Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

🤣🤣🤣🤣bac sawa mkuu hayupo kwa sababu hujanipa evidence ya uwepo wake...na nanasi kuwa tamu au Tako kuwa zuri sio evidence
Bado hujajibu swali langu, umejuaje ya kuwa Mungu hayupo ? Mpaka ukaanza kumkana ?

Usikimbie swali la msingi.

Suala la nanasi kuwa tamu na Tako kuwa zuri, hiyo ni kazi ya Mola muumba aliye viumba viwili hivyo. Hili tutalijadili wakati wake ukifika.
 
🤣bac na ulimwengu haujawahi kutokuwepo so hauhitaji muumba wako...thank u
Thibitisha hilo, usilete hitimisho la kimantiki, hitimisho la kitoto na uvivu wa kufikiria.

Ulimwengu ulitanguliwa na kutokuwepo kisha ukawepo ila kwa Mola hajatanguliwa na chochote.

Sasa msiletw ulinganyo kwa visivyo fanana ukahitimisha kitoto. Mungu aliyeumba na Ulimwengu ulio umbwa ni viwili visivyo fanana.
 
🤣Kitabu gani hiko...wakati mkikanwa ndo wakwanza kuandamana kupiga watu mawe kulipua maghorofa kuuwa etc.... hata mtoto wa la Saba ambae hajazaliwa katika dini yoyote akipewa vile vitabu anasoma anacheka kabisa
Halafu unataka kujadiliana kuhusu Mungu ?

Kitabu Qur'aan,suala la kuandamana na kupiga watu mawe hili Lina maelezo yake, na najiuliza hapa limeingiaje ?

Kucheka sio hoja, hoja kimeandikwa nini ? Maana hata huyo mtoto atakuwa na shida katika akili ndio maana akaitwa mtoto.

Mkiwa mnataka kujadili hizi mada, hakikisheni mnamjua Mungu ambaye mnamkana sio mnabanwa mnaruka ruka tu. Mnapotezea watu muda.
 
Ila ni nani!?
Hakuna muumbaji.

Dunia imekuwepo tangu enzi na enzi.

Kama kila kitu lazima kiwe na Muumbaji basi hata huyo Mungu lazima awe na muumbaji.

Na muumbaji wa Mungu, awe na muumbaji wake. Ili kanuni hii ya "lazima awepo muumbaji" ifuate muundo wake wa ulazima huo.

Hapa sasa kutakuwa na Endless ya waumbaji
( waumbaji wasio na mwisho) ili muundo wa ulazima huo ufuatwe.
 
Jibu swali nililo kuuliza kijana.

Swali hili?

Kwahiyo miungu hao ndio wameumba hii Dunia ?

Yes,

Au unadhani ni Mungu wako tu ndio anadaiwa kaumba dunia na kila kitu?

Nimekwambia una muamuni mungu wako kwakuwa umezaliwa na kulelewa na kuwa brainwashed toka utotoni
Ungezaliwa na wahindu uhundini ungekuwa budha na ungekomaa kumtetea mungu wa kihindi...... huu ni ushahidi tosha HAKUNA MUNGU isipokua tunarithishana zana ya Mungu
 
Thibitisha madai yako.

Kumsingizia mtu maneno bila uthibitisho ni jambo baya sana.

Kwa nini unaona kila anayehojibuwepo wa Mungu ni Kiranga wakati hizi habari zilikuwepo maelfu ya miaka kabla mimi sijazaliwa?

Yani kila anayehoji uwepo wa Mungu hapa ni Kiranga?

Huoni kwamba hapo unajionesha ujinga wako tu?

What the fvck?
Hahaha

Jamaa anakushushia na lawama kabisa.

Tatizo unaweza kukuta mtu kaishi kwenye echo chamber, internet aliyonayo haitumii kumtoa humo apate concepts mpya, then anakutana na atheistic comments za kiranga humu jf for the first time, hapo lazima akuone stranger na baba wa atheism duniani 😂😂😂
 
Swali la msingi liko pale pale, umejuaje ya kuwa hakipo ? Mfano rahisi sana wewe unakijuaje kitu ambacho hakipo ? Maswali marahisi yanawashinda.

Kutokuwepo kwa Mungu ni ushahidi wa kutokuwepo kwa Mungu

Kama hakuna chakula kwenye meza ni ushahidi kwamba hakuna chakula kwenye meza.... PERIOD

Post yangu # 1 nimeeleza kwanini dhana ya Mungu ni uongo
Nilitarajia utapangua hoja ka hoja
 
N
Ndugu tunapobishania haya na wewe hebu leta Facts zako (NB: Zisiegemee kwenye Imani) ya Kwamba hivi vitu (Dunia, Jua, Binadamu nk) vinatoka wapi? Usiishie tu kusema ni Nature!!
Mimi nimekwambia kwamba Vitu hivi chanzo chake ni Mwenyezi Mungu na ukiniuliza chanzo cha huyo Mwenyezi Mungu ntakwambia yeye alikuwepo toka enzi na enzi (reference from the holly books).
Sasa na wewe unaposema hivi vitu ni nature jaribu kuonyesha mfano inakuwaje kama binadamu chanzo chake ni Nature Kwanini binadamu huyo huyo anapojaribu kuImmitate nature hiyo ashindwe hali ya kuwa vingine aweze,, Sababu ni nini???
Naomba tuelewane kitu.

Usipokielewa kitu haimaanishi ni Mungu.

Usipoelewa jua limetoka wapi huo ni uthibitisho tu kuwa huelewi jua limetoka wapi, na kushindwa kuelezea jua limetoka wapi haimaanishi kuwa limetengenezwa na Mungu.!
Inawezekana ikawa sababu/chanzo ni kitu kingine kabisa ambacho wewe hukijui.

Watu wameamua kuamini tu hivyo hivyo ili kuwa comfortable na majibu wapewayo, Hawakubali kuwa weupe kichwani kwa kukubali kuwa hawana maarifa.
Na hiyo ni dhana ya Mungu wa kufukia mashimo ya ujuzi (God of gaps)

Kama unadai jibu lako la kwamba jua limetoka kwa Mungu bhasi thibitisha Mungu yupo ili jibu lako liwe halali.!!
 
Bado hujajibu swali langu, umejuaje ya kuwa Mungu hayupo ? Mpaka ukaanza kumkana ?

Usikimbie swali la msingi.

Suala la nanasi kuwa tamu na Tako kuwa zuri, hiyo ni kazi ya Mola muumba aliye viumba viwili hivyo. Hili tutalijadili wakati wake ukifika.
Huhitaji kuthibitisha kisicho kuwepo. Ila kile ambacho kipo kinaweza kuthibitishwa uwepo wake.
 
Huu uongo ulitengenezwa kwa lengo la ku control binadamu... vinginevyo duniani pasinge kalika.
 
Thibitisha kwamba miungu wao wameumba hii Dunia. Kingine utuambie kitu ili kiumbe kinatakiwa kiwe na sifa gani ?
Nimekwambia una muamuni mungu wako kwakuwa umezaliwa na kulelewa na kuwa brainwashed toka utotoni
Hii si kweli, baada ya kuzaliwa katika Uislamu, haikutosha hapo, nikaanza kumsoma na kumjua na nina endelea kumsoma, kadhalika natumia akili, mazingira kujua uwepo wake.

Mimi nataka uje na hoja, usilete vioja.
Ungezaliwa na wahindu uhundini ungekuwa budha na ungekomaa kumtetea mungu wa kihindi...... huu ni ushahidi tosha HAKUNA MUNGU isipokua tunarithishana zana ya Mungu
Hapa bado hujatoa ushahidi huenda hujui maana ya ushahidi, ushahidi ili uwe ushahidi lazima udiriki kile kinachotolewa ushahidi kwacho.

Na wale wanao zaliwa kwenye dini fulani kisha wakatoka katika dini hizo ni ushahidi wa kuonyesha Mungu yupo ? Hivi una akili kijana ?

Bado hujathibitisha ya kuwa Mungu hayupo.
 
Kutokuwepo kwa Mungu ni ushahidi wa kutokuwepo kwa Mungu
Kivipi ? Hizi falsafa tu ambazo hazina ithibati ya kiakili, uhalisia na mazingira. Nataka ulete ithibati.
Kama hakuna chakula kwenye meza ni ushahidi kwamba hakuna chakula kwenye meza.... PERIOD
Huu utoto mwingine. Huu mfano katika hii nukta hauingii, tunaongelea uumbaji unaleta mfano dhaifu wa meza na chakula. Wewe tuambie imekuwaje hii Dunia ikawepo na utuonyeshe kutokuwepo kwa Mungu.

