Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,255
- 1,565
Yawezekana Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, uongozi wake ukawa ndio uongozi ambao umetoa mwanya kwa kila kiongozi wa ngazi yoyote ile kuonyesha uwezo wake, kipawa chake, ubunifu wake, umahiri wake na hata busara za kuamua mambo kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.
Yawezekana awamu zilizopita kwa namna na staili walivyokuwa viongozi wengine walifanya maamuzi kwa maelekezo mengi, waliogopa kufanya maamuzi kwa kuhofia kuwa je aliyeniteua atapenda au hapana, kwa namna moja yawekana iliwanyima kuonyesha uwezo wao halisi au wengine walionekana viongozi shupavu kwa kubebwa na aliye juu yake.
Rais wa awamu ya Sita ametoa nafasi kwa Watanzania kuona ni viongozi wapi Wapi warefu ambao wanaweza kuona mbali na sio kesho tu, kama kuna kiongozi ni mfupi kwa maana ameshindwa kuona mbali basi huyo ni uwezo wake umeishia hapo na Watanzania tutampima kwa hilo.
Kwa namna Rais wa awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyotekeleza kuiendeleza Tanzania, uchaguzi waz 2025 ukawa mgumu kwa baadhi ya viongozi wa fupi kwa kuwa Watanzania sasa wanawaona.
Rais wa awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameifungua Tanzania, Hongera kwa Mawaziri wengi wameonyesha kuwa ni viongozi Warefu kwa namna wanavyoenda na mdundo, Hongera Waziri wa Maliasili na Utalii - Mohhamed Mchengerwa kasi yako na timu yako yote kwa muda mfupi umeonyesha kuwa ni kiongozi mrefu, Hongera Gwajima - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum umekuwa unaitika kwa haraka kwenye shida za Watanzia, wapo Viongozi wengi saaana ni Warefu na Mungu awabariki kuendelea kuwatumikia Watanzania.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.