Uongo Wa Vipimo Vya Corona Tanzania: Kwanini Waziri Mkuu Na Waziri Wa Afya wasijiuzulu?

Uongo Wa Vipimo Vya Corona Tanzania: Kwanini Waziri Mkuu Na Waziri Wa Afya wasijiuzulu?

Waziri Mkuu na waziri wa Afya wanapelekewa ripoti tu hata km una ujinga mwingi acha kujiaibisha
Imagine unatukanwa na mtu yuko mafichoni wewe ndo unarisk kwenye mikutano na misiba. Ila acha yatukanwe tu maana hawana namna hao ni walimu eeh wakiacha kazi watakula nini. Ukiambiwa kazi ni utumwa maana yake ndiyo hii.
 
Rais is a scientist who is very unscientific. Anataka kuleta vurugu tu. Hakuna vipimo ambavyo viko sahihi 100%. Viwe vya malaria, TB, huwa vina false positives na false negatives. Isitoshe vipimo hivi vilijaribiwa katika binadamu kwanza. Yeye ndiye wa kwanza kuvijaribu katika mapapai na kwale. Kama ilitokea vikawa positive kwa kwale haina maana kuwa positive zilizo kwa binadamu lazima ziwe za uongo. This is health science and not chemistry. Hakuna sababu ya ya msingi ya mtu yeyote kujiuzuru.
 
Kwamba PM anaweza pelekewa report yenye taarifa fake na kawajulisha Watanzania bado tuone ni kitu cha kawaida tu!! Labda sielewi maana ya Waziri Mkuu...Na nyie akina Bia yetu ndio mnapeleka taarifa za kijinga. Wapumbavu kabisa nyie
Waziri Mkuu na waziri wa Afya wanapelekewa ripoti tu hata km una ujinga mwingi acha kujiaibisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo Rais wa Tanzania amehutubia taifa na kusema, utaratibu mzima wa upimaji na utoaji majibu ya vipimo kwa wahisiwa wa ugonjwa wa COVID-19 hapa Tanzania yamezungukwa na uongo, ujanja ujanja na ulaghai mkubwa. Hivyo takwimu zote za COVID-19 hapa Tanzania zilizotolewa na Waziri Mkuu au Waziri wa Afya zinapaswa kutiliwa mashaka na kutokuchukuliwa maanani tena. Ni upuuzi mtupu!

Sasa katika vita hii ya kupambana na Corona, jukumu la moja kwa moja lilikuwa chini ya Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) na waziri wa Afya (Ummy Mwalimu) huku pesa nyingi zikielekezwa huko. Wao ndio waliwahakikishia watanzania toka mwezi January, 2020 kabla ya Corona kuingia nchini Tanzania kuwa, Serikali ilikuwa imejipanga vyema katika mapambano hayo kuanzia kupima, kuzuia na kujaribu kutibu maambukizi ya Corona. Na mpaka kufikia leo wao ndio waliokuwa wamesimama mstari wa mbele kutetea na kusimamia juhudi za upimaji na utoaji majibu ya Corona kwa Tanzania.

Pasipo kuegemea upande wowote (iwe shutuma hizi za Rais ni kweli au ni uongo uliozushwa), nadhani huu ni wakati muafaka kwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Mama Ummy Mwalimu kutafakari namna ya kuachia ngazi.

Sababu za kufanya hivyo ni hizi hapa.
1. Kukubali kwao kuwajibika moja kwa moja kwa hizo shutuma dhidi yao (ikiwa ni kweli) na kulinda hadhi ya serikali na hadhi ya Rais aliyewateua.

2. Kukaa pembeni ili kulinda heshima zao au kuonyesha kutokukubaliana na hiyo kauli ya mheshimiwa Rais (ikiwa shutuma hizo ni uongo).

3. Kupisha uchunguzi kamili na wahusika wengine wachukue nafasi zao ili nao wawajibike kwa namna tofauti (maana juhudi zao za mwanzo zimeonekana ni uchafu na upuuzi mtupu mbele ya yule aliyewateua)
Kwani wao ndiyo waliopima? Kazi yao ni kutangaza. Lazima kutofautisha kati ya data collectors/analyst na kuna disseminators.
 
Waziri Mkuu na waziri wa Afya wanapelekewa ripoti tu hata km una ujinga mwingi acha kujiaibisha
Kwa hiyo Uchunguzi wa Jiwe kautoa peke yake maabara au naye aliletewa?? Kumbuka wakati wa sakata la makinikia pia. Jiwe siyo wakumuamini hata kidogo labda kwa wenye akili kama zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom