Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Huyo aliyenusurika Mungu hakupenda hao wengine kama wamekufa basi ilipangwa.So ma mia wanapigwa Risasi kila siku Mungu hawapendi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo aliyenusurika Mungu hakupenda hao wengine kama wamekufa basi ilipangwa.So ma mia wanapigwa Risasi kila siku Mungu hawapendi
Wanasayansi wanavyosema binadamu ametokana na sokwe unaamini ni kweliLogical non sequitur
Mbona hakuna Mungu wala shetani ila bado tunaweza kupima mema na mabaya!?
Logical non sequitur
Wewe umeathirika na mapokeo ya dini.
Unataka kusema kuwa ubaya ni lazima awepo shetani!?
Habari ya lipi jema lipi baya ni tafsiri ya ubongo tu.
Kigezo cha kujua hayo ni kupima mambo ambayo ukifanyiwa wewe utafurahi ama utachukia.
Logical non sequitur
Ninaweza nikawa siamini na nkauchukia ama nisiuchukie ushoga.
Issue ni tafsiri ya ubongo.!!
Unauhakika na madai haya!?
Kwasababu ulimwengu unatanuka kila siku, inaonesha kabisa kuwa Ulimwengu ulianza katika nukta ndogo na ulikuwa na kiwango kikubwa cha nishati kilichojaa katika eneo dogo sana ndio ukaanza kutanuka.
ulimwengu wetu ulianza kutoka hali ya joto na mnururisho mwingi sana miaka bilioni kama 13.8 iliyopita.
Kisha, ghafla ulimwengu ulianza kupanuka kwa kasi kubwa.Hii ilisababisha joto na nishati kuanza kupoa na kuruhusu atomi na molekuli kuunda na kutokea. Baada ya mamilioni ya miaka, ulimwengu ulianza kuwa na muundo unaofanana na ulivyo leo, na nyota, sayari, na vitu vingine vyote vilivyopo katika ulimwengu wetu vilianza kutengenezeka
kugunduliwa kwa mnururisho wa cosmic microwave background (CMB) na uwezo wa kuona ulimwengu ukiongezeka kwa kasi kwa kutumia darubini za anga ni ushahidi wa madai haya.
Viumbe vimetokea vyenyewe,
reaction mbalimbali za kikemia zilisababisha viumbe kutokea
Vitu kama RNA, DNA vilitangulia.
Miller experiment ilikuwa jaribio la kujaribu kuelewa jinsi molekuli za kikaboni zinaweza kuundwa katika hali ya zamani ya dunia, inayofanana na ile iliyokuwepo kabla ya kuwepo kwa uhai. Experiment hii ililenga kujenga hali ya "dunia ya zamani" katika maabara na kuchunguza ikiwa hali hiyo inaweza kutoa molekuli za kikaboni, ambazo ni muhimu kwa uhai.
Miller alianzisha mfumo wa maabara uliokuwa na viungo vya kemikali muhimu katika ulimwengu wa zamani, kama vile methane (CH4), ammonia (NH3), maji (H2O), na hidrojeni (H2). Kisha alitumia umeme kuigiza umeme wa radi katika anga la zamani ya dunia.
Baada ya siku kadhaa za majaribio, Miller aligundua kuwa mfumo wake ulikuwa umetengeneza asidi amino, ambazo ni vitengo muhimu vya kujenga protini, molekuli muhimu kwa uhai. Hii ilikuwa ni moja ya ushahidi wa awali wa jinsi molekuli za kikaboni zinaweza kuundwa kutoka kwa viungo vya kikemia katika mazingira yanayofanana na yale ya zamani ya dunia.
Sisi ni binadamu na sio ng'ombe Because of Natural selection.
Unaweza kuthibitisha Mungu wako yupo?
Masikini ,muone na huyu na utakuta kaenda shule ,hawa jamaa ni washezi sana walitufanye ushenzi mkubwa ,walaaniweMm nakuongezea ww ni mwendawazimu
Jifunze kujibu hoja.
Jee hakuna sababu maalum ya watu kuongezeka?
Mnasema Kila kitu Lazima kiwe na chanzo, au siyo?
Kwa miaka Mingi wapinga Mungu walikuwa wanajadili kati ya Yai na kuku kipi kimetangulia?
Mwisho Wa siku wamekuja kusema kuwa Yai ndio limetangulia. Wakiulizwa Yai nalo limetoka wapi Wanasema eti lilikuwepo tu!!!
Hivi siyo utoto kudhani kuwa dunia ipo tu haina Mwanzo Wala mwisho??
