Uongo wa kiserikali umefika mwisho, tujisahihishe kwa Mbowe tujenge nchi

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Mwezi April 2021, Baada ya dakika chache tu ya kufariki Rais Magufuli aliyekuwa mfuasi kindakindaki wa hayati John Magufuli bwana Job Ndugai aliyeapa kumuongeza muda wa kutawala kidikteta Tanzania atake asitake, alimgeuka mchana kweupe na kulitangazia taifa kuwa serikali ya Rais John Magufuli ilikuwa ya UONGO MKUBWA kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Mimi nilimuunga mkono Ndugai kwa asilimia miamoja kuhusu mradi huu.

Sasa serikali ya Rais Samia nayo imetangaza rasmi kuwa serikali ya Rais Magufuli ilikuwa ya UONGO kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Haya yanadhihirishwa na kauli rasmi ya Serikali ya Tanzania iliyotolewa na Mh Waziri Mwambe katika kuhitimisha uongo wa serikali ya awamu ya tano kuhusu mradi huu.

Hili linanirejesha nyuma miaka miwili iliyopita 22 December 2019 nilipoandika Makala nikipinga hotuba ya Rais Magufuli akikataa kuendelea na ujenzi wa Mradi ya Bandari ya Bagamoyo, nilipinga hoja alizozijenga Rais ili kuhalalisha katazo lake juu ya mradi husika.

Nilieleza wazi kwamba, Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya mkataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na haki ya kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badala yake ingekusanya gawio toka kwa chombo cha wabia kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake.

Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha imeutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa. Moja ya hoja zilizotolewa na rais kama sababu ni kwamba masharti ya wabia nikuwa TRA hairuhusiwi kukusanya mapato, hoja hii ya Rais alikuwa sahihi lakini bahati mbaya alishindwa kufafanua wazi sababu za TRA kutokuwa miusanya mapato ya ubia. Pengine hili Rais alidanganywa.

Pili rais alisema kuwa masharti ya wabia nikuwa Tanzania hairuhusiwi kuendeleza bandari zake zingine. Hoja hii nayo inautata mwingi sana, Bandari zingine zote ziko kwaajili ya ndani, na mradi huu ulikuwa kwa shughuli za kimataifa. Sasa hoja ya kuwa tusikarabati bandari zetu zilizopo ni hoja isiyo na mashiko, Hili inawezekana kabisa Rais hakuambiwa ukweli. Leo Serikali ya Rais Samia imetutangazia kuwa Rais Magufuli alikuwa MUONGO.

Hoja ya Tatu aliyoitumia Rais Magufuli kukataa mradi ule, ilikuwa kwamba, wabia wanataka wapewe umiliki wa ardhi kwa miaka 99. Hili si la mwekezaji bali la sheria zetu ambazo zinatoa uwekezaji katika ardhi kwa miaka 33 hadi 99. Sasa hoja hii haiwezi kuwa kwa wabia wawili tu kati ya watatu ikiwemo Tanzania yenyewe. Hili nalo kuna uwezekano watu waliamua kumpotosha rais wetu.

Chakusikitisha kwa nchi yangu, Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi Rais Magufuli kusitisha mradi, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5 za Kimarekani, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 tu juzi Tanzania tulipowazuia wazungu wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo kwakuwa ukihojihoji tu basi ukinusurika sana utaenda mochwari au Ubelgiji, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa mimi kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against na himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa hii tuliyonayo leo ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado unaiserve CCM kwanza kisha Taifa linatafsiriwa salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm, kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Hili limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, Eneo la Ujasusi wa Kidola Tanzania kuna vitengo vya wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho kilikuwa kiko free from politics party ni CMI (central military intelligence). Lakini bahati mbaya muundo na aina ya uongozi wa Magufuli ulikiingiza katika siasa pale kilipofanywa kuwa decision maker wa nchi, lakini upande wa foreign assets ndio wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi.

Naunga mkono hatua ya serikali kujisahihisha na kuacha kuishi kwa uongo na ulaghai kuhusu mradi huu na kuanza upya mazungumzo ya mradi. Mradi huu ni key economy ya nchi baada ya SGR kukamilika.

NASISITIZA, UONGO WA KISERIKALI UMEFIKA MWISHO, TUJISAHIHISHE KWA MBOWE TUJENGE NCHI.

