Uongo mkubwa zaidi kutokea dunia - The biggest scam in the world

Mkuu naona unajaribu kukwepa msingi wa HOJA kwa kucheza na maneno

Unapo ambiwa tuonyeshe Mungu alipo maana yake thibitisha alipo na uwepo wake

Wewe tuambie huyo Mungu wako anathibitika vipi?
Binadamu tunatambua vitu kwa milango ya fahamu
We mthibitishe anavyoweza kuthibitika
Umesema ulikulia Sunday School na hata una vinasaba vya Uislamu. Kitu kama hicho.

Je, ulifundishwaje kuhusu Mungu? Unajuaje yupo?

Tuanzie hapo kwanza, maana huenda hata misingi yenyewe huijui au umeisahau.
 
Sijawahi KUJUA kama Mungu yupo...... Niliaminishwa yupo

Nimebatizwa hata sijitambui, naonaga picha na cheti cha ubatizo tu
Nimekua huku nikiwa brainwashed kuna Mungu kuanzia na wazazi wangu, ndugu na jamii
Sunday school tulifundishwa kumtii Mungu ili tusije kuchomwa moto wa milele na lishetani huko jehanamu

Mshua alipo hama Tanga Bimkubwa na wajomba wakanipeleka madrasa..... nikabadikishwa na Jina nikawa Ali
Nikapigwa sana mijeredi kujifunza kiarabu, nikafundishwa kuhusu Allah na Mudi kwamba ni mtii Mola la sivyo Jehanam ya milele inanihusu

Msingi mzima wa mafundisho ya Ukristo/Uislam imejaa vitisho na ahadi hewa
Fanya hiki Mungu atakupa vitu vizuri na bata la milele baada ya kufa
Usifanye hivi utapata laana duniani na utachomwa moto milele baada ya kufa

Kumbuka haya yote yanajiri wakati bado ni mdogo sina nafasi ya kuamua/kuchagua...... nachaguliwa cha kuamua na kufanya

Ndio maana tunauliza kwanini mtu kuwa dini fulani ni matokeo ya jiografia historia na malezi?

Mtoto wa kiyahudi aliyezaliwa na wayahudi hana chaguo zaidi ya kuwa Jew
Mtoto wa kihindu au wa kikorea hana nmna nyingine ya kuamini zaidi ya Mungu aliyepandikizwa na kukuzwa naye kuchwani mwake toka utotoni

Sasa nimekua mtu mzima na dhana nzima ya Mungu imekosa uhalisia kabisa
 
Sijawahi KUJUA kama Mungu yupo...... Niliaminishwa yupo
Hujajibu swali. Sunday School na Madrasa umefundishwa vipi kuhusu uwepo wa Mungu?

Nimekua huku nikiwa brainwashed kuna Mungu kuanzia na wazazi wangu, ndugu na jamii
Je, sasa umethibitisha kwamba Mungu hayupo?

Sunday school tulifundishwa kumtii Mungu ili tusije kuchomwa moto wa milele na lishetani huko jehanamu
Umewahi kujifunza saikolojia ya punishment & reward kama motivesheni za good behavior?

Msingi mzima wa mafundisho ya Ukristo/Uislam imejaa vitisho na ahadi hewa
Fanya hiki Mungu atakupa vitu vizuri na bata la milele baada ya kufa
Usifanye hivi utapata laana duniani na utachomwa moto milele baada ya kufa
Kwa mtazamo wako, matendo mema hayana manufaa?

Matendo mabaya hayana madhara, secularly speaking?
Kumbuka haya yote yanajiri wakati bado ni mdogo sina nafasi ya kuamua/kuchagua...... nachaguliwa cha kuamua na kufanya
Unadhani ni umri gani unaofaa mtoto kuanza kufundishwa kufuata mwenendo mwema?

Ndio maana tunauliza kwanini mtu kuwa dini fulani ni matokeo ya jiografia historia na malezi?
Kwa sababu jiografia haimfungi yeyote asimjue Mungu wa kweli.

Ndiyo maana kuna watu wamchao Mungu Bogota, Omani, Beijing, Mosko, New Delhi, Pakistani, Pyongyang, Los Angeles, na hata Pemba.

Mtoto wa Kiyahudi aliyezaliwa na Wayahudi hana chaguo zaidi ya kuwa Jew
Mtoto wa Kihindu au wa Kikorea hana nmna nyingine ya kuamini zaidi ya Mungu aliyepandikizwa na kukuzwa naye kuchwani mwake toka utotoni
Unajipinga kwa kauli zako mwenyewe; umesema ulizaliwa Mkristu, kisha ukawa Mwislamu, na sasa ni mpagani.

