Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Wanasayansi wanavyosema binadamu ametokana na sokwe unaamini ni kweli
 

Na wewe huoni ni utoto tu kudhani Mungu yupo tu, Hana mwanzo wala mwisho?

Nilisha kwambia kwamba uki anza kuweka ulazima wa dunia iwe na mwanzo na mwisho, Basi hata huyo Mungu lazima awe na mwanzo na mwisho.

Ili muundo wa ulazima huu ufuatwe, pasiwepo kitu chochote kilicho jitokeza chenyewe tu pasipo mwanzo.

Kama una amini Mungu yupo tu, Unashindwaje kuamini pia yai lipo tu?

Je na wewe sio utoto huo, kuamini Mungu yupo tu bila chanzo?
Kama ni utoto kuamini dunia ipo tu, Basi pia ni utoto kuamini Mungu yupo tu.
 
Wakisema wapo nitahoji, ili nipate ushahidi juu wa jambo hilo.

Kama siwajui nitaulizia ili niwajue, na katu siwezi kudai hawapo kisa siwajui.

Wapi sijajenga hoja ?

Naamini uwepo wa Yesu mwana wa Maryam, ama kuhusu Kristo inabidi mlete ushahidi mtuambie, tamko Ukristo limekuja lini au limeanza lini ? Je Yesu akisema yeye ni Kristo au ?

Jalia ningekuwa siamini, katu nisinge kuanusha uwepo wake au kutokuwepo kwake mpaka nipate elimu sahihi kuhusu viwili hivyo au kimoja wapi.
 
Nani kijana?

Njia aliyotumia, kwa mtazamo wako (yaani kumuua) ni ya upendo?

Je, ni ya huruma au ni ya ukatili?
Je, itafurahisha au itahuzunisha ndugu, marafiki na jamii.
Unaweza kuwa kijana au mtoto kutokana na uchache wako wa maarifa hata kama una miaka zaidi ya 80. Na unaweza kuwa mkubwa ki maarifa hata kama Nina miaka chini ya 30.

Naam, kifo ni haki ya kila mtu aliye hai. Bali ni hatua katika Ile safari ya kutafikia malengo yetu. Sasa utasemaje sio upendo na mtu unapata stahiki yako yaani haki yako ?

Haijalishi italeta huzuni au furaha, kifo ni muda tu, ndio maana tunaambiwa kila nafsi itaonja umauti. Mtoto akifa utotoni ujue huo ni wakati wake umefika, akipangiwa kufa kwa janga au kuumwa kama sababu basi hiyo haiepukiki.
 
🤣Hata brahma kasema ameumba mbingu ardhi na kila mtu...hata Zeus pia...so lazma mmoja awe mkweli au wote wawe wanadanganya
Kusema sio hoja, hata wewe unaweza kusema hilo. Shida inakuja kuthibitisha ukweli wa hilo.

Nitakuuliza Brahma alisema haya wapi na lini ?

Ili ujue ukweli, unatakiwa usome Historia za hao miungu na watu ambao wanawaelezea hao Miungu. Mfano wa haraka na mwepesi ni kuhusu Zeus, huyu anatajwa na Wagiriki, ukisoma habari za Wagiriki ni watu ambao waliacha ufunuo na kufata akili zao na matamanio yao, ndio wakaja kutofautiana juu ya ni nini chanzo Cha Maisha ? Wapo walio sema Moto, wapo waliosema Moshi, wapo waliosema Hewani, ilimradi kila mmoja alitoa maelezo yake kwa anavyo ona yeye.

Lakini anatajwa kama ni mtu. Maana yake tu kwa sifa yake hii hawezi kuwa Mungu huyu.
 
Sasa si uthibitishe ya kuwa haliendi na utuambie umejuaje kama haliendi. Mbona rahisi sana kijana.

Unapo Pinga kitu fulani sisi tunakudhania ya kuwa unaelimu kubwa juu ya kitu hicho, kwahiyo unatakiwa kututhibitishia ukweli ulivyo. Sasa haya malalamiko unayo leta hayaleti maana, unapoteza muda kwenye hakuna.
 
Msingi wa Sayansi ni nini kijana ? Maana usiipe Sayansi kazi ambayo Haina uwezo wa kuifanya.

Sasa ulisema hivyo unatakiwa ulete ushahidi hizi unazoandika wewe ni stori za wanasayansi, ambazo haina ushahidi wowote.

Nakuuliza swali dogo, ili ujue ukubwa kitu na mlinganisho wake kwa kingine au vingine, unatakiwa uzingatie vitu gani ?
 
Nimeuliza kama kitendo cha mzazi kumuua mtoto wake kitakua cha upendo. Je, kitakua cha huruma? Je, kitakua cha furaha kwa ndugu, marafiki na jamii?