Kwa undani zaidi Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
Kwamaelezo zaidi piga 0715865544
________________________

Nenda kwenye link hapo kapigie kura kitabu chako pendwa cha Ujasusi kiwe kitabu bora. 👇

View attachment 2016461
Nimekuelewa mkuu. Mradi huu ulikuja kuvunja ndoto za Zanzibar na bandari yake ya Mpigaduri lkn bahati Tanzania ikauzembea na sasa Msumbiji wameuokota. Ujasusi wetu wa kiuchumi mara nyingi unaangalia humu ndani na hauna macho maangavu kuangalia nje. Ni bahati mbaya. Tujisahihishe
 
Kwamjibu wa mapendekezo ya mkataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na haki ya kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badala yake ingekusanya gawio toka kwa chombo cha wabia kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.
hapa kwenye TRA kutokukusanya kodi ndipo sijakuelewa, kwamba huu mradi utakua haulipi Kodi au
 
Hata wewe ni mnafiki tu ulisema Lowasa ni fisadi
20211028_123608.jpg
 
Binafsi sijawahi kuamini kilichosemwa na Magufuli kuhusu mradi wa bandari ya bagamoyo naona yeye alitaka tu kuonesha umwamba wake kwamba yeye sasa ni top akitaka jambo fulani lifanyike litafanyika na akikataa halifanyiki kama alivyoamuru kuvunjwa sehemu ya lile jengo la TANESCO pale ubungo.
 
Hata mradi wa gesi mtwara ulikuwa na maelezo kama hayo.
Lakini manufaa yake hadi leo ni hadithi tu.
Kwenye SSIT hakika bado sheria na mfumo umakaa kichamaa kulindwa kwa gharama zote kuliko maslahi ya Taifa.
Mfano;
CDF,IGP,TISS DIR awamu ya 5&6 wamekuwa kazi kubwa kuhudhuria matukio ya kiserikali na makalipio hadharani kwenye media.
CDF kweli awe anapanga foleni uwanja wa ndege kumpokea kiongozi wa serikali.
 
Binafsi sijawahi kuamini kilichosemwa na Magufuli kuhusu mradi wa bandari ya bagamoyo naona yeye alitaka tu kuonesha umwamba wake kwamba yeye sasa ni top akitaka jambo fulani lifanyike litafanyika na akikataa halifanyiki kama alivyoamuru kuvunjwa sehemu ya lile jengo la TANESCO pale ubungo.
Dawa huo uchawa ndani ya chama kimoja watoe mikataba ichambuliwe,tutajua nani mpigia debe
 
Hakuna haja ya kuuzunguka mbuyu daima, utapata kizunguzungu buree! Yoote uliyoandika yanatafsirika kirahisi kabisa kwama muarobaini ni KATIBA MPYA!

Huwezi kuniridhisha na maelezo kwamba eti Rasi alidanganywa, yeye hajua kusoma? Na kwanini akubaliane na mtu mmoja au kundi moja?

Kuna wataalamu kutoka vyuo vikuu, bungeni and serikalini kwenyewe, Balozi tele ambazo zingetakiwa kutoa tafsiri huru ya mkataba tena hata Vyama vya upinzani vingetakiwa vishirikishwe, kwani wao siyo Raia? na Wazalendo pia?

Ni bora ungeandika kitabu kingine chenye kuelezea umuhimu wa Tanzania kupata Katiba Mpya!
 
Yericko ni moja ya vijana wenye uwezo mzuri ki fikra na uzalendo wa kitaifa ,Kama ilivyo kwa watu wengi aina yake bahati mbaya serikali hufikiri kila mtu anaye jitanabahisha kuwa ana amini itikadi na falsafa za upinzani ni adui.

Hatari sana kuona kila anaye onekana anafikiri kinyume na watawala ni mbaya.

Tujifunze kuishi maisha ya kupingana kwa hoja
 
Halafu Prof. Asad akamla kichwa kisiasa yaan ma ccm yanaushi sana yaan mtu anaekuambia ukweli na kutaka kuafnya maendeleo ya kitaasis unamueka pembeni am kweli Mimi nilifika hapo hua najiona jiniasi kwa aina ya viongozi tulio nao walah Mimi na akili
 
Mwezi April 2021, Baada ya dakika chache tu ya kufariki Rais Magufuli aliyekuwa mfuasi kindakindaki wa hayati John Magufuli bwana Job Ndugai aliyeapa kumuongeza muda wa kutawala kidikteta Tanzania atake asitake, alimgeuka mchana kweupe na kulitangazia taifa kuwa serikali ya Rais John Magufuli ilikuwa ya UONGO MKUBWA kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Mimi nilimuunga mkono Ndugai kwa asilimia miamoja kuhusu mradi huu.

Sasa serikali ya Rais Samia nayo imetangaza rasmi kuwa serikali ya Rais Magufuli ilikuwa ya UONGO kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Haya yanadhihirishwa na kauli rasmi ya Serikali ya Tanzania iliyotolewa na Mh Waziri Mwambe katika kuhitimisha uongo wa serikali ya awamu ya tano kuhusu mradi huu.

