Uongozi wa klabu ya Simba SC wamegoma kufanya kikao cha kocha na waandishi wa habari kisa bango lenye nembo ya GSM

Uongozi wa klabu ya Simba SC wamegoma kufanya kikao cha kocha na waandishi wa habari kisa bango lenye nembo ya GSM

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa kitengo cha habari kinachoongozwa na Ally Shantri ‘Chico’ wamegoma kufanya kikao cha kocha na waandishi wa habari kisa bango lenye nembo ya GSM.

Mkutano wa makocha kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Simba na Yanga ulikuwa unafanyika leo katika makao makuu ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF).

Kocha wa Yanga, Nassredine Nabi ndiye aliyeanza kuzungumza na alipomaliza msemaji wa TFF, Clifford Ndimbo aliwataka Simba waingie lakini waligoma.

Chico alisikika akisema ”toeni bango kwanza”.

Baada ya Simba kugoma kuingia Ndimbo aliwaruhusu wadhamini wakuu wa Ligi, NBC kuingia na kuzungumzia mchezo huo.

Ikumbukwe toka wiki iliyopita Simba waliandika barua ya kuomba ufafanuzi juu ya udhamini wa TFF na GSM walioingia na kutaka nembo ya kampuni hiyo kuwa sehemu ya jezi.

Mwanaspoti ambalo lilishuhudia magari mawili ya Simba yakiingia Harrier (Rabi Hume) na Mercedes Benz (Barbara Gonzalez, Chico na Pablo Franco) baada ya kugoma kuingia Rabi na Chico walitoka kisha wakaondoka kwa pamoja.

gsmpic.jpg
 
Safii. Na kesho wakilazimisha kuweka mabango uwanjani, Simba msiingize timu ili Yanga ipewe point 3 za bure.

Kususa kwa zamu. Yanga waliwahi kugomea mabadiliko ya kuanza kwa mechi, Leo wengine wanamgomea mfadhili wa Yanga na TFF

Kumbukeni Simba ndio inayochangamsha hii ligi yenu. Kama vipi ihamishieni Simba kule Champion League kwa kina Tambwe muone mvuto utavyohamia kule.
 
Mimi sitaki hata ku comment hapa maana unaweza kushambuliwa kuwa labda shabiki wa team fulani ila ki ukweli katika makuzi yangu nilikuwa mpenzi sana wa Simba ila siku hizi sina ushabiki wa hivyo zaidi ni Liverpool tu.

Katika hili nadhani kuna mtu anadhani mkubwa kuliko wazazi, mpira unaendeshwa kwa sheria na sheria lazima ziheshimiwe. Wako wanasheria wao ndio wanatakiwa watizame kama kuna sheria zimevunjwa watoe ushauri au tafsiri za sheria.

Maana inaondoa hata ile hali ya watu kuongelea mpira watu wako busy na mambo nje ya mpira wakati mpira wetu wenyewe bado una safari ndefu sana lakini tunajiona kama tuko level ya akina Chelsea sio huko.
 
Safii. Na kesho wakilazimisha kuweka mabango uwanjani, Simba msiingize timu ili Yanga ipewe point 3 za bure...
Mawazo ya jikoni mnaleta sebleni. Unashauri Simba isusie Mechi kwani ni mara ya Kwanza? Mbona iliwahi kuvunja rekodi Kwa kucheza kipindi kimoja ikafungwa 4 ikagoma kurudi? Nachukia siasa za kinafiki za hizi timu zenu za Kariakoo.
 
Mimi sitaki hata ku comment hapa maana unaweza kushambuliwa kuwa labda shabiki wa team fulani ila ki ukweli katika makuzi yangu nilikuwa mpenzi sana wa Simba ila siku hizi sina ushabiki wa hivyo zaidi ni Liverpool tu...
Utaonekana wewe ni Yanga.
 
Ifike kipindi tuache ushabiki na tuangalie maslahi ya timu na timu nyingine. Mimi ni mshabiki wa Simba lakini kwa hili siungi mkono. Tuangalie sheria zinasemaje kuhusu udhamini lakini pia maslahi ya timu yetu.

Pia tusijiangalie sisi kwa kuwa tuna udhamini, tuangalie pia vitimu vidogo visivyo na wadhamini na uwezo wa kulipa mishahara Kama Biashara United,Namungo nk. Mabifu ya wahindi/ waarabu tusiyavae.
 
Utaonekana wewe ni Yanga.
Najuwa hilo na matusi juu, kitu kimoja TFF hawakutakiwa hata kusign na Azam media hiyo ni kazi ya bodi ya league wala NBC. TFF sio kazi yao wao TFF mikataba ya team ya taifa ndio wao ila bodi ya league kazi yake kuendeshwa kama kampuni na wamiliki ni vilabu vya league kuu kwa kupiga kura.

Tuona huko EPL vilabu ndio vinapiga kura kwenye Premier league pamoja na upinzani wao kimpira ikija kwenye maslahi yao wanapiga kura kwa uzito ulio sawa bila kujali ukubwa wa team. TFF naamini waeleze nafasi yao katika hili na bodi ya league waeleze wajibu wao katika hili.
 
Mawazo ya jikoni mnaleta sebleni. Unashauri Simba isusie Mechi kwani ni mara ya Kwanza? Mbona iliwahi kuvunja rekodi Kwa kucheza kipindi kimoja ikafungwa 4 ikagoma kurudi? Nachukia siasa za kinafiki za hizi timu zenu za Kariakoo.
Una kumbukumbu ndogo sana. Punguza kula ugali wa sembe na matembele....
 
Ifike kipindi tuache ushabiki na tuangalie maslahi ya timu na timu nyingine. Mi ni mshabiki wa Simba lakini kwa hili siungi mkono. Tuangalie sheria zinasemaje kuhusu udhamini lakini pia maslahi ya timu yetu. Pia tusijiangalie sisi kwa kuwa tuna udhamini,tuangalie pia vitimu vidogo visivyo na wadhamini na uwezo wa kulipa mishahara Kama Biashara United,Namungo nk. Mabifu ya wahindi/ waarabu tusiyavae.
Unasemaa huungi mkono halafu unapendekeza tuangalie sheria zinasemaje. Umetumia sheria gani kutounga mkono?

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom