DOKEZO Uongozi wa UDOM unazuia matokeo ya mitihani kwa Wanafunzi ambao tumecheleweshewa malipo ya ada kutoka Bodi ya Mikopo

DOKEZO Uongozi wa UDOM unazuia matokeo ya mitihani kwa Wanafunzi ambao tumecheleweshewa malipo ya ada kutoka Bodi ya Mikopo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Usilipe ada direct. UDOM hawatarudisha hizo hela hasahasa hela ndogo .Kuna mshkaji wangu hakurudishiwa , aliishia kuzungushwa sana.
Wanafunzi wameandika barua za kurejeshewa pesa zao tangu July but chuo kipo kimya.

Wahasibu wanataka kuzipiga pesa za ada kutoka Bodi?
 
Kuna kitu kinaendelea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baadhi ya Wanafunzi wanaolipiwa hela na mkopo na Bodi ya Mikopo (HESLB) wamefungiwa matokeo yao na chuo kwa madai Bodi haijaingiza pesa za ada chuoni.

Hivyo, uongozi wa UDOM umewataarifu Wanafunzi kuwa walipie wenyewe ada direct na kama bodi wakiingiza pesa wataandika barua kuzirudisha hela.

Kushindwa kufanya hivyo basi tambua kuwa hutapata matokeo na kama ulifeli utadisco, maana muda wa kufanya ‘SUP’ utakuwa umeisha ambao ni mwezi mmoja baada ya matokeo.

Je, hii ni sawa? na kwanini Bodi ya Mikopo icheleweshe pesa? Hili ni kosa la nani? Na Kwa wale wasio na uwezo wa kulipa hiyo pesa haraka hivyo hatima yao ikoje?
Hivi vyuo ni noma,
Kwanza pole yenu. Halafu kuna wale wa YUDIZIM walilipa ada nyingi wakaambiwa mwezi wa saba watarudishiwa mpaka sasa wanasubiri manyoya
 
Ndio mkome kuchagua serikali ya wanafunzi vilaza

Kweli kabisa, UDOM na vyuo vingine washiriki siasa za mabadiliko. acheni woga. Vijana ndiyo catalysts chachu ya kudai mabadiliko huku wakijitokeza mbele kudai mabadiliko kwa maandamano, kupaza sauti na kushiriki moja kwa moja kuongeza mbinyo (pressure ) mabadiliko yapatikane sasa na wala siyo kesho au baadaye.

FIDEL CASTRO - "VIJANA ,HAKI HUDAIWA HUPEWI KWA HISANI"

Tanzania ipo katika right track kama vijana wote tutaunga mkono operasheni +255, Okoa Bandari Zetu, Haki, Uhuru wa Watu, Demokrasia na Maendeleo ya Watu.
1695130295838.png


Picha agosti 2023 mkutano mkubwa wa CHADEMA na wananchi wa Nyehunge Buchocha Sengerema Tanzania. @chademamediatv

Vijana tukiyaunga mkono madai na matamanio haya bila kutoa nafasi ya uvivu na uwoga kuendelea kutamalaki basi malengo haya ya mabadiliko hayatafifia yatakuwa endelevu bila kukoma na vijana wote kuendelea kujitokeza kwa wingi.

Vijana kujitokeza mstari wa mbele katika uwingi wao ndiyo itakuwa chachu ya kushawishi jamii yote kubwa kuwa nyuma yao idai mabadiliko, katiba mpya na haki za kisiasa pamoja na vile za kijamii kama kumiliki ardhi, kumiliki mashamba makubwa ya kisasa, kusafiri nje ya nchi kusaka maisha na uhuru wa kujumuika bila kusahau kuwakosoa viongozi .

KUTOKA MAKTABA:

VIJANA NA MABADILIKO


Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi

Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.

Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja kongwe, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k

Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.

Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhisha wananchi kama bandari kuchukuliwa kuwa vituo vya nchi ngeni, matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo zilizokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k

Huko Chile marekani ya kusini nchi iliyo viongozi wa vyama vya wanafunzi wenye kushiriki kikamilifu katika siasa pia maandamano imewezesha kiongozi kijana wa wanafunzi Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017

Gabriel Boric on the Chilean Student Movement:
59,554Views :2017 14 Jun
In a presentation at the School of Public Policy on June 7, 2017; Gabriel Boric offers a historical perspective and reflects on lessons learned. He focuses especially on the role of social movements in a well-developed democracy and provides insights on how to sustain collective action over an extended period of time. He speaks also about his transition from being a member of a political movement to being a member of Parliament. Gabriel Boric is a Chilean parliamentarian, and a former leader of the national student movement. He was the president of the Student Federation of the Universidad de Chile, one of the most important student unions in the country. Boric currently represents the Magallanes and Antarctic Region in Chile’s Chamber of Deputies. He was elected as an independent candidate and is not associated with either one of the two political coalitions that have traditionally dominated politics in Chile. Source:

Department of Public Policy at CEU​

Mwanafunzi wa chuo kikuu Tanzania toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa anaimani na matumaini potofu ya Ilani ya CCM imeandika ahadi ya mambo ya uongo ya kupata ajira, mazingira ruhani kuwa wataweza kupata vyeo vya ulaji vya kisiasa UVCCM, kuwa MNEC Halmashauri Kuu ya CCM, mbunge wa CCM n.k au kuwepo mazingira (hewa) ya kujiajiri.
1695130351439.png

Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.


Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric

gabriel boric presidente from time.com
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist
 
Mcheki kiongozi wa mapinduzi ya Cuba kamandate Fidel Castro hapa clip ikionesha kijana kiongozi wa nchi ya Cuba mwaka 1959 akiwa na umri wa miaka 33 akihojiwa kuhusu visheni ya uongozi mpya mwaka 1959

The young Prime Minister of Cuba comrade Fidel Castro rare interview conducted in English

On April 19, 1959, Fidel Castro appeared on “Meet the Press” for his first visit to the United States since the Cuban revolution, nearly three months earlier. When asked if he was a Communist, he said, “I am not a Communist.
 
CHADEMA INAWAITA VIJANA WOTE KUJA INGIA KATIKA SAFINA YA KUELEKEA UKOMBOZI

Freeman Aikaeli Mbowe safari yake ndefu ya kiuongozi yeye pamoja na vijana wa BAVICHA wakijenga kile Julius Nyerere alisema kuwa vijana lazima wajiamini kuingia na kugombea nafasi za juu kuongoza mabadiliko na pia kuwemo katika nafasi za juu za kufanya maamuzi
1695129966604.png


Freeman Aikaeli Mbowe ni mmoja wa waasisi muhimu wa Chadema tangu mwaka 1992 na ndiye alikuwa muasisi kijana zaidi kuliko wote walioanzisha chama hicho.

Baada ya kuasisiwa, alipewa jukumu la kuongoza kurugenzi ya vijana kwa miaka kadhaa lakini pia akiwa mtu muhimu katika utekelezaji wa masuala ya michakato ya ujenzi wa chama na ushauri wa usimamizi wa fedha.

Baada ya kukitumikia chama chake kati ya mwaka 1992 – 2003, Freeman Mbowe alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Taifa mwaka 2004, na ameendelea kuongoza chama hicho kwa miaka zaidi ya 19 hadi sasa.
 
Pumbavu zenu, nyie Udom ndio mnajifanya micahwa ya CCM wacha wasiwape hayo matokeo kama mna visapu mdisco kabisa!!. Udom na hiyo bodi ya mikopo wote ni CCM kwahiyo ungepeleka malalamiko ofisi za ccm.
 
Kuna kitu kinaendelea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baadhi ya Wanafunzi wanaolipiwa hela na mkopo na Bodi ya Mikopo (HESLB) wamefungiwa matokeo yao na chuo kwa madai Bodi haijaingiza pesa za ada chuoni.

Hivyo, uongozi wa UDOM umewataarifu Wanafunzi kuwa walipie wenyewe ada direct na kama bodi wakiingiza pesa wataandika barua kuzirudisha hela.

Kushindwa kufanya hivyo basi tambua kuwa hutapata matokeo na kama ulifeli utadisco, maana muda wa kufanya ‘SUP’ utakuwa umeisha ambao ni mwezi mmoja baada ya matokeo.

Je, hii ni sawa? na kwanini Bodi ya Mikopo icheleweshe pesa? Hili ni kosa la nani? Na Kwa wale wasio na uwezo wa kulipa hiyo pesa haraka hivyo hatima yao ikoje?

Kuna vitu vingine wala sio vyakutilia shaka au wasiwasi maana vitakuwa na suluhisho tu
 
Nimepigiwa sim juzi na mdogo wangu akinitaka ada ya scenario kama hiyo na Chuo iko iko Udom, sema yeye alikuwa mkweli kuwa hakusaini ada na basa kamuonesha kabisa zile sheet na anadai watu wengi tu hawajasaini tena kwa uzembe wao wenyewe, bodi wamesharejssha pesa hazina hivyo inatakiwa walipe ili wafunguliwe matokeo

Wewe mleta mada unakuja kuchafua reputation ya Chuo huku mtandaoni unashindwa kusema kuwa hukusaini ada....

Kuna taasisi brand yake ni kubwa sana kuchafua reputation zao kienyeji kama hivi ni uongo
 
Nimepigiwa sim juzi na mdogo wangu akinitaka ada ya scenario kama hiyo na Chuo iko iko Udom, sema yeye alikuwa mkweli kuwa hakusaini ada na basa kamuonesha kabisa zile sheet na anadai watu wengi tu hawajasaini tena kwa uzembe wao wenyewe, bodi wamesharejssha pesa hazina hivyo inatakiwa walipe ili wafunguliwe matokeo

Wewe mleta mada unakuja kuchafua reputation ya Chuo huku mtandaoni unashindwa kusema kuwa hukusaini ada....

Kuna taasisi brand yake ni kubwa sana kuchafua reputation zao kienyeji kama hivi ni uongo
Kama Bodi wameshaingiza pesa za ada kwanini wanafunzi wenye over payments zao hawajalipwa?
Huoni kama wahasibu wa hiko chuo wamekula pesa za hao wanafunzi?
 
Back
Top Bottom