Uongo wa Viongozi wetu

Uongo wa Viongozi wetu

KASULI

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
599
Reaction score
677
Nimefungua uzi huu kama njia ya kuwakumbusha viongozi wetu sio kwamba hatujali ambavyo huwa wanatudanganya ili ni vile hatuna cha kufanya.

Hapa tutakuwa tukiweka baadhi ya yale ambayo tumekuwa tukiambiwa na viongozi na kutuaminisha wengine mpaka kwa viapo kumbe wanatuambia uongo.

Naanza mimi.....

1. Mkurugenzi mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa. Treni kuanza kusafirisha abiria kati ya Morogoro na Dar Es Salaam mwezi March 2023. Huu ni uongo ambao umedumu kwa miaka 4 sasa. Mara ya kwanza tuliambiwa treni ya abiria ya umeme ingeenza kazi mapema mwaka 2019. Haikuwaa ivyo ikawa ni dec 2020, chenga ikawa february 2021, kimya ikawaa july 2021, Kimya ikawaa June 2022 kimya ikawa Dec 2022 Kimya. Baadae yakaletwa mabehewa na ngonjera nyingi zikiongezwa chumvi na watetezi wa Mabehewa Feki, Msemaji wa Serikali, Waziri Mkuu na Waziri wa Uchukuzi, MAKAME MBALAWA.

Kwamba mabehewa yaliyokuja na mengine pamoja na vichwa yako njia yangefika hapa mapema February na Treni kuanza safari za majaribio mapema Machi na Kuanza kusafirisha Abiria mapema June mwaka huu. Huu UONGO kuongezwa Chumvi tukaletewa mpaka MIJADALA YA NAULI ZA SAFARI KUTOKA DAR MPAKA DODOMA. Binafsi sioni kinachoendeleaa Zaidi ya ziara za Mara huyu mara Yule. Leo wataenda Wabunge kesho wanafunzi keshokutwa ataenda Mbunge mmoja kesho wataenda wanne.

UONGO NI DHAMBI.
 
Kabisaa tuteme nyongo kwa kuwa mama alishasema anapitaa aone uongo wa wasaidizi wake......
 
Back
Top Bottom