Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Walau nusu ya swali ulipouliza umelijibu kuwa pamoja na kupewa manual si manual yote wanadamu wanaielewa. Na kutoielewa kwenye haini ni uthibitisho wa kutokuwapo kwa Muumba wa kila kitu.

Pili ngoja nikupe kisa kimoja cha wakati wa mtume.

Mtume ktk siku zake za mwisho wa uhai wake alikaa na baadhi ya wanafunzi wake na kuwauliza maswali matatu.

Mmoja wa wanafunzi wake alifahamaika ABU DHAR AL GIFARIY:

Alipoulizwa wewe unapenda nini ktk hii dunia.
Alisema Ninapenda vitu vitatu hapa duniani.

a. Njaa,
b. Ugonjwa,
c. Na kifo

Alipoulizwa kwann, Abu Dharr akajibu:👇🏼 a. Ninapenda njaa ili kulainisha moyo wangu.
b. Ninapenda magonjwa ili kupunguza dhambi yangu.
c. Na mimi napenda mauti kwa kuwa nimejiandaa kukutana na Mola wangu Mlezi.

Angalia hii falsafa na ndio spirit tunayoishi sisi waislam.

Kwamba pamoja na kuwa tetemeko limeua watu wema na wabaya lkn wale wema wana spirit ya kuamini amerudi kwa mola wake hali ya kuwa yuko na amani ktk nafsi na moyo wake.

Wakati ninyi kwa upande wenu mnaona ni mateso.

Same case kwa magonjwa haya dume kama canser kwa watoto
🤣🤣🤣So ukiumwa ndo unafurahi dhambi zinapungua...duu mpo serious, yaani dini ni watu wengi kuwa machizi
 
Mazingira yako wazi sana. Uwepo wa usiku na mchana unathibitisha ya kuwa yupo aliye uweka tena mwenye ujuzi na mpangiliaji wa mambo.

Jua kuzama Magharibi na kuchomoza Mashariki, uwepo wa Mwezi kadhalika, mabadiliko ya majira hivi haviwezi kuwepo pasi na kupangiliwa. Hii tunaita "Self evident Truth".

Akili iliyo salama, inakataa ya kuwa Dunia Haina mwenyewe, akili iliyo salama ina hoji kwanini tupo duniani ? Je tupo ili tuoshi tu kisha iwe basi ? Akili iliyo salama inakusukuma wewe kujua lengo la kuishi kwako, hapo lazima utakiri ya kuwa yupo aliye tuumba tena kwa malengo.

Akili iliyo salama, inatafuta lengo la maisha, inakataa ya kuwa, iweje muovu adhulumu halafu iwe basi tu, au fisadi afisidi halafu iwe basi. Lazima kutakuwa na ukomo na siku ya malipo.

Mambo yako mengi sana yanayo onyesha uwepo wa Mungu.
🤣🤣🤣 Nyie si ndo mlisema day, night, jua na mwezi vinazunguka dunia, jua linazama kwenye tope, jua linaomba ruhsa kwa Allah kuchomoza asubuhi....na siku ya mwisho litaambiwa lirudi lilipotoka ndo litachomoza magharibi...🤣🤣🤣🤣all this is primitive knowledge...yaani huyo mtume wenu alikuwa hajui lolote kuhusu dunia na Sayansi halisi alikuwa anatoa vitu akilini anasema Allah's knows best ..kingine hayo maswali unayouliza don't prove the existence of a god and also don't prove the existence of Allah...it proves kwamba Kuna vitu hatuvijui...hizi zingine ni imagination tu kujikosha unataka watu unaowachukia waumie na wewe ule bata...ni mentality ya kimaskini 🤣🤣🤣all in all ni utoto na ujinga...no proof
 
Sasa kwanini unasema hakipo na umekiri ya kuwa huwezi kuthibitisha ? Unatumia nini kufikiri ?

Mimi nimeshakuthibitishia, nataka uje ukosoe ithibati zangu.

Kwanini unalazimisha kutokuwepo kwake na unashindwa kuthibitisha hilo ? Huu ni upumbavu wa hali ya juu.

