Uongozi wa Simba SC, niliwatahadharisheni mapema mno kuhusu hili hapa JamiiForums na leo ndiyo mnalifanya acheni Dharau sawa?

Uongozi wa Simba SC, niliwatahadharisheni mapema mno kuhusu hili hapa JamiiForums na leo ndiyo mnalifanya acheni Dharau sawa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
GENTAMYCINE zaidi ya mara Tatu (tena hapa hapa) JamiiForums na Threads zangu zipo niliwaonyeni (niliwatahadharisheni) kuwa mkikaribia Kucheza Mechi Kubwa za Kimataifa na Kitaifa msiwe mnajiandaa (mnafanya Mazoezi) katika Uwanja wetu wa Bunju wa Mo Arena kwa sababu za ndani nilizowapa ila mkanipuuza.

Na tena GENTAMYCINE nikaenda mbele zaidi hadi Kuwaibieni Siri kuwa Wachezaji wa Simba SC Wamefungwa Miguu yao na Kiutendaji (Kiufanisi) Kiushirikina na Waganga wa Kienyeji wa Timu Moja (Kubwa nayo) nchini ili ifanye vibaya Kimataifa na katika Mechi za Kitaifa ila mkanipuuza Malaika Mimi wa Kizanaki, Kimakuwa na Kitutsi.

Simba SC niliwaambieni kuwa mnapokuwa mnafanya Mazoezi Kujiandaa na Mechi Muhimu za Kimataifa na hata za Kitaifa msiwe mnafanyia pale Bunju Mo Arena (bali Kajificheni eneo lingine) kwakuwa kuna Watu Wabaya (Wachawi) huveshwa Jezi za Simba SC na kila Wakija Kuangalia Mazoezi ya Simba SC huokota Udongo na Nyasi kisha Kuupeleka kwa Fundi (Mganga) ambaye huwa Anawaroga Wachezaji wetu wa Simba SC wasiwe na Viwango vyao na Wachoke kabisa.

Hongereni Uongozi wa Simba SC (japo mmechelewa mno) kwa sasa Kuamua (kile nilichowatahadharisheni b) kuhama huo Uwanja wa Bunju Mo Arena na kwenda Kufanyia Mazoezi eneo lingine kwa kile mlichosema kuwa Wachezaji wa Simba SC (Timu ya Simba SC ) inarogwa vibaya.

Sasa Viongozi wa Simba SC kama tu Rais Samia ananisoma GENTAMYCINE Kutwa ( 24/7 ) hapa JamiiForums na mengine ninayosema hapa huyafanyia Kazi Kwanini nyie huwa hamnisikii kila Nikiwaonya wakati mnajua kuwa Naipenda sana Simba SC yangu?
 
Sina uhakika na mambo hayo ya ulozi, ila nakumbuka game na Coastal Union ya ASFC pale kwa Mkapa, wachezaji walikuwa wazito mnooo kama wanacheza huku wamebeba magunia. Nadhani hapo ni baada ya Robertinho kwenda kwao kwa muda.

Nakumbuka kucomment kuhusu hilo nikidhani uwanja ndiyo ulikuwa tatizo.
 
Back
Top Bottom