Uongo uliowahi kutokea JF: Kila mtu kujifanya tajiri na ana maisha mazuri

Uongo uliowahi kutokea JF: Kila mtu kujifanya tajiri na ana maisha mazuri

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Kwamba, kila mtu ni tajiri…

Kila mtu ana gari/ magari.

Kila mtu ana digrii. Kila mtu ana nyumba.

Kila mtu ana nguvu [nyingi] za kiume.

Kila mdada ana umri chini ya miaka 20.

Kila mtu hivi. Kila mtu vile.

Ili mradi tu ni ‘kila mtu’.

Huo ni uongo. Ni uzushi.

Hakuna sehemu yoyote ile ambayo ‘kila’ mtu anasema alivyo na/au alichonacho.

JF ina wanachama mamia ya maelfu.

Kusema kwamba kila mmoja wao hao watu huwa anasema hayo yanayosemwa, ni uzushi mkubwa.

Mliozoea kutunga uongo acheni mara moja.

Hamjawahesabu wanachama wote wa JF, wa kwanza hadi wa. mwisho, na kupata mitazamo yao juu ya mambo mbalimbali.

Kukaribisha uzushi kama huo kichwani mwako kunaonyesha jinsi mtu alivyo goigoi wa kufikiri.

And with that, I yield the balance of my time for others to chime in.

Happy hump day 😉.
 
Jf kila mtu anakaa sehemu za kishua!

Hakuna anayekaa Tandale, Buguruni Malapa, Vingunguti n.k

Jf hakuna anayekaa nje ya mji, wote wako pembeni kidogo tu ya mji na hawapandi daladala wanaenda kazini kwa gari zao binafsi.
 
Nilivyojiunga jf mara ya kwanza niliogopa sana maana kila mtu ni tajiri ila baada ya wiki moja nikakutana I'd mpya imefunguliwa alafu imeleta uzi wa kuomba buku mbili akanywe chai maana hajala siku 3, jamaa alivyosaidiwa akapata buku mbili zilifunguliwa I'd mpya nyingi sana kila mtu anaomba buku mbili ndo nikajua humu jf wamejaa watu miyeyusho tu.
 
Jf kila mtu anakaa sehemu za kishua!

Hakuna anayekaa Tandale, Buguruni Malapa, Vingunguti n.k

Jf hakuna anayekaa nje ya mji, wote wako pembeni kidogo tu ya mji na hawapandi daladala wanaenda kazini kwa gari zao binafsi.
Hizo ni assumes mnazozifanya kwenye vichwa vyenu sijawahi kuona member wa Jf anajitangaza eti ana gari na nyumba kali labda Chief Godlove .
 
Kigezo gani kimetumika kuhakiki hoja hii. Uongo ni hulka ya mtu, wapo wanaoleta hali halisi za maisha yao wanayopitia na wanapata msaada, wengine wanatunga stories. Ni wazi na uzi huu pia una kasoro ya kuwekwa "Kila mtu" humu JF yupo hivyo, kitu ambacho si kweli.
 
Kwamba, kila mtu ni tajiri…

Kila mtu ana gari/ magari.

Kila mtu ana digrii. Kila mtu ana nyumba.

Kila mtu ana nguvu [nyingi] za kiume.

Kila mdada ana umri chini ya miaka 20.

Kila mtu hivi. Kila mtu vile.

Ili mradi tu ni ‘kila mtu’.

Huo ni uongo. Ni uzushi.

Hakuna sehemu yoyote ile ambayo ‘kila’ mtu anasema alivyo na/au alichonacho.

JF ina wanachama mamia ya maelfu.

Kusema kwamba kila mmoja wao hao watu huwa anasema hayo yanayosemwa, ni uzushi mkubwa.

Mliozoea kutunga uongo acheni mara moja.

Hamjawahesabu wanachama wote wa JF, wa kwanza hadi wa. mwisho, na kupata mitazamo yao juu ya mambo mbalimbali.

Kukaribisha uzushi kama huo kichwani mwako kunaonyesha jinsi mtu alivyo goigoi wa kufikiri.

And with that, I yield the balance of my time for others to chime in.

Happy hump day 😉.
Mkuu umerudia kusoma ulichopost???
 
Wewe nyani ngabu na wenzako enzi hizo mlikuwa mnaringa sana kujipost mpo ughaibuni location nzuri nzuri na ndinga kali kali na mkija bongo mnatembelea classic locations sio uswazi kwa hela za kusukuma box.

Ulitegemea na sisi tukae kinyonge sio tuwaache mtuchukulie mademu zetu kisa nyie ni wabeba box?

Ilikuwa lazima na sisi tujimwambafai ili angalau ku mantain status zetu.
 
Back
Top Bottom