Unajibu kifo ni haki ya mtu aliye hai.
Haijalishi kinaleta huzuni au furaha.
Mara mtoto akifa ujue huo ni wakati wake umefika.

Hapo umejibu swali gani kati ya niliyo kuuliza?
 
Infropreneur ngoja nisake ugali kwanza jioni nitarudi kuendelea na huu mnakasha.

Dunia ipo tu bila ya kusudio la kuwepo kwake. Kuwaza hivi ni utoto.

Ni sawa na kusema eti binadamu yupo tu bila ya kusudio la kuwepo kwake.

Huu Muundo tata wa maumbile ya binadamu inasadifu kweli kusema kwamba upo tu bila kusudio.

Yaani mwanaume awe na uume na mwanamke awe na uke usifanana na uume halafu ukawa unaingiliana bila ya kusudio?

Ipo tu kwamba mwanaume ana mbegu halafu mwanamke akawa na mji wa uzazi?

Ipo tu mtoto anavokuwa na kuzaliwa baada ya miezi Tisa na kuanza kukua.

Hivi si utoto kudhani kuwa hakuna mbunifu wa maumbile hayo?

Yaani dunia ipo inajiendesha yenye kiuyakinifu Kwa mfumo ambao upo tu.

Yaani majira ya ulimwenguni yapo tu na hayana kusudio la kuwepo kwake?

Mito kutirirsha maji Baharini ni kanuni ambayo ipo tu haina kusudio?

Unapanda mbegu Moja ya Hindi mhindi unabeba mahindi yenye mbegu mamia toka kwenye mbegu hiyo Moja Kwa nasibu tu!?

Unasema sayansi kama ilivyo Imani ya kuamini Kuna Mungu haina majibu yote. Ila wewe unayeamini hakuna Mungu ndiye mawazo yako ni kamilifu na timilifu??!! KWA NINI??
 
Je ni lazima kwamba kila kilichopo kwenye maandishi ni uthibitisho?

Wewe unasema uthibitisho wa "Allah" kuwepo ni Quran kwa vile eti, ime andikwa hivyo.

Ila uki ambiwa Ukristo umeandikwa kwenye Biblia una anza kubisha bisha, kwa vile si maandiko ya dini yako.

Sasa je, Biblia sio uthibitisho wa uwepo wa ukristo?

Kama sivyo, Wewe kwa nini unataka kulazimisha Quran iwe ni uthibitisho wa uwepo wa huyo Allah?

Yani unajenga hoja kwa kutetea imani yako tu.

Na kuita dini yako na hiyo Quran kwamba eti ndio uthibitisho.

Je nikisema kwamba Biblia ndio uthibitisho wa uwepo wa Mungu utakubali?
 
Infropreneur ngoja nisake ugali kwanza jioni nitarudi kuendelea na huu mnakasha.

Dunia ipo tu bila ya kusudio la kuwepo kwake. Kuwaza hivi ni utoto.
Na mimi nakwambia hivi, Kuwaza Mungu yupo tu ni UTOTO.
Ni sawa na kusema eti binadamu yupo tu bila ya kusudio la kuwepo kwake.

Ukianza kuweka ulazima wa kusudio la uwepo wa binadamu, Basi pia lazima uweke kusudio la uwepo wa Mungu.
Huu Muundo tata wa maumbile ya binadamu inasadifu kweli kusema kwamba upo tu bila kusudio.

Ndio upo tu bila kusudio, kwa vile hatuwezi kujua tusicho kujua.

Ukianza kusema unajua kusudio lipo, lazima uthibitishe kusudio hilo lipoje na liliwezaje kuwepo?

Na kusudio la kusudio hilo liliwezaje kuwepo, ili muundo ule ule wa ulazima kuwepo kusudio ufuatwe.
Yaani mwanaume awe na uume na mwanamke awe na uke usifanana na uume halafu ukawa unaingiliana bila ya kusudio?
Ndio inawezekana kabisa, si lazima kusudio liwepo.

Ukianza kuweka ulazima wa kuwepo kusudio hilo, Basi hata kusudio hilo lazima liwe na kusudio lake.

Na makusudio mengi to infinity....
Ipo tu kwamba mwanaume ana mbegu halafu mwanamke akawa na mji wa uzazi?

Ndiyo ipo tu, kwa vile hatujui Tusicho kijua.

Ila ukianza kusema unajua, lazima uthibitishe unajuaje na umejuaje.
Ipo tu mtoto anavokuwa na kuzaliwa baada ya miezi Tisa na kuanza kukua.
Ndio ipo tu, ila kama unadhani kuna kitu kinafanya mtoto huyo azaliwe.

