Uongo Wa Vipimo Vya Corona Tanzania: Kwanini Waziri Mkuu Na Waziri Wa Afya wasijiuzulu?

Uongo Wa Vipimo Vya Corona Tanzania: Kwanini Waziri Mkuu Na Waziri Wa Afya wasijiuzulu?

Hakuna ushahidi wa kisayansi unao watuhumu Waziri Mkuu na Waziri wa Afya.
Raisi kaonyesha dukuduku ya wingi wa positive kwa eneo ambalo anadai analifahamu vizuri.
Lakini yawezekana hizo samples was contaminated
Kuchukuwa samples kuna procedures, na katika hizo procedures from fetching a sample mpaka hatua ya mwisho makosa yaweza kufanyika ndio tunaita HUMAN ERROR au Equipment Error n.k
Tusitafute mbuzi wa kafara,huo ni mchezo mchafu.
 
Aliyepeleka sampuli za mapapai badala ya sampuli zilizokusudiwa ndo ana tatizo, mtaalamu atapima kile alichopelekewa na kusoma majibu. Ukimpotosha kwa kumpa kitu tofauti apime linakuwa siyo tatizo lake.....ina maana unataka afanye kazi ya ziada ya 'forensic' ili aweze kugundua kama hiyo sampuli ni genuine na hilo linaweza kufanywa na maabara tofauti au na wataalaamu tofauti, huna haja ya kufuata mlolongo wote huo....kuna namna bora ya kuthibitisha majibu ya vipimo hasa kama utakuwa umefanya 'rapid test' itabidi ufanye 'confirmatory test' hasa kwa zile sampuli ambazo ni positive au zile ambazo una mashaka na majibu yake......ila chonde chonde usipeleke sampuli ambazo hazikukusudiwa kwa lengo la kuwalaghai wapimaji...
 
Hii kitu ya COVID kwa TZ naona kama kawaida yetu imegeuka kuwa jambo fulani kama tamthiliya vile
 
Leo Rais wa Tanzania amehutubia taifa na kusema, utaratibu mzima wa upimaji na utoaji majibu ya vipimo kwa wahisiwa wa ugonjwa wa COVID-19 hapa Tanzania yamezungukwa na uongo, ujanja ujanja na ulaghai mkubwa. Hivyo takwimu zote za COVID-19 hapa Tanzania zilizotolewa na Waziri Mkuu au Waziri wa Afya zinapaswa kutiliwa mashaka na kutokuchukuliwa maanani tena. Ni upuuzi mtupu!

Sasa katika vita hii ya kupambana na Corona, jukumu la moja kwa moja lilikuwa chini ya Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) na waziri wa Afya (Ummy Mwalimu) huku pesa nyingi zikielekezwa huko. Wao ndio waliwahakikishia watanzania toka mwezi January, 2020 kabla ya Corona kuingia nchini Tanzania kuwa, Serikali ilikuwa imejipanga vyema katika mapambano hayo kuanzia kupima, kuzuia na kujaribu kutibu maambukizi ya Corona. Na mpaka kufikia leo wao ndio waliokuwa wamesimama mstari wa mbele kutetea na kusimamia juhudi za upimaji na utoaji majibu ya Corona kwa Tanzania.

Pasipo kuegemea upande wowote (iwe shutuma hizi za Rais ni kweli au ni uongo uliozushwa), nadhani huu ni wakati muafaka kwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Mama Ummy Mwalimu kutafakari namna ya kuachia ngazi.

Sababu za kufanya hivyo ni hizi hapa.
1. Kukubali kwao kuwajibika moja kwa moja kwa hizo shutuma dhidi yao (ikiwa ni kweli) na kulinda hadhi ya serikali na hadhi ya Rais aliyewateua.

2. Kukaa pembeni ili kulinda heshima zao au kuonyesha kutokukubaliana na hiyo kauli ya mheshimiwa Rais (ikiwa shutuma hizo ni uongo).

3. Kupisha uchunguzi kamili na wahusika wengine wachukue nafasi zao ili nao wawajibike kwa namna tofauti (maana juhudi zao za mwanzo zimeonekana ni uchafu na upuuzi mtupu mbele ya yule aliyewateua)
Mkuu wala hakuna sababu ya kuwapa nafasi ya kujitafajari, Kama aliyewateua anajielewa anapaswa kuwafuta kazi Mara moja,haiwezekani mama kilango Malechela aliyedanganya issue ya wafanyakazi hewa pale shinyanga atumbuliwe Mara moja lakini hawa waliotoa taarifa zilizozua taharuki ndani na nje ya nchi kiasi Cha kuua sector ya utalii,kuzuia watoto wa wanyonge kuendelea na masomo kwa miezi sasa,kuikosesha wanyonge ajira, kuisababishia serikali hasara za kununua masanduku na sanda na kuwazika watu usiku wapewe muda wa kujitafakari.haiwezekani
 
Dah!..baraza la mawaziri litavunjwa miezi michache ijayo kupisha uchaguzi,Sasa wakijiuzulu hicho kiinua mgongo chao (pension) utawapa wewe?
 