Swali, yanayosemwa kwenye vitabu ni ya uongo ? Mfano nimeweka aya hapa lakini hakuna aliye jadili kilicho andikwa kwenye aya mnaruka ruka. Aya inauliza kwamba je hii Dunia imetokana pasi na chochote au imejiumba ? Ukootafakari hii aya kwa umakini no sahihi, Sasa mje mseme ya aidha imejiumba au imetokana pasi na chochote, kisha mthibitishe hilo.
Huyo Allah nae katokeaje bila kuumbwa?
 
Kwanza Allah ndio ameumba ndimi za watu, katika surat al Insaan amegusia hilo, ya kuwa ameumba mataifa na makabila mbali mbali lengo tupate kujuana.

Kwahiyo Allah ndie ameumba lugha na mataifa, na haongei Kiarabu, bali Allah akituma mjumbe sehemu anampa ujumbe kwa lugha yakez ndio maana Ibrahim aliongea kwa lugha yao, Musa, Yesu na kadhalika Mtume aliongea au kupewa ujumbe kwa lugha ya Kiarabu sababu alianza kuzungumza na watu wake kwa lugha hiyo, vipi Mtume awe Muarabu halafu apewe ujumbe kwa Kisukuma na watu wake wanaongea Kiarabu ?

Allah anaeleweka kwa lugha zote, ndio maana tunamuomba na kumsoma. Lakini lugha sio kikwazo kama ukiamua kujifunza, na ukianalgalia lugha ya Kiarabu ni tofauti na lugha nyinginezo bali husemwa lugha hii ni ya watu wote na ushahidi uko wazi, ukisoma Historia ya fani za Kiarabu utakuta wasomi wa kubwa wa lugha hii Ulimwenguni kote si Waarabu kiasalia, lakini tafuta lugha nyingine hilo hulikuti. Tukiongelea katika mlango huo hakuna lugha kuishinda Kiarabu.

Kujua Kiarabu ni lazima kama ukitaka kujua Dini hii, sababu imekuja kwa lugha ya Kiarabu. Lakini hakuna aliye zaliwa anajua, hata wewe Leo hii umezaliwa hujui kusoma Wala kuandika lakini umesomeshwa na ukajua. Sasa kwanini hili hulisemi ? Leo hii ulienda Saudia utakuta Waafrika wanawasomesha Waarabu Kiarabu,maana yake nini ? Hii ni elimu Haina wenyewe ukitaka kujua unajua ukizembea ni wewe na uzembe wako.

Hajashindwa kufanya hivyo, bali angetaka sote tumuamini tunge kumaini kama ilivyo nukuliwa hivyo katika Qur'aan, ila amefanya haya na kuweka hali wezekano za kujua ambayo wewe unayadai ukitaka. Mola wetu hapendi watu wazembe.
Swali la kwanza kwa Nini katumia means ya communication ambayo ni ngumu...lyk kwa Nini kila mtu asingezaliwa anamjua Allah lazma afundishwe na mama ake muislam na Kama Hana wazazi waislamu coz of geography labda anakuwa dini nyingine. Why religion is just an accident of history and geography?
 
Kwanin

Kwanini unaandika uongo ? Mara ngapi nimewakosoa kuhusu logic na mkashindwa kutetea utoto wenu ?

Nakupa kazi hapa, kati ya maneno na logic kipi kilianza ?

Kingine njoo uthibitishe ukweli wa logic katika kuthibitisha kutokuwepo kwa Mungu, zaidi ya kucheza na maneno na kuikimbia hoja.

Msingi wa logic ni akili, akili ambayo ni dhaifu na ina ukomo vipi utumie akili pekee kukufokisha katika ukweli ?

Shida yenu hizi elimu mlizichukua kiushabiki ndio maana zinawafanya muwe wajinga na msio weza kufikiria nje ya mawazo ya waasisi wa logic zenu.
🤣Unajua ungekuwa mkristo ungekuwa unamtetea Yesu hapa afu unasema sisi ndo mashabiki
 
Una Assume vipi kwa jambo ambalo lipo tayari ?

Badilisha namna ya ujengaji hoja.