Hivi hapo ni kweli huna uamuzi wowote kuhusu unachopaswa kuamini?
Sasa nimekua mtu mzima na dhana nzima ya Mungu imekosa uhalisia kabisa
Je, siku dhana nzima ya upagani nayo ikikukosa uhalisia, utamgeukia Mungu tena?

Au sasa umeshajiridhisha pasi na shaka kwamba hayupo.
 
Hujajibu swali. Sunday School na Madrasa umefundishwa vipi kuhusu uwepo wa Mungu?

Je, sasa umethibitisha kwamba Mungu hayupo?
.
Nimejibu nilicho fundishwa

Nimejiridhisha hayupo... soma post #1

Kwa mtazamo wako, matendo mema hayana manufaa?

Matendo mabaya hayana madhara, secularly speaking?

Unadhani ni umri gani unaofaa mtoto kuanza kufundishwa kufuata mwenendo mwema?
.
Hapa tunazungumzia “matendo mema/mabaya” kwa mujibu wa “Mungu”
Mengine ni upuuzi na ukatili mtupu

Kwa sababu jiografia haimfungi yeyote asimjue Mungu wa kweli.

Ndiyo maana kuna watu wamchao Mungu Bogota, Omani, Beijing, Mosko, New Delhi, Pakistani, Pyongyang, Los Angeles, na hata Pemba.

Unajipinga kwa kauli zako mwenyewe; umesema ulizaliwa Mkristu, kisha ukawa Mwislamu, na sasa ni mpagani.
.

Yes kwa asilimia kubwa sana Jografia historia na makuzi inamfunga mtu kumjua huyo Mungu wako wa kweli na inaamua mungu gani utamuamini

Tu assume wewe ni Mkristo.... trust me kuna watu wanazaliwa hadi wanakufa huko korea au china na hawajui kama Yesu ni Mungu, wanachojua wao Mungu ni Budha wao tu
Hawajui kwasababu hawa access hiyo ya kumjua sababu ya jiografia historia na makuzi
Kuna watu hapa Tz hawajui hata kama kuna Mungu anaitwa ZEUS...... why?
BTW “mungu wa kweli” ndio yupi? Maana kuna Miungu zaidi ya milioni moja duniani

Sijipingi..... soma vizuri utanielewa
Haijatokea bahati mbaya kwamba kwanini Zanzibar 90% ni waislam wa Suni
Sio Mungu aliyeamua 90% ya wa Iran kuwa waislam tena wa Shia na China 90% ni Budha
Unadhani kwanini asilimia kubwa ya waisrael ni dini ya kiyahudi?....... ni jiografia historia na makuzi

Je, siku dhana nzima ya upagani nayo ikikukosa uhalisia, utamgeukia Mungu tena?

Au sasa umeshajiridhisha pasi na shaka kwamba hayupo.

Mkuu siwezi kupinga kitu ambacho KIPO

Kama Mungu atajithibitisha/atathibitika yupo utapingaje sasa kuwa hayupo?

Mungu akiwepo na upagani haupo
 
Nimejibu nilicho fundishwa
Nimejiridhisha hayupo... soma post #1
Kwamba ukimwita mtu fulani unayemdhania yumo ndani, asipoitikia wito wako kadiri upendavyo, maana yake hayupo?

Kwamba chochote ambacho huwezi wewe ^kukiona,^ maana yake hakipo?

Mantiki yako inafikirisha sana.

Hapa tunazungumzia “matendo mema/mabaya” kwa mujibu wa “Mungu”
Mengine ni upuuzi na ukatili mtupu
Nisaidie kujua jinsi mafundisho kuhusu upendo mkuu wa Mungu yaIivyo upuuzi na ukatili kwako.

Yes kwa asilimia kubwa sana Jografia historia na makuzi inamfunga mtu kumjua huyo Mungu wako wa kweli na inaamua mungu gani utamuamini
Sasa siyo tena kwamba jiografia ndiyo inaamua hatima ya kila mtu, bali ^asilimia kubwa sana^?

Nisaidie kuelewa jinsi gani hiyo asilimia ndogo sana iliyobaki inaweza kuepuka vifungo vya kijiografia, ikaamini chochote kinyume na imani ya walio wengi?

Na, hivi hilo halithibitishi pasi na shaka kwamba jiografia kamwe katu siyo kisingizio cha kutomjua Mungu (wa kweli)?
Tu assume wewe ni Mkristo.... trust me kuna watu wanazaliwa hadi wanakufa huko korea au china na hawajui kama Yesu ni Mungu, wanachojua wao Mungu ni Budha wao tu
Hawajui kwasababu hawa access hiyo ya kumjua sababu ya jiografia historia na makuzi
Kuna watu hapa Tz hawajui hata kama kuna Mungu anaitwa ZEUS...... why?
Niambie hii dhana inahusianaje na uelewa wako wa kutowepo kwa Mungu?

