BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel ametoa muda wa miezi miwili kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kujitafakari kuhusu uwezo wao wa kusimamia ubora wa huduma za afya.
Amesema hayo kufuatia malalamiko ya mara kwa mara yanayotolewa na wananchi wanaopewa huduma katika hospitali hiyo.
Dk. Mollel ametoa maagizo hayo leo Aprili 4, 2022 katika kikao cha ndani kilichomshirikisha Mganga Mkuu wa Serikali na viongozi wote wa Hospitali za Taifa za Kanda, Mikoa na waganga wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Pia, Waziri Mollel ameutaka uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha unakuja na suluhu za kudumu za upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Chanzo: Global Publishers