Ukisoma vitabu kila kitu ameandika na amefafanua, shida yenu hamsomi hivi vitabu, hasa Qur'aan. Jaribuni kutenga muda msome haya mambo.

Shida nyingine ni kuwa hamsomi.
🤣Quran inayosema nyota zipo anga ya karibu ili ziwapige mashetani wasikaribie kitu Cha Allah
 
Safi kabisa, uje tena kusema ya kuwa mantiki ni jambo la msingi. Nitakuuliza swali kwanini umefikia hitimisho la juu ya kuwa watu kuingia motoni ni kwamba Allah Hana upendo wowote ?

Nilipokosoa Mantiki kama fani pweke, sababu najua logic, logic ina udhaifu wa kuchukua mambo juu juu. Huwezi kujiuliza kwanini watu wameingia motoni ? Ni baada ya nini na nini ?

Mpaka watu wanaingia motoni ni mchakato wa matendo, nia, na kufata mafundisho. Ukiona watu wanaingia motoni ujue huo ni mchakato, ni kwamba walifikishiwa ujumbe wakaukataa, hawakufanya toba muda ambao nafasi ya kufanya hivyo ilikuwepo, walikuwa na uwezo wa kufanya mema hawakufanya bali walikuwa na uwezo wa kutofanya uovu wakazembea.

Sasa kwa kutumia logic yenu kwa jambo kamilifu kama hilo onyesha wapi Lina makosa na halina mantiki kwa maana ya kuleta maana.

Allah akisema ya kuwa atatupa mitihani na hili liko wazi, akupime utasubiri au utakufuru, muda ambao tayari ameshakupa na njia ya kufaulu mtihani huo. Hapa anaonyesha upendo wa hali ya juu alio nao kwa waja wake.

Naam, anajua hayo sababu yeye ni Mjuzi wa kila kitu. Lakini kujua kwake yeye hakukuzuii wewe kufanya unalo taka, sababu ametupa uhuru huo.

Usiseme yanakosa mantiki kwa kuhitimisha juu juu na kutoangalia mchakato mzima.

Sasa nataka uje hapa uonyeshe kutokuwa na maana kwa maneno haya.
🤣🤣🤣🤣Acha uwongo ...Quran inasema all non Muslims wanaenda hell forever ..afu waislamu ndo wanachaguliwa according to behavior...so automatically Mungu ameumba watu billions ambao hawajazaliwa waislamu ili awachome
 
Kuna watu hawaamini kabisa kwamba inawezekana akawepo mtu haamini katika uwepo wa Mungu, yani katika akili zao, hicho kitu hakiwezekani.

Kwa sababu ya udogo wa mawazo yao.

Kwahiyo unaona watu wote tuna amini Mungu tuna mawazo madogo?

Unapata faida gani kutumia nguvu kumpiga Mungu
Bora utumie muda huo kuzidi kumtafuta na hakika utamjua
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Acha uwongo ...Quran inasema all non Muslims wanaenda hell forever ..afu waislamu ndo wanachaguliwa according to behavior...so automatically Mungu ameumba watu billions ambao hawajazaliwa waislamu ili awachome

Unapata faida gani kukomaa kumpinga Mungu?

Nakushauri tumia muda wako kuzidi kumtafuta na utamjua bila shaka
 
Kwahiyo unaona watu wote tuna amini Mungu tuna mawazo madogo?

Unapata faida gani kutumia nguvu kumpiga Mungu
Bora utumie muda huo kuzidi kumtafuta na hakika utamjua
Wapi nimesema watu wote mnao amini Mungu mna mawazo madogo?

Unaweza kunionesha hiyo sehemu?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
😂😂Kwa nn wwe hauna majibu na hutaki kuelewa?

Nimekuuliza haujawahi kujibu hata mara moja .!
Mkuu, eleza chanzo cha binadamu na utoe facts kama ulivyosema.

Hayo mengine unayoyafanya hapa ni uhuni tu.

Sijui kila kitu, ndo maana nakwambia unipe hizo facts za chanzo cha binadamu.
 
