Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Wewe unayesema huyo Allah yupo mthibitishe muonekano wake.

Usilete ngonjera za Quran ambazo ni fictions stories.
Muonekano wake au kuhusu muonekano wake hili nilishalisema huko nyuma. Sisi tunamuelezea Allah kutokana na yeye alivyo jielezea kwenye kitabu chake "Qur'aan" na kama alivyo elezwa na Mtume wake Muhammad.

Katika yale yaliyo tufukia kuhusu Allah ni kuwa ana Mikono miwili yote ipo upande wa kulia, ana mguu, ana Cheka, ana kasirika, anajua, anasikia, anaona.

Ama kuhusu Qur'an kuwa ni "Fictions" mpaka unakufa huwezi kuikosoa Qur'aan, unaandika haya sababu huijui Qur'aan. Nakupa kazi hapa njoo uthibitishe ya kuwa Qur'aan ni fictions, uache utoto na kurula ruka. Nasubiri hilo, maana nyinyi naona huwa mnaandika andika mambo pasi na elimu.
 
🤣 Nimeweka mfano halisi, so far huna hoja... hoja yako ni kitabu Cha muarabu kimesema na ninaamini...so hatuwezi kuwa na serious convo
Mfano ulio uweka una makosa.

Sasa kitabu Cha Muarabu kinasema uongo ? Kwanini hamukosoi hicho kitabu mnaishia kurula ruka ? Inaonekana hata kukisoma hamjawahi kukisoma, halafu mnakuja hapa kutaka mjadala ? Mna akili kweli vijana ?

Nakosaje hoja wakati unakimbia hoja zangu na maswali yangu ?
 
Nacheka sana, naona huna Cha kuandika tena ?

Haya yote yanayotokea alishayapanga miaka elfu 50 kabla ya kuiumba hii Dunia, kwahiyo ni mipango yake tu, lianze hili lofate lile mwisho iwe hivi.

Anatumia kitabu ? Kivipi ? Kitabu ni maneno yake kwa ajili ya kuwaongoza waja wake. Tuliza akili uandike vya maana.
 
🤣So Kati ya Morocco na Tanzania wapi Kuna waislamu wengi...bana hii metric unayotaka leta ni point ya kijinga Sana...🤣
Haijalishi, huenda Morocco wakawepo wengi ila wakawa wanafanya uovu au maovu kuzidi Tanzania. Hujaona huko juu niliandika kuhusu Uislamu sahihi ?!
 
🤣Yaani we unaona ni freshi coz umedanganywa dini yako ya ukweli na wengine watachomwa...🥺kumbe mmelishwa matangopori na muarabu
Sasa si uonyeshe ya kuwa dini yangu ni ya uongo ?

Hivi unajua kanuni za mjadala ?
 
Chanzo Cha kila kitu kina kuwaje na chanzo ?
Thibitisha kwamba Allah huyo ni chanzo cha kila kitu.
 
Jibu swali, nlitegemea unapoquote unatoa jibu.

Kumbe sivyo
Sasa hapa nani anatakiwa kujibu swali ?

So umedai yamekosolewa na Geography ? Au unasahau ulicho kiandika ? Sasa tumia hiyo hiyo Geography unayo dai imekosoa ulete hoja zako tuzijadili.
 
Unauhakika na ukizungumzacho!?

Na inahusiana nini na nlichokuuliza mimi?
Rejea Sasa ulichokiandika utaona uhusiano uliopo na nilicho kiandika Mimi.

Weka nchi hapa ambayo imepishana masaa 24 na nchi nyingine.
 
Kosoa hoja kwa kutumia Geography unayo sema imekosoa.

Unaandika kama uko kijiweni, huku ukilalama.

Kumbe hata hiyo Geography huijui. Acheni kusikia sikia tu mambo.
 

Allah katika ubora wake

Yaani katoto kakifa kachanga kwenye shuruba ya kansa au taunami na bado anakasubiria hadi siku ya kiama anakapa tena mtihani kakifeli moto unakahusu
Huyu ndio Mungu mwenye upendo wote?

Kuamini ujinga huu inabidi ujitoe ufahamu
 
Binafsi yangu naona siku Utakapopatwa na #Shurba ndipo Utakaposadiki Utukufu wa Mwenyezi Mungu na Kutambua Uwepo wake,
Kwa nini Mungu huyo anatambulika tu wakati wa shurba?

Kama Mungu alitaka atambulike, aabudiwe, asadikiwe na asujudiwe. Alishindwaje kuumba Binadamu wema tu, watakao mtambua yeye yupo pasipo utata?

Na afute ufahamu wa sisi binadamu kutomtambua yeye Hayupo.

Kama Mungu huyo anaweza yote, kwa nini ajifiche? Akionekana hadharani kwamba yeye ni Mungu, itabadilisha nini yeye kuwa Mungu?
Siwezi Kulaumu wala Kushangaa maana Maisha ya Mwanadamu Duniani ni Fumbo au Mfano wa Giza (Ndiyo maana kuthibitisha hilo hatujui kinachojiri hata lisaa limoja inayofuata) kifupi hatujui kesho yetu.
Kama unakiri kwamba maisha ya mwanadamu duniani ni fumbo, Na hatuwezi kujua wala kuthibitisha kinachojiri, Na hatujui kesho yetu..👇

Sasa, Ni nani aliye jua kwamba Mungu huyo yupo?

Huyo aliyesema Mungu yupo,Alijuaje na ali thibitishaje Mungu huyo yupo?

Maana, si binadamu wote hatujui kesho yetu wala kinachojiri mbele yetu.

Aliyesema Mungu yupo yeye aliwezaje kufahamu hilo?

Alimwona wapi huyo Mungu?
Kama mwenyezi Mungu alitaka tumfahamu yeye yupo, Alishindwaje kuumba Binadamu watakao mtambua yeye yupo kwa wakati wote?

Na kufuta ufahamu wa sisi binadamu kutomtambua yeye Hayupo?
 

Unajaribu kusema nini mkuu?

Mimi kutokua na lakufanya kuna uhusiano gani na kuwepo kwa Mungu?

Niliaminishwa kuhusu mungu wa upendo wote ndio nikaanza kujiuliza why aruhusu haya maswahibu kwa vitoto vichanga visivyo na hatia?
 
Hatujawahi kumpangia ila wewe ndio unampangia maana kama majanga analet yeye ,wewe unataka pasiwe na majanga huoni kama unampangia?

Ushaambiwa mambo yote hapa duniani anapanga yeye 😂,wwe nawe unataka yale unayotaka wewe na haiwezekani.
 
Logical non sequitur

Narudia swali langu!!

Kwanini Mungu mjuzi wa yote atake kutupima ilihali anajua hata matokeo?

Je Mungu si mjuzi wa yote!??
Binadamu ana akili na anaweza kupambana na mitihani na amempa akili ...

Sio kila mtihani unapelekea wewe kufa mengine ni kuvumilia kama ugonjwa unaweza kuvumilia mpaka ukapona ,kama kifo kimepangwa basi haina shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…