BTW “Mungu wa kweli” ndio yupi? Maana kuna miungu zaidi ya milioni moja duniani
Unaamini kuna pesa bandia na halali? Vilevile kuna Mungu wa kweli na sanamu (miungu).

Sunday School & Madrasa ulifundishwa kuhusu Mungu gani miongoni mwa hao ^miungu zaidi ya milioni moja^?

Sijipingi..... soma vizuri utanielewa
Haijatokea bahati mbaya kwamba kwanini Zanzibar 90% ni waislam wa Suni
Sio Mungu aliyeamua 90% ya wa Iran kuwa waislam tena wa Shia na China 90% ni Budha
Nasema unajipinga kwa sababu kwa nini iwe 90% na wala siyo 100%?

Mleta-mada alisema kitu fulani kama, ^Mungu amemuumba mwanadamu ili aje amchome moto milele, kwa sababu ya makosa yaliyo nje ya mwanadamu.^

Naamini haya pia ni mawazo yako wewe. Sasa, ikiwa ndivyo, hii asilimia ndogo ya watu wanaoonekana kwenda kinyume na walio wengi, na wanamtii Mungu, wao inawezekanaje?
Unadhani kwanini asilimia kubwa ya Waisrael ni dini ya Kiyahudi?....... ni jiografia historia na makuzi
Wazo lako la msingi ni kwamba jiografia inamfunga mtu, amjue ama asimjue Mungu.

Sasa umeongeza historia na makuzi. Nami nasema kwamba ni zaidi ya hapo.

Suala la kumjua au kutomjua Mungu hushamirishwa na sababu mbalimbali.

Lakini moja kubwa kuliko zote ni uamuzi wa mtu mwenyewe, licha ya mazingira husika.

Ndiyo maana kuna wapagani pamoja na watu wamchao Mungu kila mahali.

Maana yake ni nini? Jiografia siyo udhuru wa kutomjua Mungu.

Mkuu siwezi kupinga kitu ambacho KIPO
Kama Mungu atajithibitisha/atathibitika yupo utapingaje sasa kuwa hayupo?
Utapingaje? Kwa kujiwekea vigezo vyako mwenyewe kuhusu namna Mungu anavyopaswa kuwa ama kutenda kazi.

Mfano👇
Mungu akiwepo na upagani haupo
 
Kwamba ukimwita mtu fulani unayemdhania yumo ndani, asipoitikia wito wako kadiri upendavyo, maana yake hayupo?

Kwamba chochote ambacho huwezi wewe ^kukiona,^ maana yake hakipo?

Mantiki yako inafikirisha sana.

Nisaidie kujua jinsi mafundisho kuhusu upendo mkuu wa Mungu yaIivyo upuuzi na ukatili kwako.

Sasa siyo tena kwamba jiografia ndiyo inaamua hatima ya kila mtu, bali ^asilimia kubwa sana^?

Nisaidie kuelewa jinsi gani hiyo asilimia ndogo sana iliyobaki inaweza kuepuka vifungo vya kijiografia, ikaamini chochote kinyume na imani ya walio wengi?

Na, hivi hilo halithibitishi pasi na shaka kwamba jiografia kamwe katu siyo kisingizio cha kutomjua Mungu (wa kweli)?

Niambie hii dhana inahusianaje na uelewa wako wa kutowepo kwa Mungu?

Unaamini kuna pesa bandia na halali? Vilevile kuna Mungu wa kweli na sanamu (miungu).

Sunday School & Madrasa ulifundishwa kuhusu Mungu gani miongoni mwa hao ^miungu zaidi ya milioni moja^?

Nasema unajipinga kwa sababu kwa nini iwe 90% na wala siyo 100%?

Mleta-mada alisema kitu fulani kama, ^Mungu amemuumba mwanadamu ili aje amchome moto milele, kwa sababu ya makosa yaliyo nje ya mwanadamu.^

Naamini haya pia ni mawazo yako wewe. Sasa, ikiwa ndivyo, hii asilimia ndogo ya watu wanaoonekana kwenda kinyume na walio wengi, na wanamtii Mungu, wao inawezekanaje?

Wazo lako la msingi ni kwamba jiografia inamfunga mtu, amjue ama asimjue Mungu.

Sasa umeongeza historia na makuzi. Nami nasema kwamba ni zaidi ya hapo.

Suala la kumjua au kutomjua Mungu hushamirishwa na sababu mbalimbali.

