Uongozi wa Yanga ujitafakari

Uongozi wa Yanga ujitafakari

Aliyekuwa Mchezaji wa Yanga Hafiz Konkoni ameshinda kesi yake ya madai dhidi ya Klabu hiyo (Yanga) akidai fidia yake baada ya kuvunjiwa mkataba, Yanga wamepokea barua ya maamuzi ya kesi hiyo kutoka FIFA Jana Oktoba 17, 2024.

Hii inakuja siku chache baada ya Mchezaji mwingine Augustine Okrah kushinda kesi kama hiyo dhidi ya Yanga.
Dah Yanga inatia huruma.
 
Ukitaka kitu kizuri lazima uingie gharama, fikiria kama leo timu ingekua na strier Konkoni ingefika wapi?
Kuachana na mchezaji asiye na umuhimu kwenye timu na kisha kuleta mchezaji mzuri siyo tatizo .Tena kwa hilo nawapongeza Yanga . Tatizo ni kutowalipa hao wachezaji kwa wakati hadi wanafikia hatua ya kwenda FIFA hali inayoharibu taswira ya timu
 
Shangilienir
Walipe pesa za watu halafu mambo ya kujitafakari yafuate

Kuachana na mchezaji asiye na umuhimu kwenye timu na kisha kuleta mchezaji mzuri siyo tatizo .Tena kwa hilo nawapongeza Yanga . Tatizo ni kutowalipa hao wachezaji kwa wakati hadi wanafikia hatua ya kwenda FIFA hali inayoharibu taswira ya timu
Kama hapo ulipo haudaiwi nyoosha mkono
 
5imba wamepata kichaka kingine cha kujifurahisha. Mwanasheria wa Yanga.


YANGA BINGWA!
 
Dili za watu hizo mkuu, ndiyo mbinu watu wanakula hela za timu,wanaipigisha shot,then timu inapaswa kulipa,Hapo Hafiz atakula percent yake na baadhi ya viongozi wanakula chao......yale yale hata Okra.....

Usione watu wanakula maisha mjini hapa,hela ndiyo hizo wanakula na wachezaji
 
Hii sasa ni kuifedhehesha nchi yetu aisee

Halijapoa la Okra, limeibuka la Konkon

Ndani ya miezi michache tu barua kutoka FIFA zimeleta madai ya
1. Gael Bigirimana
2. Luc Aeymael (aliyekuwa Kocha wa Yanga)
3. Lazarus Kambole
4. Okra
5. Hafiz Konkon
6. Barua nyingine ilikuja mwezi APRIL baada ya Yanga kushindwa kukamilisha mchakato wa usajili kwa njia ya mfumo

Uongozi wa Hersi ujitafakari juu ya hili, kwann iwe Yanga tu kila mara ilhali usajili wa wachezaji unafanywa pía na majirani zetu kina Simba na Azam na wala Husikii hizi barua za kufungiwa fungíwa kila mara

Au kuna 10% kwenye hizi ishu (inside job), mchezo ukiundwa kati ya baadhi ya viongozi wa Yanga na players kwamba tutakuvunjia mkataba alafu wewe kimbilia FIFA, kisha leta barua ya madai na zuio tukikulipa tu hakikisha unanimegea changu pembeni
 
Back
Top Bottom