Tatizo la bodi kuchelewasha pesa za ada lipo sana tu hasa kwa vyuo vya serikali
Lakini kwa ninavyo fahamu, chuo huwa kinaruhusu tu wanafunzi wafanye mitihani kama pesa imekuwa allocated tayari. Ndiyo utamaduni wa vyuo vingi vya serikali. Serikali ikileta, zitalipwa.
Japo viongozi wa hicho chuo wanaweza kuwa wazembe, sina shaka serikali ya wanafunzi hapo UDOM imejaa vilaza.
Kazi yao ni nini hasa??
Hili jambo lingetokea kipindi fulani tungeshuhudia kundi la wanafunzi wakiandama kutetea haki yao tena wakiongozwa na viongozi wa serikali ya wanafunzi. Hawa viongozi wa siku hizi wapo tu kuitukuza serikali. Waoga kupindukia. Wala hawajali matatizo ya wanafunzi wenzao.
Poleni.