Hili linanirejesha nyuma miaka miwili iliyopita 22 December 2019 nilipoandika Makala nikipinga hotuba ya Rais Magufuli akikataa kuendelea na ujenzi wa Mradi ya Bandari ya Bagamoyo, nilipinga hoja alizozijenga Rais ili kuhalalisha katazo lake juu ya mradi husika.

Nilieleza wazi kwamba, Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya mkataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na haki ya kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badala yake ingekusanya gawio toka kwa chombo cha wabia kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake.

Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha imeutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa. Moja ya hoja zilizotolewa na rais kama sababu ni kwamba masharti ya wabia nikuwa TRA hairuhusiwi kukusanya mapato, hoja hii ya Rais alikuwa sahihi lakini bahati mbaya alishindwa kufafanua wazi sababu za TRA kutokuwa miusanya mapato ya ubia. Pengine hili Rais alidanganywa.

Pili rais alisema kuwa masharti ya wabia nikuwa Tanzania hairuhusiwi kuendeleza bandari zake zingine. Hoja hii nayo inautata mwingi sana, Bandari zingine zote ziko kwaajili ya ndani, na mradi huu ulikuwa kwa shughuli za kimataifa. Sasa hoja ya kuwa tusikarabati bandari zetu zilizopo ni hoja isiyo na mashiko, Hili inawezekana kabisa Rais hakuambiwa ukweli. Leo Serikali ya Rais Samia imetutangazia kuwa Rais Magufuli alikuwa MUONGO.

Hoja ya Tatu aliyoitumia Rais Magufuli kukataa mradi ule, ilikuwa kwamba, wabia wanataka wapewe umiliki wa ardhi kwa miaka 99. Hili si la mwekezaji bali la sheria zetu ambazo zinatoa uwekezaji katika ardhi kwa miaka 33 hadi 99. Sasa hoja hii haiwezi kuwa kwa wabia wawili tu kati ya watatu ikiwemo Tanzania yenyewe. Hili nalo kuna uwezekano watu waliamua kumpotosha rais wetu.

Chakusikitisha kwa nchi yangu, Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi Rais Magufuli kusitisha mradi, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5 za Kimarekani, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 tu juzi Tanzania tulipowazuia wazungu wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo kwakuwa ukihojihoji tu basi ukinusurika sana utaenda mochwari au Ubelgiji, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa mimi kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against na himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa hii tuliyonayo leo ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado unaiserve CCM kwanza kisha Taifa linatafsiriwa salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm, kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Hili limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, Eneo la Ujasusi wa Kidola Tanzania kuna vitengo vya wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho kilikuwa kiko free from politics party ni CMI (central military intelligence). Lakini bahati mbaya muundo na aina ya uongozi wa Magufuli ulikiingiza katika siasa pale kilipofanywa kuwa decision maker wa nchi, lakini upande wa foreign assets ndio wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi.

Naunga mkono hatua ya serikali kujisahihisha na kuacha kuishi kwa uongo na ulaghai kuhusu mradi huu na kuanza upya mazungumzo ya mradi. Mradi huu ni key economy ya nchi baada ya SGR kukamilika.

NASISITIZA, UONGO WA KISERIKALI UMEFIKA MWISHO, TUJISAHIHISHE KWA MBOWE TUJENGE NCHI.

Kwa undani zaidi Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
Kwamaelezo zaidi piga 0715865544
________________________

Nenda kwenye link hapo kapigie kura kitabu chako pendwa cha Ujasusi kiwe kitabu bora. 👇

View attachment 2016461
Haaa! unanikumbusha usemi huu 'pesa zipoo!'
 
Magufuli hakukataa huu mradi bali alikataa yaliyomo kwenye mkataba wa kuanzisha mradi kwa manufaa ya nchi...Mradi unapoanza kutekelezwa ni muhimu uwekwe wazi ili tujue kama kuna marekebisho au la...na kama tukiamua kuendelea nao hivyo hivyo basi tufahamu.Mifano ya miradi hii haijafanya vizuri na mingi inaingiliana na sovereignty ya nchi husika.Mfano Djibouti...tusidanganywe na masuala ya ajira kwani viwanda vya kisasa vinapimwa na kuwa na wafanyakazi wachache...tusisahau pia kuwa tunazo bandari nyingine za Tanga..Mtwara na Zanzibar ambazo tunazimiliki wenyewe na ambazo tumetumia fedha nyingi kuzikarabati na kuziongezea uwezo.
 
Back
Top Bottom