plan z
JF-Expert Member
- Jun 10, 2019
- 1,394
- 1,434
UONGO TULIOAMINISHWA KUHUSU FEDHA
Nafahamu wengi wetu tumejaribu kwa namna mbalimbali kutafuta kanuni ya fedha. Hebu jiulize binafsi ni vitabu vingapi umesoma, semina ngapi umehudhuria, maombi mangapi umeomba, ushauri ngapi umefuata. Lakini huoni matokeo yeyote.
Bado umestuck kwenye shughuli ambayo huipendi, na umejaribu kujinasua umeona imeshindikana.
Lakini ukiangalia pembeni unaona wengine kama wameneemeka tena wengine unaona ni wadogo kuliko wewe na ndipo unapoanza kupatwa na hasira na kujihisi una laana na maneno mengine mabaya unajinenea.
Je kama nikikuambia ulidanganywa, je kama nikikuambia kanuni nyingi za fedha ulizoambiwa ni uongo. Fuatana nami
Sasa tuangalie namna tulivyodanganywa kuhusu fedha bila kupoteza muda.
1. BIDII
Sasa hivi ukifuatilia kila mahali, ukijaribu kutafuta kanuni ya kufanikiwa au kuwa huru kifedha, utakutana na ushauri unaokuambia fanya kazi kwa bidii.
Sasa jilize swali lifuatalo, kwanini mfanya usafi pale ofisini anayetokwa na jasho kila siku katika kazi yake, anaingiza kiwango kidogo cha fedha kuliko mhasibu anayekaa kwenye meza na hatoi jasho lolote Je, dunia haina usawa? Je, hatupaswi kufanya kazi kwa bidii? Jibu ni hapana!
Mfanya usafi anaingiza kiwango kidogo cha fedha kuliko mhasibu anayekaa kwenye meza mda wote kwa sababu nafasi ya mfanya usafi inaweza kuchukuliwa na yeyote. Lakini nafasi yake mhasibu sio kila mtu anaweza kuichukua kama hafahamu chochote kuhusiana na fani hiyo.
Bidii tunayopaswa kufanya ni kutafuta maarifa ambayo yatatupa thamani kwenye maisha yetu na kufanya nafasi zetu ziwe ngumu kuchukuliwa.
Hapa simaanishi urudi shule ukaongeze elimu, kama wewe ni mfanya biashara angalia ni kwa namna gani utatatua matatizo yanayoikumba jamii yako, ongeza maarifa ya jinsi ya kuona fursa ambayo inatokana na uhitaji uliopo kwenye jamii yako.
Hivyo ndivyo namna ambavyo bidii inapotakiwa iwe, lakini namna tulivyodanganywa. Sasa mtu unaambiwa matajiri hawalali na wewe unaamua kukesha ili uwe kama wao. Then what???
Bidii yako inatakiwa iwe kwenye kubuni ni namna gani utatatua matatizo mbalimbali kwenye jamii. Na pesa zitakujia.
2. VITABU
Utasikia Bill Gates anasoma vitabu 50 kwa mwaka, sijui flani amesoma vitabu kadhaa! Then what???
Kwanini hivi vitabu vinakuwa promoted kwa kiwango kikubwa? Nini kipo nyuma ya pazia?
Swali la kujiuliza, unasoma vitabu mia moja kwa mwaka ili nini? Baada ya kuvimaliza unapata faida gani? Maisha yako yatakuwa yamebadilka kwa kiwango gani? Je unasoma kitabu ili ukimalize usome kingine? Au unasoma kitabu ili ukitendee kazi kibadilishe maisha yako ndipo uhamie kitabu kingine chenye mada tofauti.
Yes, kusoma vitabu sio mbaya, hata mimi nasoma vitabu. Lakini kuna dhana potofu imejengwa kwetu kuhusiana na vitabu, kuhusu mahusiano kati ya vitabu na utajiri au fedha. Unaamini kwamba ukisoma vitabu vingi ndipo utafanikiwa haraka au utapata fedha.
Soma vitabu vichache kwa mwaka, kisha vifanyie kazi, chukua hatua ya matendo, anza kufanyia kazi kile ulichojifunza, kisha ukiona unakwama rudi tena vitabuni ujifunze ni namna gani ya kuendeleza pale ulipoishia. Hakuna faida ya kusoma vitabu 100 kwa mwaka halafu hujachukua hatua yeyote ile. Vitabu havibadilishi maisha ya mtu bali vinatoa taarifa na miongozo ambayo ndiyo inaweza kubadilisha maisha ya mtu.
3. ELIMU
Jamii yetu inaamini ili ufanikiwe ni lazima uwe umesoma hadi upate angalau degree, kisha utafute kazi uajiriwe, uishi maisha yako yote, kisha ustaafu uchukue mafao yako usubirie uzee ukujie. Hata ukiacha kazi na kuamua kuanza biashara, bado jamii itakuona umepotea.
Kupata elimu au degree sio jambo baya, jambo baya ni kuwekeza akili yako kwenye ajira peke yake. Hausomi ili uajiriwe, unasoma ili upate maarifa yatakayokuwezesha kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii yako. Na kuajiriwa sio vibaya pia. Ila inatakiwa ifike hatua na wewe utoke ili uweze kuanzisha ajira kwa wengine. Ili na wengine waingie na chain iendelee hivyo.
HITIMISHO
Unapaswa kujua wewe ni bidhaa, hivyo chagua kwa makini. Unaposhindana kusoma vitabu 100 kwa mwaka, unawafaidisha waandishi. Sisemi usinunue, bali nunua vile ambavyo unaweza kuvitendea kazi.
Unapoongeza elimu ambayo hutaitendea kazi, unafaidisha taasisi za elimu. Sisemi usiongeze elimu, ila ongeza elimu ukiwa unajua unaenda kuitendea kazi.
Vilevile kuna mambo mengi unaweza ukajifunza online na ukawa vizuri kuliko aliyekaa darasani miaka mingi akijifunza kitu hichohicho kimoja. Lakini wewe unaweza ukamaliza kwa mda mfupi kulingana na kichwa chako.
DON'T FORGET TO SHOW SOME LOVE.