Lakini moja kubwa kuliko zote ni uamuzi wa mtu mwenyewe, licha ya mazingira husika.

Ndiyo maana kuna wapagani pamoja na watu wamchao Mungu kila mahali.

Maana yake ni nini? Jiografia siyo udhuru wa kutomjua Mungu.

Utapingaje? Kwa kujiwekea vigezo vyako mwenyewe kuhusu namna Mungu anavyopaswa kuwa ama kutenda kazi.

Mfano[emoji116]

Mkuu natamani kujibu kwa mtindo huu wa quote na jibu.... lakini inanichosha sana ku copy paste cut reply halafu unarudia tena na tena

Twende na hoja moja labda unaweza KUNITHIBITISHIA uwepo wa Mungu mkuu

Tuanze na kipi kinapelekea mtu kumuamini Mungu fulani

Wewe unasema kuna Mungu wa kweli mmoja tu...... Natamani nimjue ni yupi ili tujikite naye
Maana kuna Mungu zaidi ya milioni moja duniani
 
Huyo jamaa alihoji kama kweli Mungu yupo tuonyeshe huyo mungu Yuko wapi?
Yeye alikua anataka amuone Mungu kwa macho ndio maana nikamtolea huo mfano.
Pia nimemuuliza kama anayo akili lakini hakunijibu, angenijibu ningemuomba anioneshe hio akili yake ili niamini kama kweli anayo hio akili.
Daa, Kweli hapa Shule inahitajika
 
Daa, Kweli hapa Shule inahitajika

Ukitaka kujua waamini Mungu wana ufahamu hafifu basi muulize kuhusu uthibitisho wa uwepo wa Mungu [emoji23][emoji23]

Siku zote hawana majibu zaidi ya kuhoji swali lako au wao kuuliza maswali
 
Twende na hoja moja labda unaweza KUNITHIBITISHIA uwepo wa Mungu mkuu
Ndiyo. Kuna vithibitisho chungu nzima.

Mojawapo ni kwamba huwezi kuthibitisha kwamba Mungu hayupo. Au unaweza?

Tuanze na kipi kinapelekea mtu kumuamini Mungu fulani
Usahibi asilia (natural affinity). When God created human, He kinda placed a void in the soul which can never be filled by anything except Himself.

That emptiness is a spiritual thirsty and soul hunger that God alone can satisfy.

Afterall, we're made in the image and likeness of God. How can we not naturally want to believe Him?

The only thing that we're doing it wrong is when, by exercising our own freedom of choice or freewill, we try so hard to override and resist His rightful place in us.

Wewe unasema kuna Mungu wa kweli mmoja tu...... Natamani nimjue ni yupi ili tujikite naye
Maana kuna Mungu zaidi ya milioni moja duniani
Unataka umjue kwa namna gani? Because there are countless ways of knowing God. One way, is to ask yourself where you came from.

Ukitaka kujua waamini Mungu wana ufahamu hafifu basi muulize kuhusu uthibitisho wa uwepo wa Mungu

Siku zote hawana majibu zaidi ya kuhoji swali lako au wao kuuliza maswali
Kwani hujui kwamba swali kwa swali huzaa jibu?

Tatizo lako maswali hayo huyasomi. Unarukaruka tu kama mvua za vuli.

Pili, ukiuliza swali halafu ukatarajia jibu fulani ulilo nalo, maana yake ni kwamba wewe mwenyewe tayari umeshajichorea mipaka yako.

Nimekuuliza maswali, lakini umeshindwa kujibu; umebaki kuporojeka tu.
 
Nimebatizwa hata sijitambui, naonaga picha na cheti cha ubatizo tu. Sunday school tulifundishwa kumtii Mungu ili tusije kuchomwa moto wa milele na lishetani huko jehanamu

... wakanipeleka madrasa..... nikabadikishwa na Jina nikawa Ali
Nikapigwa sana mijeredi kujifunza kiarabu, nikafundishwa kuhusu Allah na Mudi kwamba ni mtii Mola la sivyo Jehanam ya milele inanihusu
Wacheki PUBLISHER huwezi kukosa ajira [emoji2960]
 
Wewe ndiyo huna akili unaamini Mungu wa kutoka Mashariki ya kati anayeongea kiarabu na Hebrew .
Mtumwa wa Wakoloni
Ulitaka atokee wapi? Hebu angalia hicho kigazi (gadget) chako, niambie kimetengenezewa kiwanda gani hapa kwenu Bongo?

You need to appreciate the undisputed fact that others have more advanced knowledge than you.

Wake up! God's true religion is no respector of regions. It's universal and transcends all cultural entanglements.
 
Back
Top Bottom