Uongo wa karne huu: Mwanamke sura! Tabia inatengenezwa

Uongo wa karne huu: Mwanamke sura! Tabia inatengenezwa

Dah sjajua nyie wenye sura mbaya tuwasaidiaje .ila wanaume wanaume wanaopenda sura mbaya wapo .ila kuwen nao makini wameamua kujilipua huwez ishi na mwanamke ana sura kama nsyuka halafu dishi kichwan likawa sawa
Leo wenye sura mbaya zamu yetu kunangwa...nipo hapa mbunge wao tiririkeni na wakati huo mkumbuke hatukujiumba na hakuna namna tutakuwa tofauti na hivi tulivyo ndo tumeshazaliwa. Msisahau pia na kutupa ushauri tufanyeje ili tuweze kuonekana na sisi kwamba ni wanawake na tuna mahitaji yale yale kama wanawake wengine wenye chura na sura nzuri
 
Hii kauli mkuu siwezi kuikataa moja kwa moja,lakini ikiwa ni hivi nadhani tutaangukia pua tukiwa na maamuzi haya au mfano wa haya.

Unajua kaka kwa watu waliooa tunajua fika kwamba uzuri wa sura haumati sana kiasi iwe kigezo cha kuoa ni sura tu pasi na kuangslia tabia,au iwe kigezo cha kuoa ni chura tu pasi na kuangalia tabia.

Mwanamke ukimpenda umbo lake,ukaipenda tabia yake,ukaipenda sura yake hata kama wengine wakamuona sio mzuri lakini kwa kuwa umempenda basi hilo ndo linahitajika kwa mwanaume ili amuoe mwanamke.

Lakini sasa mwanaume unapoangalia sura tuuuu ukasahau tabia,au ukaangalia chura tuuu ukasahau tabiaa huku hivyo ndo vigezo vyako vya kuchagua basi hapo hakiya Mungu utaangukia pua tu.

Ni kwa sababu ya uhalisia kwamba mwanaume anahitaji mwanamke ambaye atamuona mzuri machoni mwake,mwanaume anahitaji heshima ya kusikilizwa ndani,kuheshimiwa na kutiiwa pamoja kumjulia mume huyo.

Uzuri wa sura bwana ni rahisi kutengeneza kuliko kutengeneza uzuri wa tabia,yaani kuifanya sura iwe nzuri ni rahisi sana,lakini kuifanya tabia iwe nzuri aisee hapo ni kasheshe kuuuuuuubwaaa sana.

Unajua uzuri wa tunayemuona upo machoni mwetu,wakati huo tabia ipo kwa yule mtu mwenyewe.

Yaani nskusudia,unaweza kumuona mwanamke fulani mzuri alafu ajabu anakuja mtu anasema mbona wa kawaida tuuuuuu? Ni kuonyesha tu kwambaa uzuri wa mtu fulani watu wanaweza kutofautiana.

Ila mtu akiwa na tabia nzuri zinazojulikana kuna watu wanaweza sema kwamba mbona mimi tabia ile kwangu sio nzuri?

Yaani mfano mtu aseme yule binti fulani anawaheshimu watu mpole ila mbons kwangu tabia hizo sio nzuri? Yupo huyo mtu timamu? Bila shaka hayupo..

Sasa hapo ndo tunajua kwamba uzuri wa tabia ni kitu ambacho kinafahamika kwa watu woteeee hawatofautiani.

Ni muhimu sana kuchagua mwenye sura unayoipenda lakini usitupe na kusema unataka miss wa dunia,usichague saaaana.inatakiwa uoe mwanamke uweze kumkemea,kumuelekeza,kumnunia n.k.

Hhawa wanawake bhana akiwa na tabia njemaa romantic analishwa vizuri,anakunwa vizuri furaha tele utamuona mzuri tuuuu mkuu.

Watu wanakula mahouse girl zao baada ya kuwaleaa weeeee alafu mwisho wa siku wanawaona wananona,wanawaona wazuriiii kumbe macho yao wakati ungine.


