Kwahiyo hili ulichokiandika unasema hoja. Sasa njoo tujadili kwa masharti haya mawili tu :
1. Hakikisha kila swali ninalo kuuliza unajibu
2. Hakikisha unamjua huyu Mungu ambaye unamkana.
Naanzia hapa, Wapi kimeandikwa kama Dunia itaangamizwa kwa ajili yetu ? Mimi ni Muislamu, nataka ujadili jambo kwa mujibu wa Uislamu, maana Kuna sehemu ulijinadi kwamba unajua Uislamu ( Ila kiukweli kwa ulicho kiandika unaonyesha wazi huujui Uislamu).
Nukta ya kuiangamiza Dunia kwanza unatakiwa ulete ukweli wake.
Nakuja kwenye kuumba Moto, Mola wetu ametuumba kwa malengo, na akaweka utaratibu ya kuwa watakao faulu watalipwa pepo na watakao feli wataingizwa motoni, hili alilijua na anajua fulani wa motoni na fulani wa peponi.
Lakini alipo tuumba akatupa akili, matashi na hali wezekano ya kufanya mema na kufanya maovu. Katika hayo akaweka mlango wa kusamehe pale mtu utakapo kosea.
Hakuna sehemu ambapo kimeandikwa kwamba Mola wetu ametuumba ili tukosee, hili halipo. Haya maneno umeyapata wapi ? Bali ametuumba katika hali zote za kupatia na kukosea, na ukikosea ukiombwa msamaha kwake unasamehewa.
Sahihi kabisa na angetaka wote tumuamini angefanya hivyo, akatuumba na kutupa uhuru wa kufanya tunayotaka, ndio maana wewe Leo hii unamkana na humjui, lakini anakupa pumzi na kukulea.
Kwa akili ya mwanadamu, ungeumbwa katika hali hiyo unayo itaka pia ungelala, na Mola wetu ni Mjuzi wa kuumba.