Kutokuwepo kwa chakula kwenye meza kinahitaji maelezo. Kwamba je kilikuwepo hapo kabla kisha kikawa hakipo, na hakikuwepo kabisa utuambie umejuaje kama hakipo ?
Post yangu # 1 nimeeleza kwanini dhana ya Mungu ni uongo
Nilitarajia utapangua hoja ka hoja
Hujaonyesha hilo, zaidi ya kurudia hichi ulichokiandika kwa kutoa mfano wa meza na chakula.
 
Thibitisha kwamba miungu wao wameumba hii Dunia. Kingine utuambie kitu ili kiumbe kinatakiwa kiwe na sifa gani ?
.
Wewe umemthibitisha huyo Mungu wako?
 
Ameumba dunia kwaajili yetu na ataiangamiza dunia kwaajili yetu
Alijua ataiangamiza dunia kabla hata hajaiumba lakini aliiumba hivyo hivyo ili aje kuiangamiza,
Ameumba moto wa jehanamu kwakuwa ametuumba tukosee ili atuchome moto japo alikua na UWEZO wakutuumba tusiwe wakosefu ili atuumbie Pepo tu tukale bata
Kwahiyo hili ulichokiandika unasema hoja. Sasa njoo tujadili kwa masharti haya mawili tu :

1. Hakikisha kila swali ninalo kuuliza unajibu
2. Hakikisha unamjua huyu Mungu ambaye unamkana.

Naanzia hapa, Wapi kimeandikwa kama Dunia itaangamizwa kwa ajili yetu ? Mimi ni Muislamu, nataka ujadili jambo kwa mujibu wa Uislamu, maana Kuna sehemu ulijinadi kwamba unajua Uislamu ( Ila kiukweli kwa ulicho kiandika unaonyesha wazi huujui Uislamu).

Nukta ya kuiangamiza Dunia kwanza unatakiwa ulete ukweli wake.

Nakuja kwenye kuumba Moto, Mola wetu ametuumba kwa malengo, na akaweka utaratibu ya kuwa watakao faulu watalipwa pepo na watakao feli wataingizwa motoni, hili alilijua na anajua fulani wa motoni na fulani wa peponi.

Lakini alipo tuumba akatupa akili, matashi na hali wezekano ya kufanya mema na kufanya maovu. Katika hayo akaweka mlango wa kusamehe pale mtu utakapo kosea.

Hakuna sehemu ambapo kimeandikwa kwamba Mola wetu ametuumba ili tukosee, hili halipo. Haya maneno umeyapata wapi ? Bali ametuumba katika hali zote za kupatia na kukosea, na ukikosea ukiombwa msamaha kwake unasamehewa.

Sahihi kabisa na angetaka wote tumuamini angefanya hivyo, akatuumba na kutupa uhuru wa kufanya tunayotaka, ndio maana wewe Leo hii unamkana na humjui, lakini anakupa pumzi na kukulea.

Kwa akili ya mwanadamu, ungeumbwa katika hali hiyo unayo itaka pia ungelala, na Mola wetu ni Mjuzi wa kuumba.
 
Kivipi ? Hizi falsafa tu ambazo hazina ithibati ya kiakili, uhalisia na mazingira. Nataka ulete ithibati.

Huu utoto mwingine. Huu mfano katika hii nukta hauingii, tunaongelea uumbaji unaleta mfano dhaifu wa meza na chakula. Wewe tuambie imekuwaje hii Dunia ikawepo na utuonyeshe kutokuwepo kwa Mungu.

Kutokuwepo kwa chakula kwenye meza kinahitaji maelezo. Kwamba je kilikuwepo hapo kabla kisha kikawa hakipo, na hakikuwepo kabisa utuambie umejuaje kama hakipo ?

Hujaonyesha hilo, zaidi ya kurudia hichi ulichokiandika kwa kutoa mfano wa meza na chakula.

Utoto ni kuamini kwamba kama hujui kitu basi ni Mungu kakifanya

Mimi sijui dunia imetokeaje lakini hii sio sababu ya uwepo wa mungu

NARUDIA TENA KAMA HAKUNA CHAKULA KWENYE MEZA NDIO USHAHIDI WENYEWE KWAMBA CHAKULA HAKIPO..... period

Kama hautaki siwezi kukulazimisha ila huo ndio ukweli
 
Back
Top Bottom