Ushauri wangu ni tuangalie vigezo vyetu tunavyopenda lakini tabis ndio nguzo kuu,ndoa ina shida na raha,lszims upate mwanamke imara.

Sio mpo katika dhiki mwanaume uwe na kszi mbili,yaani kazi ya kwanza kupambana na dhiki alafu kazi ya pili ni kumuelwesha na kumuaminisha mkeo kwamba mupo kwenye dhiki alafu ukute hakuelewi,hapo ndo utaona kwamba kumbe kuna haja ya kuchagua tabia naayo.

Mwanamke mwema mkiwa kwenye dhiki anakuliwaza nafsi na kukutia moyo huku ukipunguza kazi mojs ambayo muoa sura na chura inamkabili.

Uzuri25% + chura25%+tabia 50%= ndoa imara
Sasa kwanini uoe nwanamke asiyependwa na watu wengine?
 
Kila mwanadamu anadeserve to love and be loved ...upendo ndo mwisho wa yote ukiwa na upendo ubaya wa mwenzi wako hutouona....tujifunze upendo kilamtu anastahiri na anahaki ya kupenda na kupendwa
Huyo wa pembeni alieshika mike anaitwa Lizzie Velásquez she is suffering from marfan syndrome Mwaka 2006 alikuta video yenye picha zake YouTube zikimuongelea kama the most ugliest woman in world na sisi yeye aliweka wenzake walikuwa wakimsakama na hali yake pind yupo high school.najua sio vizur kusema MTU kutokana na hali yake binadamu wote sawa every one deserve love.swali langu je unaweza ukaoa huyo ?tukiangalia na reference kile ulichosema hapo juu ?
908b10cc316103521ea76ce9446cc893.jpeg
 
Kuulizia sawa ila unaulizia tabiaa zake na mwenendo wake.

Sio uulizie mzurieeeeh?

Unaonaje shepu yake au sura yakee?

Ninachokimaanisha ni kuwa kupenda jinsi alivyo kimaumbile unatakiwa uiskilize nafsi yako,lakini kuhusu tabia na mwenendo wake lazima uwaulize wanaomfahamu vizuri.

Kuuliza hakuna mafungamano na kupenda.

Au utawaulia. Kama wamempenda au
Ulizia majirani mwanamke unayetaka kumwoa.
 
Safuha, Nakupata vizuri ujue...nabaki pale pale.

Kwanini umpende mtu asiyependwa na watu?

Wewe ndiye mwokozi wake.!
 
Hakuna mtu mbaya. Kwako akiwa mbaya kwa wengine mzuri.
 
Huyo wa pembeni alieshika mike anaitwa Lizzie Velásquez she is suffering from marfan syndrome Mwaka 2006 alikuta video yenye picha zake YouTube zikimuongelea kama the most ugliest woman in world na sisi yeye aliweka wenzake walikuwa wakimsakama na hali yake pind yupo high school.najua sio vizur kusema MTU kutokana na hali yake binadamu wote sawa every one deserve love.swali langu je unaweza ukaoa huyo ?tukiangalia na reference kile ulichosema hapo juu ?View attachment 969526
Upendo sio lazima umuoe hpana kumjari kumthamini kumuonesha kuwa ni wathamani na wakipekee katika hii dunia kuwa karibu nae kumsikiliza ,kutembea nae njiani ukiwa umemshika mkono yan kumake sure anafeel good upendo ni mpana sana mkuu kwaio uyo mwanamke anastairi kupendwa na kutendewa matendo ya upendo refer wimbo wa ambwene mwasongwe UPENDO
 
Macho yako yatakuwa yana matatizo mkuu embu muuangalie vizur .ukimtambulisha mbele za watu unaweza ambiwa umeoa mwanaume mwenzako
Usiishi kutokana na watu wanasemaje mkuu ukiwa na upendo ata huoni kama anasura ya baba
 