Lazima uki thibitishe.
Hivi si utoto kudhani kuwa hakuna mbunifu wa maumbile hayo?
Kwanza, kwa nini unadhani mbunifu huyo yupo?

Au kwa nini una lazimisha awepo?

Umewezaje kuamini mbunifu huyo ambaye hujawahi kumuona na humjui, kwamba yupo na hana mbunifu wake pia?

Ila unashindwa kuamini Maumbile haya hayana mbunifu, Na una lazimisha awepo mbunifu usiye mjua?
Yaani dunia ipo inajiendesha yenye kiuyakinifu Kwa mfumo ambao upo tu.
Ndio ipo hivyo.

Wala hakuna ulazima wa kuwepo muongozaji.
Yaani majira ya ulimwenguni yapo tu na hayana kusudio la kuwepo kwake?

Ndio majira ya ulimwengu yapo tu.

Na si lazima yawe na kusudio.

Ukianza kuweka ulazima wa kuwepo kusudio hilo lazima pia kusudio hilo liwe na kusudio lake.
Mito kutirirsha maji Bahari ni kanuni ambayo ipo tu haina kusudio?

Ndio ipo ni kanuni ambayo ipo tu.

Si lazima kuwepo kusudio.
Unapanda mbegu Moja ya Hindi mhindi unabeba mahindi yenye mbegu mamia toka kwenye mbegu Hiyo Moja Kwa nasibu tu!?
Si lazima awepo anaye fanya mbegu moja ya mahindi itoe mahindi mengi.

Uki anza kuweka ulazima huo, Basi hata hilo kusudio lazima liwe na anaye lifanya.
Unasema sayansi kama ilivyo Imani ya kuamini Kuna Mungu haina majibu yote. Ila wewe unayeamini hakuna Mungu ndiye mawazo yako ni kamilifu na timilifu??!! KWA NINI??
Kwa sababu hatuwezi kujua tusicho kijua.
(Nili kufafanulia jana, kupitia theory ya Einstein relativity) Rudi tena kasome vizuri post yangu ile.

kwamba "The rate at which time passes depends upon your frame of reference"

kwamba , vitu vyote utakavyo vijua ni vile tu, utakavyo vijua kwanzia kuzaliwa kwako mpaka kufa kwako.

nje ya hapo Huwezi kuelezea kitu chochote pasipo USAIDIZI na marejeleo ya WATUNGULIZI wako.

mfano kwa sasa, Hatuwezi kujua mwaka 7090 utakuwa vipi, kutakuwa na nini?

kwa vile hapo ni nje ya "Frame of our reference"

Tutafanya makadirio tu(predictions) lakini hatuwezi kujua exactly, mwaka huo wa 7090 utakuwa vipi.

Vivyo hivyo atakaye sema anajua chanzo cha ulimwengu, Lazima aseme "frame of reference" yake ni ipi? Na athibitishe, sio mawazo yake ya kufikirika tu.
 
Nacheka sana.

Shughuli yangu unalijua, utakimbia huu uzi.

Shida sipotezi muda na wewe, sababu hujawahi kuwa na hoja.
Ukidanganya lazima nikuumbue , Allah anapanga kabla hujazaliwa , ata wewe unaweza Kuta kashakupangia moto , ata usali uruke sarakasi haitakusaidia

  • Kuna kisa Al Khidr alimuua Mtoto wa kiume , Muhammad kaelezea wazi huyu mtoto alipangiwa na Allah atakuwa Kafir, allah alimpangia atakuwa Kafir na akapanga auliwe kwa sababu kampangia hivyo, na dogo akachinjwa kikatili
    • Koran 18:80. Na ama yule kijana, wazazi wake walikuwa ni Waumini. Tukakhofu asije watia mashakani kwa uasi na ukafiri.
      • Prophet (ﷺ) said: "The boy that Al-Khidr killed was destined to be a disbeliever the day he was created.'" Jami` at-Tirmidhi 3150
 
Appreciation is not Easy sometimes ila Hapo hapo inatosha wewe tunakuweka pending acha tudili na wengine sasa
 
We Can never learn anything from the Atheist perspective. They just have nothing to stand for coz literally you can't say that something is as it is simply bcoz it's as it is 🤣
 
Umewahi kuona, Kushika au kuisikia HEWA ?
 
Vivyo hivyo kuhusu Mungu, Ukiwa na imani "utahisi uwepo wake"
 
Kama hauamini kuhusu rohoni, njia moja rahisi ambayo unaweza kuifanya hata wewe, pitia mafunzo ya meditation then ulete mrejesho hapa,
Kwamba ile hali unayoipitia wakati wa meditation ni hali gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…