Leo Rais wa Tanzania amehutubia taifa na kusema, utaratibu mzima wa upimaji na utoaji majibu ya vipimo kwa wahisiwa wa ugonjwa wa COVID-19 hapa Tanzania yamezungukwa na uongo, ujanja ujanja na ulaghai mkubwa. Hivyo takwimu zote za COVID-19 hapa Tanzania zilizotolewa na Waziri Mkuu au Waziri wa Afya zinapaswa kutiliwa mashaka na kutokuchukuliwa maanani tena. Ni upuuzi mtupu!

Sasa katika vita hii ya kupambana na Corona, jukumu la moja kwa moja lilikuwa chini ya Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) na waziri wa Afya (Ummy Mwalimu) huku pesa nyingi zikielekezwa huko. Wao ndio waliwahakikishia watanzania toka mwezi January, 2020 kabla ya Corona kuingia nchini Tanzania kuwa, Serikali ilikuwa imejipanga vyema katika mapambano hayo kuanzia kupima, kuzuia na kujaribu kutibu maambukizi ya Corona. Na mpaka kufikia leo wao ndio waliokuwa wamesimama mstari wa mbele kutetea na kusimamia juhudi za upimaji na utoaji majibu ya Corona kwa Tanzania.

Pasipo kuegemea upande wowote (iwe shutuma hizi za Rais ni kweli au ni uongo uliozushwa), nadhani huu ni wakati muafaka kwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Mama Ummy Mwalimu kutafakari namna ya kuachia ngazi.

Sababu za kufanya hivyo ni hizi hapa.
1. Kukubali kwao kuwajibika moja kwa moja kwa hizo shutuma dhidi yao (ikiwa ni kweli) na kulinda hadhi ya serikali na hadhi ya Rais aliyewateua.

2. Kukaa pembeni ili kulinda heshima zao au kuonyesha kutokukubaliana na hiyo kauli ya mheshimiwa Rais (ikiwa shutuma hizo ni uongo).

3. Kupisha uchunguzi kamili na wahusika wengine wachukue nafasi zao ili nao wawajibike kwa namna tofauti (maana juhudi zao za mwanzo zimeonekana ni uchafu na upuuzi mtupu mbele ya yule aliyewateua)
wajiuzulu kwa sababu gani?watangaza data kama zilivyokuja.ulitaka wawabishie bila kuwa na reaearch.wapinzani tumieni akili siyo makalio kufikiri.juzi mmelazimisha data zitoke leo ooh wajiuzulu。you are like cameleon !!!Mliomba corona iingie nchini leo mnalialia .
 
Nina wasi wasi ukipeleka hata sampuli ya kuku unaweza kuta corona

Sasa kama papai zina corona tatizo ni nini!!
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UDSM ni chuo bora hufundisha kuwa kila mgogoro anza kuchambua source (causes) si effects!! kwa mawazo yangu hapa hakuna mtu kujiuzulu, wa kurara nae mbere kwa mbere na kutupa selo ni Afisa au Waziri yule alienunua vifaa feki vya maabara vya kupima Covid19, kisha kushitaki WHO na kudai pesa yetu kwa kampuni au kiwanda ambako vifaa vilipotoka, kwanza sheria ya manunuzi ilifuatwa? kisha kukagua kama bajeti ya kununua vifaa hivyo ni sawa na pesa iliyolipwa, kisha kuangalia miamala ya pesa na benki akaunti za watu waliolipa pesa ya serikali kununua vifaa hivyo, kisha kuangalia kama vifaa vyetu ni bora na ndivyo aina hiyo hiyo vyatumika US na UK kwa Boris!! kisha kuangalia kama Vifaa vyetu ni tekno au apple!!!

Tunaweza pia kuazima Kenya , US na UK vifaa wanavyotumia kupimia Covid19 ili tujiridhishe kisha tukarushia humo zile samples za mapapai na mafenesi na mbuzi na mbwa na za sokwe mtu na za wabunge na kuona majibu kama ni the same na mashine zetu inamaana nao wana takwimu feki!! Mzee Baba kwa hili ni Genius tuache wivu na uadui wa vyama ni lazima tumpongeze ni haki yake!
 
Mkurungenzi mkuu wa maabara ya Taifa mara baada ya hutuba ya Rais hivi leo!
africansafaris_B_iSBULpOZZ.jpg
 
Back
Top Bottom