Kama ni utoto kuamini dunia ipo tu, Basi pia ni utoto kuamini Mungu yupo tu.Hofu ni kusema kama Ina Mwanzo basi Lazima isemwe ilianzaje, na ukisema ilianzaje itabidi ukiri yupo aliyeanzisha na kama Ina mwisho mwisho wake utakuwaje.
Nadharia nyingi mnazotumia kupinga kwamba Kuna Mungu ni za kukariri toka watu wengine na ndiyo maana mkiulizwa maswali rahisi mnasema ni maswali ya kitoto.
Wakisema wapo nitahoji, ili nipate ushahidi juu wa jambo hilo.Hivi kwani kila kisemwacho kipo, lazima kiwepo?
Wakristo waki kuambia wewe Kisai "Yesu na Bikira Maria" wapo utakubali kwamba wapo kwa vile umeambiwa wapo na umesikia wapo?
Kama huwajui "Yesu na Bikira Maria" je ni kwamba hawapo au wapo?
Inaonekana una tetea sana dini yako ya uislamu, Hujengi hoja.
Niambie una amini uwepo wa Yesu kristo?
Na kama huamini, je ni kwamba Yesu huyo hayupo?
Unaweza kuwa kijana au mtoto kutokana na uchache wako wa maarifa hata kama una miaka zaidi ya 80. Na unaweza kuwa mkubwa ki maarifa hata kama Nina miaka chini ya 30.Nani kijana?
Njia aliyotumia, kwa mtazamo wako (yaani kumuua) ni ya upendo?
Je, ni ya huruma au ni ya ukatili?
Je, itafurahisha au itahuzunisha ndugu, marafiki na jamii.
Nacheka sana.Nimemaliza , danganya kwenye Uzi ambao sipo
Kusema sio hoja, hata wewe unaweza kusema hilo. Shida inakuja kuthibitisha ukweli wa hilo.🤣Hata brahma kasema ameumba mbingu ardhi na kila mtu...hata Zeus pia...so lazma mmoja awe mkweli au wote wawe wanadanganya
Sasa si uthibitishe ya kuwa haliendi na utuambie umejuaje kama haliendi. Mbona rahisi sana kijana.🤣🤣🤣Watu washakuchoka wewe...Kama unatetea ujinga eti jua linaenda kuomba ruhsa kwa Allah usiku ili lichomoze... unategemea nani atakaa kubishana na wewe...we pekee ndo unabaki kutetea dini yako ya mchongo... wenzako wanatetea uumbaji something outside religion we bado unakomaa na pedophile mudi
Msingi wa Sayansi ni nini kijana ? Maana usiipe Sayansi kazi ambayo Haina uwezo wa kuifanya.Tofautisha Muhammad aliyejua jua linazunguka dunia afu nyota ni mapambo na silaha za kupiga mashetani wasikaribie the throne of allah na wanasayansi waliothibitisha jua ni nyota. Wewe na elimu yako ya 690 AD huwezi elewa ukiambiwa nyota zile zipo mbali sana ndo maana zinaonekana vile na kuwa jua ni dogo compared to hizo nyota
Nimeuliza kama kitendo cha mzazi kumuua mtoto wake kitakua cha upendo. Je, kitakua cha huruma? Je, kitakua cha furaha kwa ndugu, marafiki na jamii?Unaweza kuwa kijana au mtoto kutokana na uchache wako wa maarifa hata kama una miaka zaidi ya 80. Na unaweza kuwa mkubwa ki maarifa hata kama Nina miaka chini ya 30.
Naam, kifo ni haki ya kila mtu aliye hai. Bali ni hatua katika Ile safari ya kutafikia malengo yetu. Sasa utasemaje sio upendo na mtu unapata stahiki yako yaani haki yako ?
Haijalishi italeta huzuni au furaha, kifo ni muda tu, ndio maana tunaambiwa kila nafsi itaonja umauti. Mtoto akifa utotoni ujue huo ni wakati wake umefika, akipangiwa kufa kwa janga au kuumwa kama sababu basi hiyo haiepukiki.
Je ni lazima kwamba kila kilichopo kwenye maandishi ni uthibitisho?Wakisema wapo nitahoji, ili nipate ushahidi juu wa jambo hilo.
Kama siwajui nitaulizia ili niwajue, na katu siwezi kudai hawapo kisa siwajui.
Wapi sijajenga hoja ?
Naamini uwepo wa Yesu mwana wa Maryam, ama kuhusu Kristo inabidi mlete ushahidi mtuambie, tamko Ukristo limekuja lini au limeanza lini ? Je Yesu akisema yeye ni Kristo au ?
Jalia ningekuwa siamini, katu nisinge kuanusha uwepo wake au kutokuwepo kwake mpaka nipate elimu sahihi kuhusu viwili hivyo au kimoja wapi.
