Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi issues nafikiri ni Mimi tu kumbe ni majanga. Ninaomba kama Kuna mwanasheria humu tufungue kesi ya huu wizi ili kukomesha huu unyang'anyi na ujambazi... kwa sababu huu ni wizi kama wizi mwingne..Kutokana na matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi ya vifurushi vya Internet. Tarehe 01/08/2022, nilijiunga na kifurushi cha Tsh.1500 (Mb850) na niliamua kuanza kufuatilia na kujipimia matumizi ya vifushi vya Internet kwenye simu yangu kupitia Mobile data usage ambapo nilipata fursa ya kuweka ukomo wa matumizi ya kifushi nilichojiunga kwa siku nisizidishe Mb100.
Lakini cha ajabu niliweza kutumia Jumla ya Mb490 pekee na kuletewa ujumbe kuwa nimetumia kifurushi cha Internet kwa 100%.
Nilishangaa sana na kugundua kuwa kumbe hivi viwango wanavyotuandikia ni Uongo mtupu. Huu mtandao wanafanya utapeli mkubwa sana.
Pamoja na maelezo haya nimeambatanisha screenshot za manunuzi ya kifurushi na matumizi.
Kama kuna mtu anaweza fuatilia pia ajaribu atajionea mwenyewe.
View attachment 2316699View attachment 2316700View attachment 2316701
Kaka umepigwa hapaNdani ya dk kumi kifurushi kimetoka 75% hadi kuisha kabisa. Nimeamini airtel ni wezi. Ngoja tuendelee na zantel, naona ina unafuu 200%View attachment 2322089
Duh....[emoji16][emoji16]Inategemea aina matumiz na aina simu , kama simu Ina ram kuanzia 3 , bando lazima itembee
Utupe mrejesho huko zantel ili tujisogeze mkuuNdani ya dk kumi kifurushi kimetoka 75% hadi kuisha kabisa. Nimeamini airtel ni wezi. Ngoja tuendelee na zantel, naona ina unafuu 200%View attachment 2322089
Nimejiunga hiki kifurushi saa 7:20 asubuhi, mpaka saa 8:33 asubuhi hiyohiyo natumiwa ujumbe wa kumaliza kifurushi changu. Nimeingia whatsapp, JF na nimecheza game kidogo tu kama dk 10. Nahisi airtel leo wamenipiga mchana kweupee. Na sina mpango wa kujiunga tena, mpaka kesho hiyo ndio watapata buku yangu tena!Airtel na wao leo wamepunguza vifurushiView attachment 2400063View attachment 2400064