Ndio mkome kuchagua serikali ya wanafunzi vilaza
Kweli kabisa, UDOM na vyuo vingine washiriki siasa za mabadiliko. acheni woga. Vijana ndiyo catalysts chachu ya kudai mabadiliko huku wakijitokeza mbele kudai mabadiliko kwa maandamano, kupaza sauti na kushiriki moja kwa moja kuongeza mbinyo (pressure ) mabadiliko yapatikane sasa na wala siyo kesho au baadaye.
FIDEL CASTRO - "VIJANA ,HAKI HUDAIWA HUPEWI KWA HISANI"
Tanzania ipo katika right track kama vijana wote tutaunga mkono operasheni +255, Okoa Bandari Zetu, Haki, Uhuru wa Watu, Demokrasia na Maendeleo ya Watu.
Picha agosti 2023 mkutano mkubwa wa CHADEMA na wananchi wa Nyehunge Buchocha Sengerema Tanzania. @chademamediatv
Vijana tukiyaunga mkono madai na matamanio haya bila kutoa nafasi ya uvivu na uwoga kuendelea kutamalaki basi malengo haya ya mabadiliko hayatafifia yatakuwa endelevu bila kukoma na vijana wote kuendelea kujitokeza kwa wingi.
Vijana kujitokeza mstari wa mbele katika uwingi wao ndiyo itakuwa chachu ya kushawishi jamii yote kubwa kuwa nyuma yao idai mabadiliko, katiba mpya na haki za kisiasa pamoja na vile za kijamii kama kumiliki ardhi, kumiliki mashamba makubwa ya kisasa, kusafiri nje ya nchi kusaka maisha na uhuru wa kujumuika bila kusahau kuwakosoa viongozi .
KUTOKA MAKTABA:
VIJANA NA MABADILIKO
Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi
Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.
Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja kongwe, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k
Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.
Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhisha wananchi kama bandari kuchukuliwa kuwa vituo vya nchi ngeni, matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo zilizokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k
Huko Chile marekani ya kusini nchi iliyo viongozi wa vyama vya wanafunzi wenye kushiriki kikamilifu katika siasa pia maandamano imewezesha kiongozi kijana wa wanafunzi Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.
Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017
Gabriel Boric on the Chilean Student Movement:
59,554Views :2017 14 Jun
In a presentation at the School of Public Policy on June 7, 2017; Gabriel Boric offers a historical perspective and reflects on lessons learned. He focuses especially on the role of social movements in a well-developed democracy and provides insights on how to sustain collective action over an extended period of time. He speaks also about his transition from being a member of a political movement to being a member of Parliament. Gabriel Boric is a Chilean parliamentarian, and a former leader of the national student movement. He was the president of the Student Federation of the Universidad de Chile, one of the most important student unions in the country. Boric currently represents the Magallanes and Antarctic Region in Chile’s Chamber of Deputies. He was elected as an independent candidate and is not associated with either one of the two political coalitions that have traditionally dominated politics in Chile. Source:
Department of Public Policy at CEU
Mwanafunzi wa chuo kikuu Tanzania toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa anaimani na matumaini potofu ya Ilani ya CCM imeandika ahadi ya mambo ya uongo ya kupata ajira, mazingira ruhani kuwa wataweza kupata vyeo vya ulaji vya kisiasa UVCCM, kuwa MNEC Halmashauri Kuu ya CCM, mbunge wa CCM n.k au kuwepo mazingira (hewa) ya kujiajiri.
Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.
time.com › collection › gabriel-boric
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist