tumependelewa halafu bado anataka tuamini anatupenda sana na anatuwazia mema kiukweli tukionana naye sio sisi wakumuomba msamaha yeye ndo anatakiwa atuombe sisi msamaha.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…