GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Siyo kwamba kila Siku GENTAMYCINE nikiwa Nawachokoza, Nawananga na Nawatania mno Watani zetu Yanga SC basi Kwetu huku ( Simba SC ) mkikosea nitawanyamazia.
Huwa sina Unafiki na Upumbavu na ndivyo hata nilivyo Kiuhalisia wangu.
Kama Kipa Ally Salim ( japo ana Mapungufu kadhaa ) ameweza Kudaka Mechi Kubwa Tatu ( ikiwemo ile dhidi ya Watani zetu Yanga SC ) na zile Mbili za Kimataifa kwanini tu Kipindi hiki ambacho Kipa Aishi Manula anaumwa asingeaminiwa moja kwa moja huku Yule Ferouz Kipa aliyepandishwa kutoka Simba B akiendelea Kupikwa na Kuimarishwa kwa baadae?
GENTAMIYCINE niliwasihi mno hapa na hata kwa baadhi yenu Viongozi kuwa msimuache Kipa Beno Kakolanya kwani bado alikuwa anatufaa, ni mzuri, kaimarika na angetufaa sana Golini mkanipuuza na Kumuacha mazima.
GENTAMYCINE najua kuwa huyu Kipa Mzungu alipokuja Dar es Salaam Wiki Mbili zilizopita mlimkataa kwakuwa alikuwa hajui Lugha ya Kiingereza au Kifaransa na Kumruhusu arejee Kwao ila mlipomsajili Jose Luis Miquissone Majuzi ( ambaye anaongea Kireno Lugha ambayo inazungumzwa zaidi buko Brazil ) ndipo mkaona mumsajili haraka Kipa Mbrazili Jefferson Luis kwakuwa tayari Mkalimani wake Mr. Bench Always Kapatikana.
Tusifichane Simba SC kweli nakiri Safari hii tumejitahidi Kusajili ila kwa Kipa wala tusipepese ukweli ni kwamba tumebahatisha tu na hakuna Kipa hapo.
Uongozi wa Simba SC mmetudharau na kama kututukana pia Tusi Kubwa Sisi Mashabiki wenu hivi Mtu mwenye Akili Timamu anaweza Kumsajili Kipa ambaye 90% ya Carrier yake katika Vilabu alivyocheza ilikuwa ni kwa Mkopo, Ligi atokayo ni Daraja la Nne sijui la Tatu halafu Kacheza Mechi 12 ila Kafungiwa Goli 17?
Halafu mwambieni huyu Kipa wetu Mpya aache Mkwara kwani nimemuona Jana akiwa Mazoezini akiwa na Mikwara mingi, akiruka huku na kule huku Mdomo wake ukiwa wazi na Usoni akijifanya yuko Serious ile mbaya.
Tumtahadharishe mapema kuwa bado mpiga Mawe wa Yanga SC Aziz K yuko na kule Azam FC kuna Wapiga Mawe Wawili Feitoto na Mwingine Mgeni ambaye nimedokezwa ukiona anajiandaa kutaka kupiga Shuti mwambie Kipa wako ( wa Timu yako ampishe tu ) kwani ana Mashuti makali ambayo Kipa yoyote akiwa na Kiherehere cha kutaka Kudaka kuna Mawili ama adake na aingie nao Golini liwe Goli au audake kisha akimbizwe haraka ICU Muhimbili National Hospital au akayaanze Maisha mapya Mochwari akisubiria tu Maziko yake huko Kijijini Kwao Kyaka Nkunde au Ikupilipa Nkoba.
Simba SC kwa Kipa tumekosea mno.