Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Leo Rais wa Tanzania amehutubia taifa na kusema, utaratibu mzima wa upimaji na utoaji majibu ya vipimo kwa wahisiwa wa ugonjwa wa COVID-19 hapa Tanzania yamezungukwa na uongo, ujanja ujanja na ulaghai mkubwa. Hivyo takwimu zote za COVID-19 hapa Tanzania zilizotolewa na Waziri Mkuu au Waziri wa Afya zinapaswa kutiliwa mashaka na kutokuchukuliwa maanani tena. Ni upuuzi mtupu!
Sasa katika vita hii ya kupambana na Corona, jukumu la moja kwa moja lilikuwa chini ya Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) na waziri wa Afya (Ummy Mwalimu) huku pesa nyingi zikielekezwa huko. Wao ndio waliwahakikishia watanzania toka mwezi January, 2020 kabla ya Corona kuingia nchini Tanzania kuwa, Serikali ilikuwa imejipanga vyema katika mapambano hayo kuanzia kupima, kuzuia na kujaribu kutibu maambukizi ya Corona. Na mpaka kufikia leo wao ndio waliokuwa wamesimama mstari wa mbele kutetea na kusimamia juhudi za upimaji na utoaji majibu ya Corona kwa Tanzania.
Pasipo kuegemea upande wowote (iwe shutuma hizi za Rais ni kweli au ni uongo uliozushwa), nadhani huu ni wakati muafaka kwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Mama Ummy Mwalimu kutafakari namna ya kuachia ngazi.
Sababu za kufanya hivyo ni hizi hapa.
1. Kukubali kwao kuwajibika moja kwa moja kwa hizo shutuma dhidi yao (ikiwa ni kweli) na kulinda hadhi ya serikali na hadhi ya Rais aliyewateua.
2. Kukaa pembeni ili kulinda heshima zao au kuonyesha kutokukubaliana na hiyo kauli ya mheshimiwa Rais (ikiwa shutuma hizo ni uongo).
3. Kupisha uchunguzi kamili na wahusika wengine wachukue nafasi zao ili nao wawajibike kwa namna tofauti (maana juhudi zao za mwanzo zimeonekana ni uchafu na upuuzi mtupu mbele ya yule aliyewateua)