Safi kabisa, uje tena kusema ya kuwa mantiki ni jambo la msingi. Nitakuuliza swali kwanini umefikia hitimisho la juu ya kuwa watu kuingia motoni ni kwamba Allah Hana upendo wowote ?
Je unaweza kuwa na upendo wote na ukamchoma mwanao kwenye moto hata kama kaua!?

Nilipokosoa Mantiki kama fani pweke, sababu najua logic, logic ina udhaifu wa kuchukua mambo juu juu. Huwezi kujiuliza kwanini watu wameingia motoni ? Ni baada ya nini na nini ?

Mpaka watu wanaingia motoni ni mchakato wa matendo, nia, na kufata mafundisho. Ukiona watu wanaingia motoni ujue huo ni mchakato, ni kwamba walifikishiwa ujumbe wakaukataa, hawakufanya toba muda ambao nafasi ya kufanya hivyo ilikuwepo, walikuwa na uwezo wa kufanya mema hawakufanya bali walikuwa na uwezo wa kutofanya uovu wakazembea.

Sasa kwa kutumia logic yenu kwa jambo kamilifu kama hilo onyesha wapi Lina makosa na halina mantiki kwa maana ya kuleta maana.
Haijalishi kwamba kakosea nini.

Kwasifa za Mungu huyo zinazotajwa inaonesha kabisa jinsi alivyo na upendo wa hali ya juu.

Kitendo cha kiumbe wake kukosea haimfanyi Mungu mwenye upendo wote kumuadhibu kwa kumchoma moto.

Je Mungu muweza wa yote angeshindwa kuumba ulimwengu ambao hauwezekani kutendeka uovu wa aina yeyote ile ili kusiwe na watakaoenda motoni?

Kwanini Mungu mwenye upendo wote kaumba ulimwengu huu wenye matetemeko yanayoua maelfu kwa maelfu?
Allah akisema ya kuwa atatupa mitihani na hili liko wazi, akupime utasubiri au utakufuru, muda ambao tayari ameshakupa na njia ya kufaulu mtihani huo. Hapa anaonyesha upendo wa hali ya juu alio nao kwa waja wake.

Naam, anajua hayo sababu yeye ni Mjuzi wa kila kitu. Lakini kujua kwake yeye hakukuzuii wewe kufanya unalo taka, sababu ametupa uhuru huo.
Kwanini Mungu atake kututest wakati anajua yote hata matokeo ya mtihani huo?
Usiseme yanakosa mantiki kwa kuhitimisha juu juu na kutoangalia mchakato mzima.

Sasa nataka uje hapa uonyeshe kutokuwa na maana kwa maneno haya.
Psychology ya theist sku zote ilijengwa ili kusifu,

yani ni kwamba unahisi kuwa huyo Mungu anafuatilia hata unavyopost hapa JF

Kwaakili yako kwakuwa unadhani hivyo, unajaribu kupambana kwa hali na mali ili upate nafasi ya kuhesabiwa haki mbinguni.

Hilo ni tatzo la psychology tu, ndiyo maana unakataa contradiction za wazi kabisa.
 
Kwahiyo unaona watu wote tuna amini Mungu tuna mawazo madogo?

Unapata faida gani kutumia nguvu kumpiga Mungu
Bora utumie muda huo kuzidi kumtafuta na hakika utamjua
Mna mawazo madogo sana kwa vile mna amini kisicho kuwepo.

Mungu huyo kama yupo anacho jifichia ni nini?

Kwani ange jitokeza tumjue, inge badilisha nini yeye kuwa Mungu?

Kama yeye ni muweza wa yote, Anaogopa nini kuonekana hadharani?
 
Mungu yupo hata utoe mifano ambayo haipo ila ukweli Mungu yupo mratibu wa mambo yote...
Basi tukubaliane hivi,

Kama Mungu huyo Yupo na ndiye mratibu wa mambo yote,

Basi Mungu huyo pia ni mratibu wa Uovu wote, Ubaya wote, Mateso yote, Ukatili wote, Unyama wote, na makosa yote.

Mungu huyo hana huruma na ni mkatili sana

Maana yeye ndiye mratibu wa mambo yote.
 
Back
Top Bottom