Na mimi nakwambia hivi, Kuwaza Mungu yupo tu ni UTOTO.Infropreneur ngoja nisake ugali kwanza jioni nitarudi kuendelea na huu mnakasha.
Dunia ipo tu bila ya kusudio la kuwepo kwake. Kuwaza hivi ni utoto.
Ni sawa na kusema eti binadamu yupo tu bila ya kusudio la kuwepo kwake.
Huu Muundo tata wa maumbile ya binadamu inasadifu kweli kusema kwamba upo tu bila kusudio.
Ndio inawezekana kabisa, si lazima kusudio liwepo.Yaani mwanaume awe na uume na mwanamke awe na uke usifanana na uume halafu ukawa unaingiliana bila ya kusudio?
Ipo tu kwamba mwanaume ana mbegu halafu mwanamke akawa na mji wa uzazi?
Ndio ipo tu, ila kama unadhani kuna kitu kinafanya mtoto huyo azaliwe.Ipo tu mtoto anavokuwa na kuzaliwa baada ya miezi Tisa na kuanza kukua.
Kwanza, kwa nini unadhani mbunifu huyo yupo?Hivi si utoto kudhani kuwa hakuna mbunifu wa maumbile hayo?
Ndio ipo hivyo.Yaani dunia ipo inajiendesha yenye kiuyakinifu Kwa mfumo ambao upo tu.
Yaani majira ya ulimwenguni yapo tu na hayana kusudio la kuwepo kwake?
Mito kutirirsha maji Bahari ni kanuni ambayo ipo tu haina kusudio?
Si lazima awepo anaye fanya mbegu moja ya mahindi itoe mahindi mengi.Unapanda mbegu Moja ya Hindi mhindi unabeba mahindi yenye mbegu mamia toka kwenye mbegu Hiyo Moja Kwa nasibu tu!?
Kwa sababu hatuwezi kujua tusicho kijua.Unasema sayansi kama ilivyo Imani ya kuamini Kuna Mungu haina majibu yote. Ila wewe unayeamini hakuna Mungu ndiye mawazo yako ni kamilifu na timilifu??!! KWA NINI??
Ukidanganya lazima nikuumbue , Allah anapanga kabla hujazaliwa , ata wewe unaweza Kuta kashakupangia moto , ata usali uruke sarakasi haitakusaidiaNacheka sana.
Shughuli yangu unalijua, utakimbia huu uzi.
Shida sipotezi muda na wewe, sababu hujawahi kuwa na hoja.
Appreciation is not Easy sometimes ila Hapo hapo inatosha wewe tunakuweka pending acha tudili na wengine sasaI don't kwa kweli...🤣Ila hii ni issue ya personal belief Kama timu ya kushabikia. It can be any team coz zote Zina ubora wake. Same as the cosmological argument... Ila kusuppose kwamba ur god of ur religion ameumba kila kitu na amekutokea wewe na anatupangia wote pa kumwagia..🤣hapo I'll have a problem
Umewahi kuona, Kushika au kuisikia HEWA ?Mkuu,
Kisicho kuwepo Haki hitaji uthibitisho wa kutokuwepo kwake kwa vile hakipo kwa namna yoyote ile ya kuonekana, kusikika au kushikika.
Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo either ya kuonekana, kusikika au kushikika.
Sasa Mungu hayupo kwa namna yeyote ile, Haonekani, Hashikiki wala Hasikii.
Ni dhana ya kufikirika tu, imaginations just an illusion.
Vivyo hivyo kuhusu Mungu, Ukiwa na imani "utahisi uwepo wake"Bibilia haijaandikwa na Mungu ndugu yangu imeandikwa na binadamu kama wewe
Kumfananisha “Mungu muweza wa yote” na upepo ni kumshushia heshima kwa mnao muamini
Upepo unasikika, upepo una uhisi, upepo unapimika, upepo unatengenezeka
Halikadhalika hewa inapimika, inatengenezeka nk nk
Mungu hayupo hivyo hakuna chochote kuhusu Mungu zaidi ya vitabuni
Kama hauamini kuhusu rohoni, njia moja rahisi ambayo unaweza kuifanya hata wewe, pitia mafunzo ya meditation then ulete mrejesho hapa,Hiyo “kiroho” si ingewekwa wazi na rahisi kwa watu wote kumjua huyu Mungu?
Hapo “kirohoni” ni kichaka kingine cha kumfichia Mungu
Yaani uki assume Mungu yupo halafu uanze kutafakari ukuu wake na yanayojiri hata wanao amini katika Mungu wenyewe wanaona kweli hai make sense
Ndio hapo sasa wanakuja na kichaka kingine eti kirohoni
Hiyo kirohoni yenyewe concept yake ni kama ya Mungu tu..... HAIPO