Uongo wa vifurushi vya Intaneti vya Airtel Tanzania

Uongo wa vifurushi vya Intaneti vya Airtel Tanzania

Airtel sina hamu nao asee.., yaani nmejiunga kifurushi cha wiki nkaingia zangu jamii forum kidogo tu naambiwa Mb zimeisha
 
Airtel sina hamu nao asee.., yaani nmejiunga kifurushi cha wiki nkaingia zangu jamii forum kidogo tu naambiwa Mb zimeisha
Acheni kulalamika,Angalieni settings za simu zenu. Unakuta mtu kaweka auto update, au download Whatsap huko halafu ana magroup yanayo tuma video. Ana lalamika tuu...

Mtandao unao kula Mb zaidi ni Voda Kwa sababu ya Kasi yake. Inayo fuata ni Halotel


Airtel?? [emoji28] . Unajiunga mpaka unajiuluza mbona mb haziishi?

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Kutokana na matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi ya vifurushi vya Internet. Tarehe 01/08/2022, nilijiunga na kifurushi cha Tsh.1500 (Mb850) na niliamua kuanza kufuatilia na kujipimia matumizi ya vifushi vya Internet kwenye simu yangu kupitia Mobile data usage ambapo nilipata fursa ya kuweka ukomo wa matumizi ya kifushi nilichojiunga kwa siku nisizidishe Mb100.

Lakini cha ajabu niliweza kutumia Jumla ya Mb490 pekee na kuletewa ujumbe kuwa nimetumia kifurushi cha Internet kwa 100%.

Nilishangaa sana na kugundua kuwa kumbe hivi viwango wanavyotuandikia ni Uongo mtupu. Huu mtandao wanafanya utapeli mkubwa sana.

Pamoja na maelezo haya nimeambatanisha screenshot za manunuzi ya kifurushi na matumizi.

Kama kuna mtu anaweza fuatilia pia ajaribu atajionea mwenyewe.

View attachment 2316699View attachment 2316700View attachment 2316701
Ni kweli kabisa. Siku hizi internet inaisha tu hata bila kutumia
 
Acheni kulalamika,Angalieni settings za simu zenu. Unakuta mtu kaweka auto update, au download Whatsap huko halafu ana magroup yanayo tuma video. Ana lalamika tuu...

Mtandao unao kula Mb zaidi ni Voda Kwa sababu ya Kasi yake. Inayo fuata ni Halotel


Airtel?? [emoji28] . Unajiunga mpaka unajiuluza mbona mb haziishi?

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Hapana ni wezi tu, mimi mwaka 4 internet natumia airtel ila recently wameshusha vifursh na wakaanza kutuibia
 
Nadhani ifikie hatua tuache kulalamikia huu WIZI..mimi ninajipanga kuwafungulia kesi ya madai ili UTAPELI HUU UKOME...niliweka GB 2.7 AMBAZO WANAUZA ELF 5, baada ya matumizi ya siku 2 tu wakasema nimetumia asilimia 75 ya bando, ile namaliza kuisoma tu hiyo msg inafuata nyingine nimetumia asilimia 100!!! yaani kuna ujambazi mkubwa kwenye hii sekta....
Wengi tutakua nyuma yako boss wew wafungulie tu
 
Kwa Nape usitegemee kitu kwani ana majibu meoesi na ya hovyo kwenye mambo muhimu na siriaz kama haya.View attachment 2316712
Nape amekuwa mtetezi wa makampuni. Ameji-position nafasi ya operation managers/CEO anayejua operation costs za kampuni.

Anahisi anajua kumbe wanamdanganya. Gharama za uzalishaji sio mafuta/nishati peke yake! Zipo nyingi. Ni jukumu la mameneja wa makampuni kuona eneo lipi wanaweza kupunguza hizo gharama ili waweze kupanga bei yenye unafuu kwa mlaji/mtumiaji.

Yeye anapaswa kusimama kwa niaba ya wananchi. Nape anamuangusha Mama Samia.
 
Nimeipenda hii ya TTCL Kuna bando hazina mda wa kuisha kwa line za special ambazo bei yake 1000 tu
Sio kuwa ni nzuri sana lakini angalau kwa watu walio bize mpaka bando Zina expire

Hilo ni salio la 1000
Ndugu mteja , Salio kuu: 1.0 TZS, litumike kabla ya [2023-08-06 09:48:49].
---
Jumla Data(MB): 659.87 MB, zinazo jumuisha , Bufee Data ni 659.87 MB, litumike kabla ya [2023-08-11 09:58:14]
 
Baada ya mda mrefu kutumia zantel kwa internet, jana network yao ikawa mbovu nikashindwa kujiunga. Ngoja nione airtel watanifanyaje na hii 1.95GB.
Screenshot_20220811-104526_Messages.jpg
 
Hiki kitu nilishawaambiaga humu, unanunua 1GB ila kimsingi unaungwa na qouta ya O.6GB, kwa sisi wenye uelewa kidogo na system zinavyofanya kazi ni rahisi tu, una edit statement tu ya ku display ujumbe unaandika uongo.

Mfano:
if (qouta ==O.6) {
print = "Umefanikiwa kujiunga na kifurushi cha week cha 1GB toka Airtel";
}

Ambacho utaona wewe ni huo ujumbe wa 1GB ila system imekuachia O.6GB kiuhalisia so unakuwa umepigwa 4OOMB bila kujua.
Zamani xvid

Hadi unachoka just 1Gb tu sa hivi video nne kwsha gb 1
 
Zamani xvid

Hadi unachoka just 1Gb tu sa hivi video nne kwsha gb 1
Wahuni sana hao mi nilihamia Zantel mazima huku walau mtandao ulikuwa chini ya mashehe wa kizenji wizi hakuna ila toka kanunua yule mwekezaji wa oysterbay polisi mambo yashaanza kuharibika sahizi huduma zimeungwa na Tigo.

Bado utapeli haujaanza rasmi ila mabadiliko flani nayaona
 
Bando la wiki hata ujitahidi vipi humalizi siku tatu
Bando la mwezi ni wiki 2 tu na hapo umejitahidi sana
Hakuna Instagram, TikTok wala YouTube
Hahahahah wahuni sana jamaa bora kujiungia ile TTCL fibre ya 5O,OOO ya nyumbani halafu waiweke iwe kama dstv mobile kuwa kifurushi chako unaweza tumia ukiwa unatembea hata kama hauko home.

Naamini TTCL wanaweza hilo wafanye haraka iwe unalipa 50,OOO ya fibre kisha unaweza itumia kwenye simu ukiwa unatembea kupitia line yao.
 
Back
Top Bottom