Hapa kwenye huu uzi wanazungumzia upendo wa kuoa
Upendo sio lazima umuoe hpana kumjari kumthamini kumuonesha kuwa ni wathamani na wakipekee katika hii dunia kuwa karibu nae kumsikiliza ,kutembea nae njiani ukiwa umemshika mkono yan kumake sure anafeel good upendo ni mpana sana mkuu kwaio uyo mwanamke anastairi kupendwa na kutendewa matendo ya upendo refer wimbo wa ambwene mwasongwe UPENDO
 
Mwanamke ni bidhaa kwa mujibu wa mila za kiAfrika ndio maana tunalipia mahari. Suala la msingi ni kuchagua bidhaa ambayo gharama yake unaweza kuimudu.
Hiyo midori unayoisifia, ni ngumu kuimudu kama hautakuwa na pesa za kuchezea.
Kumbuka mwanamke hatulii wala kutulizwa, mpaka ajitulize mwenyewe na Mwanaume, hatulii mpaka atulizwe.
Suala la msingi ni kutafuta atakayeweza kukidhi haja ya moyo wako na mahitaji yako.
 
Baba hapa hatuongelei uchi wala nguo, hapa mjadala ni shepu.

Hayo mambo ya wazungu tuachane nayo, tuongelee flavor zetu blacks kwanza, maana kama hujui Mungu alimuumba adam akiwa black wazungu walitokea baadae sana, kuna ushahidi kuwa race ya wazungu inatokana na malaika walio asi, fallen angels.
Hiyo ya Adam kuwa alikua black naisikia kwa mara ya pili.. Nitaifuatilia, ila ukiingia deep utasaidia mkuu....
 
Kupenda unakokuzungumzia ni kupi?

Tabiaa zake?

Au maumbile yake jumla alivyo?

Alafu pia ikiwaa watu hawajapenda muonekano wa mkeo kimaumbile alafu ikawa wewe umempenda jee utamuacha kwa kuwa watu hawajampenda maumbile yake tu?
Nakupata vizuri ujue...nabaki pale pale.

Kwanini umpende mtu asiyependwa na watu?

Wewe ndiye mwokozi wake.!
 
Kupenda unakokuzungumzia ni kupi?

Tabiaa zake?

Au maumbile yake jumla alivyo?

Alafu pia ikiwaa watu hawajapenda muonekano wa mkeo kimaumbile alafu ikawa wewe umempenda jee utamuacha kwa kuwa watu hawajampenda maumbile yake tu?
Kisichopendwa na wengine hata Mungu hakipendi.

Asiyependwa na binadamu wengine isipokuwa wewe tu jua mnakasoro wote.

Nakuonya tena " Usimpende mwanamke asiyependwa na watu" kwani unapooa unaolea jamii hauoi kwa ajili yako tu.

Nimemaliza.
 
Kisichopendwa na wengine hata Mungu hakipendi.

Asiyependwa na binadamu wengine isipokuwa wewe tu jua mnakasoro wote.

Nakuonya tena " Usimpende mwanamke asiyependwa na watu" kwani unapooa unaolea jamii hauoi kwa ajili yako tu.

Nimemaliza.
Wasiompenda watu hapendwi na Mungu kwa lipi?

Ina maana hata mimi nikisema mke wa fulsni sijapenda wembamba wake ina maana hata Mungu hampendi huyo mke wa fulani kwa kuwa mimi simpendi?

Huyo mungu atakuwa ni wewe mkuu.
 
Wasiompenda watu hapendwi na Mungu kwa lipi?

Ina maana hata mimi nikisema mke wa fulsni sijapenda wembamba wake ina maana hata Mungu hampendi huyo mke wa fulani kwa kuwa mimi simpendi?

Huyo mungu atakuwa ni wewe mkuu.
Hatuelewani.....Nikutakie Wakati mwema.
 
Back
Top Bottom