Kichwamoto
JF-Expert Member
- Jan 21, 2019
- 3,403
- 4,692
Habari za leo wana JF
Naomba sana usome bila kuchoka tafadhari ni ombi.
Naomba tushirikiane kwa elimu,kukumbushana na umuhimu wa hadidu za rejea kwa wenye dhamana za mamlaka za uteuzi au wateule wenyewe, na pia umuhimu wa mamlaka za uteuzi kuainisha na kuzingatia vigezo msingi katika uteuzi.
Binafsi nimepata bahati ya kuona viongozi baadhi ndani ya serikali wakijikita katika visingizio vya kukosa pesa hasa uchache au kukosa pesa kama msingi wa kero ama changamoto kutotatuliwa. Na wakati mwingine upungufu wa kibajeti unakuwa umetokana na jambo la akili tu, kikanuni tu au uwajibikaji au kiuweledi
Sambamba na hilo ukifuatilia majibu ya hao viongozi hayawi na chembe zenye kuonesha kwa namna gani kama watendaji wanapambana kutatua kero zisizo hitaji pesa katika utatuzi hasa kuiishi usimamizi, ufuatliaji, tathimini, ushirikishwaji na matumizi pomoni ya hazina ya rasilimali watu. Au utatuzi wa swala la kipesa kwa namna isiyo hitaji pesa (mfano usafi na uchafuzi wa mazingira) sheria kanuni na adhabu zake au elimu isiyokikomo na usimazi, utunuku wa vyeti vya pongezi.
Mfano taasisi kuajiri watu wenye sifa sahihi kwa mahitaji sahihi, kutumia fursa mfano kutimiza maombi ya kuajiri kutafakari aina ya watu unaopaswa kuwa nao, vifaa, ukubwa wa majukumu na huduma hitajiwa, mahitaji kulingana na wakati, usinamizi wa ukarabati, kujua bei za vitu sokoni (kitengo cha manunuzi), urasimu na kudhibiti wizi.
Mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu na yasiyo ndani ya uwezo wetu katika muktadha huo huo wa masuala ya kifedha na yasiyo ya kifedha mfano utekelezaji wa kiratiba wa mpango wa kifedha mfano matumizi, kuomba fedha kuainisha mahitaji, kuomba mrejesho kwa wakati sahihi, matumizi ya adhabu na maonyo, matumizi ya sheria kanuni na miongozo, kutoa elimu ya taratibu za kazi. Malezi kwa watumishi
Kuchota na kutumia mawazo ya wafanyakazi kama rutuba ya uongozi bora.
Kuwa na mfumo wa kumbukumbu za utekelezaji wa maazimio mbalimbali, mafunzo na uendelezaji wa watumishi kuongeza ujuzi na maarifa, utendaji haki na usawa etc.
Utatuzi wa kero kwa kuzingatia urahisi na uharaka wa mawasiliano, kutoa taarifa kwa wakati na utoaji wa haraka wa majibu, viongozi na ofisi zao kuwa wenye kufikika na kuweka wazi mwenye wazo lolote kuandika hata barua na imfikie boss mwenyewe etc.
Uitishwaji wa mikutano iliopo kikanuni na kisheria ya kusikiliza kero na kutatua kero au kutoa tumaini na faraja au kujenga mioyo stahimilivu subra na uzalendo, kujenga umoja na mshikamano.
Nawakaribisha sana sana tupeane madini ya kiongozi iwe faida kwa vizazi vyote na watu wa aina zote.
Kwa heshima na taadhima naomba kuwasilisha
Ndugu yenu Kichwamoto.