Hapo kwa Tadeo Lwanga ikitokea wamemwacha kama tetesi zinavyosema kuwa sababu kubwa ni majeruhi mara kwa mara kwa kweli uongozi itabidi wafanye "homework" haraka sana bila kuchelewa kumpata mbadala wake. Sio siri Simba ilihangaika muda mrefu sana kupata kiungo mkabaji ambaye anajua majukumu yake kiufasaha bila mafanikio. Kuna wakati alipita Majabvi toka Zimbabwe akaimudu hiyo nafasi lakini aliondoka baada ya muda mfupi. Kidogo akaja Kotei alijaribu kwa kiasi chake akaondoka. Akaja Fraga "akastruggle" sana mwanzoni lakini baadae ndie alikuja kucheza hiyo nafasi kwa ufahasa. Alipoondoka Fraga kutokana na majeruhi akaja Lwanga bahati nzuri naye ameitendea haki hiyo nafasi. Lwanga hata akiondoka leo nadhani mashabiki wa Simba hawatamdai chochote kutoka na kazi aliyoifanya na ikaonekana na kila mpenda mpira wa miguu nchini.
Uongozi usije ukafanya kosa la kiufundi kwenye usajili kwenye nafasi ya kiungo mkabaji kwani itawagharimu sana kama ambavyo eneo la ushambuliaji linavyowagharimu sasa hivi. Nikiwaangalia Mkude, Kanoute, Bwalya na Muzamiru sioni kiungo mkabaji kati yao ambaye ni mtu wa kufanya kazi chafu. Tangu ujio wa Fraga na baadae Lwanga kiukweli kabisa zile kelele kuwa Simba ina ukuta mbovu zilipungua sana kama sio kwisha kabisa kutokana na hao watu wawili kufanya kazi zao kwa weledi. Hata Wawa aliyekuwa analalamikiwa sana sasa hivi amebaki na kazi ya kuanzisha mashambulizi na anaonekana ni beki mzuri kutokana na uwepo wa kiungo mkabaji imara japo umri ndio kikwazo kikubwa kwake.
Kama kuna kuvunja benki mwaka huu basi itawabidi Simba wavunje benki ili kumpata mchezaji wa kimataifa atakeyeimudu hiyo nafasi ya kiungo mkabaji. Iwapo kulikuwa na ufuatiliaji wa maendeleo ya Fraga kwa upande wa uongozi ukajiridhisha kama anacheza mpira wa ushindani na kapona vizuri kwani ni mwaka sasa toka atoe taarifa kuwa amepona basi ni vyema wakamrudisha kwani kazi yake inafahamika na yeye anaijua Simba vizuri nje ndani. Na kwa wachezaji wa ndani kwangu binfsi naona ni wakati wa Simba kumrudisha Abdulswamad waliyemtoka kwa mkopo, naamini akipata muendelezo mzuri atakuwa msaada sana kwenye hiyo nafasi huko mbeleni kutokana na aina yake ya ukabaji wa kutumia nguvu.
Na ukitaka kujua kwa nini nafasi ya kiungo mkabaji kwenye timu ni muhimu na inahitajika apatikane mtu kweli kweli itazame Yanga ya mwaka huu chini Bangala. Kazi chafu anayoifanya Bangala pale kati kati imewafanya Mwamnyeto na Dickson Job kazi yao iwe rahisi kwa kiasi fulani lakini hata kipa wao hafikiwi kirahisi na timu pinzani kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Ni mtizamo wangu tu.