Wanabodi,
Kati ya vyombo vyote vya habari duniani, chombo kikuu kabisa cha kuaminika, kwa sisi Anglophone Africa ni our colonial master, The British na shirika lao la habari la kibeberu la BBC London, na kwa Francophone Africa ni France na RFI na F24 TV. Sasa inapotokea chombo kama BBC London, Wakaripoti, kitu cha uongo, kwa upotoshaji kwa kukosa weledi, nani atakuwa mkweli?
Angalizo: Kutokana na umaarufu na heshima ya BBC, akitokea mwandishi tuu wa kawaida kama mimi kuikosoa BBC, wengi bado wataamini
BBC is always right, na mimi ndie niko
wrong, hawaamini kama BBC BBC inaweza kuwa biased kama kwenye story hii, kusema uongo, inaweza kupotosha, na inaweza kuripoti jambo fulani bila kufuata weledi wa kihabari.
Naomba kuwathibitishia kuwa japo ni kweli BBC ni weledi, lakini katika vita ya Kiuchumi na kutishiwa kwa Maslahi ya mabeberu, hata BBC huwa inaweka weledi pembeni, kutangaza uongo, upotoshaji kwa Maslahi ya mabeberu.
Huko nyuma mifano ipo ya BBC kusema uongo na kupotosha, imeshitakiwa mahakamani, imehukumiwa na kukutwa na hatia, imeomba radhi, na kulipishwa faini, hivyo katika upotoshaji wa jambo hili, BBC iombe radhi, vinginevyo sisi Tanzania tusikae kimya, tukanushe na kuinyoosha habari yenyewe.
Upotoshaji wenyewe ni huu
Uchaguzi 2020 - BBC Swahili wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa.
Nimemsikiliza Zuhura Yunus, kwanza makala yenyewe ni biased kwa kujadili baadhi tuu ilani za baadhi ya vyama, na kuviacha vyama vingine. Huwezi kufanya analysis ya ilani za vyama, ukaiepuka ilani ya CCM!.
Pili BBC ni waongo, hakuna mkataba wala makubaliano ya 2017, wala 2019, bali mkataba ni mmoja tu, ule uliosainiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam January 2020!. Yale ya 2017 yalikuwa ni mapendekezo tu na ya 2019 ni mapendekezo tuu, mkataba ni mmoja tuu wa January 2020!. How come BBC Swahili missed these facts?. BBC Swahili Iache Uongo!.
NB, uongo kama huu wa BBC pia uliwahi kuletwa mwanasiasa fulani, baada ya kuona makubaliano yamekuwa initialed, akaandika mkataba umesainiwa!, BBC nao wakaingia kichwa kichwa na kuamini mkataba umesainiwa!, wanaweza kuandika makala ndefu namna hiyo bila ku
double-check na ku
cross-check kuibalance makala yao na wahusika wa wizara husika? Huku ni kukosa weledi! Sasa kama BBC London inaweza kukosa weledi wa kiwango hiki, nani atakuwa mweledi?
Sio kwamba najidai, lakini kwenye mgogoro wa makinikia ya Acacia, hakuna mwana JF aliyeandika na kufuatilia kama mimi, na kwa jinsi nilivyomsikia Waziri Prof. Kabudi na Rais Magufuli, kuna maeneo ninaamini, ninayafahamu vizuri zaidi kuliko hata wahusika wenyewe wa kwetu, kwasababu issues nyingine ni issue ndogo tuu za lugha za watu, na watu wanaingizwa chaka, kama ilivyoelezwa kuwa tutagawana economic benefits pasu kwa pasu, tukaelezwa tutagawana faida, profits 50/50 kitu ambacho sii kweli.
Hata Mtaalamu wa Madini naye ni muongo na mpotoshaji.
Kwenye hili la Mtaalamu, naomba kuheshimu mawazo ya yule Mtaalamu kwa kiasi kikubwa yuko right ila na yeye pia ni muongo baadhi ya maeneo na mpotoshaji.
Uongo mkubwa wa Mtaalamu ni ameshindwa kutofautisha Acacia, Barrick na Twiga. Baada ya Barrick kuinunua Acacia, ofisi zote za Acacia zilizokuwa London na South Africa, zilifungwa.
Accounts zote za Acacia zilizokuwa London na South Africa zilifungwa, Ofisi za Twiga ziko Tanzania tuu, na accounts za Twiga zina bank na City bank ya Tanzania.
Kwenye huu ubia, Barrick anamiliki 84%, na Tanzania anamiliki 16%, Barrick kama Barrick bado yuko huru kuwa na ofisi zake popote duniani na ku bank fedha zake na benki zozote!.
Wito kwa serikali yetu
Naiomba serikali yetu ikanushe uongo huu wa BBC London kuihusu Tanzania haswa kipindi hiki cha kampeni. Dr. Abbas, hili usilinyamazie. Tukinyamaza, dunia itawaamini BBC wataonekana ni wa kweli.
Waelezeni BBC London na dunia ielewe kuwa hakuna makubaliano mawili kati ya serikali yetu na Barrick, makubaliano ni mamoja tuu, mkataba ni mmoja tuu, ambapo, japo tumepigwa fulani, lakini Tanzania ndio wafaidika wakubwa wa mkataba huo!.
Ofisi za Twiga ziko Mwanza Tanzania, na Accounts za Twiga ziko City Bank ya Tanzania!.
Namalizia kwa hili swali, Je, uongo na upotoshaji huu wa BBC London, kuhusu Tanzania kipindi hiki cha kampeni, kwa kuiepuka ilani ya CCM, kujadili ilani za Chadema na ACT tuu ni wa kawaida tuu kwenye media, au una maana gani?
Tukitafuta kitu kinachoitwa
the motive behind, haiwezi kuwa ni mbinu za mabeberu? Wapi weledi wa Ki-BBC?
Paskali