kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Team working (kufanyakazi kwa pamoja) hakumaanishi kusogeleana sana kimwili kati ya viongozi na watumishi wake, bali ni kiongozi kufanya na kuwepo pale unapohitajika kuwepo kwa wakati na wale wanaokuhitaji na kufanya Yale unayopaswa kufanya kwenye taasisi kwa wakati.
Viongozi wa Yanga walikuwa wakiimba, kucheza, kunywa na kula na kocha Gamondi. Kuna wakati kiongozi alikuwa anambeba na kumsifia mno Gamondi. Hii ilisababisha kocha kufanya kazi kwa mazoea badala ya malengo ya club.
Viongozi wakuu walikuwa karibu mno na kocha na wachezaji kiasi cha kupoteza hofu ya kazi kwa kocha na wachezaji na kocha alikuwa karibu mno na wachezaji wake kiasi cha kupoteza hofu ya kazi kati ya wachezaji na kocha wao.
Hofu ya kazi ikipotea inashusha ufanisi katika kazi. Yaani mfano, kama mhudumu wa vinywaji atakuwa karibu sana na supervisor hata wateja hawatapata huduma iliyotukuka.
Viongozi wakuu acheni kusogelea sana makocha na wachezaji wenu. Nyie jikiteni zaidi katika kutimiza majukumu yenu TU ili Kila mtu ajihisi Yuko kazini na ni sehemu ya timu. Kiongozi mkuu anaposifia wachezaji hawa hadharani na kuwaacha wale inashusha morali kambini. Kama Kuna Aziz Ki day lakini hakuna Kibwana day unategemea nini? Bacca day bila Mzize day ni upuuzi sawa na upuuzi mwingine TU.