Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

ACHENI acheni ACHENI mnasomwa hapa nyie nyie nyie. Laleni asubui muhamke
 
Basi jua alianzia TISS huwezi kwenda kuwa spy TISS jaribu kuficha ujinga na kupunguza pipipili kwenye chai.
Hahahaa we jamaa umenifanya nicheke kwa sauti..
Nadhani ujui sheria za kijeshi au za kujiunga na army laiti unge jua usinge andika huo upupu wako.
Ukimuona mwanajeshi yupo anapiga kazi TISS sio kwamba ameenda kupeleleza mambo ya huko, yupo kwa ajili ya tasks flani acha kuwa kichwa box.
Nadhani hujui ndani ya military ina vyuo vikumbwa vya intelligence na vinafundisha usalama wa ndani na nje kuliko hata vyuo vya TISS.
Na hata siku moja uwezi kuta eti usalama wa jeshi yupo anafanya kazi polisi eti kama undercover kuchunguza polisi wanafanyaje kazi au yupo kule TISS anachunguza wanafanyaje kazi,
Sasa wewe uli skia wapi kuna TISS yupo kama undercover ndani ya jeshi ana peleleza mambo ya jeshi huyo si atakuwa kama jasusi na sheria za jeshi lolote adhabu ni kupigwa risasi mpaka kufa.
 
mengine hayawezi kuandikwa hapa yote, ila ujue kuna watu ni wanajeshi wako kwenye majeshi ya nchi nyingine huko kwa watu.
wamefanya usaili na wanapiga kozi basic mpaka wanafanikiwa kupanda ranks za juu kabisa, lakinina huku kwao wana vyeo kijeshi tena.

maofisa wa usalama wanafanya upelelezi wa mashaka yote yanayohatarisha usalama wa taifa kwa ujumla wake, ndio hapo muingiliano na kitengo cha jeshi(MI) huzaliwa.

lakini si kweli kwamba wa role kubwa kabisa kwenye mfumo wa wa utendaji wa jeshi, hapana.
Labda wewe atakuelewa
 
Linaweza kuwa swali lisiloeleweka haraka, Labda nianze na simulizi kwanza

Mwaka 1979 Tanzania iliingia kwenye vita na Uganda maarufu kama vita ya KAGERA. Mwaka 1995 nilikutana na mzee Mkumbi(marehemu) mmoja wa watu ambao walikaribia kabisa kupigana vita hiyo. Miongoni mwa mambo aliyonisimulia ni kuwa yeye alirudia eneo la mwisho ambalo angetoka hapo ilikuwa ni moja kwa moja anaingia uwanja wa vita. Anasema alifurahi sana kwani akiwa kwenye eneo la mwisho ambalo daktari alikuwa anawapima afya ndipo alinusurika, kilichomnusuru ni kukutana na daktari ambaye alikuwa ndugu yake, akamuokoa kwa kueleza kuwa afya yake si mzuri.

Binafsi ingawa sikusema nilimshangaa sana huyu mzee kwa sababu alichokifurahia ni kukwepa majukumu yake ya msingi kama Mwanajeshi, hata huyo daktari kwangu bado hakuwa Mzalendo alitaka mtoto wa nani afe na wa nani abaki? Na hawa ndio wale ambao ni wengi wanaajiriwa kwenye majeshi yetu kwa njia za upendeleo lakini je tumeangalia nini athari yake?

Kuna hii idara maarufu ambayo wengi wanatamani kuajiriwa ambayo ni usalama wa Taifa, Licha ya mshahara na marupurupu yake upande wa pili wa idara hii ukoje(side effect yake ni ipi?) Kuna jamaa waliibuka kwa ahadi za kuajiri watu kwenye Idara hiyo ambapo walikuwa wanahongwa Mil 1 na kuendelea ili kuwapatia watu kazi kwenye Idara hiyo, Hivi ni kweli watu wanaoingia kwa mtindo huo watayaweza hayo majukumu? Au kazi yenyewe ni ile ya kupita kurekodi tu watu wanaomkosoa Rais kwenye vijiwe vya kahawa? Hakuna majukumu ambayo yanamtaka mtu kujitoa ambayo yanaweza kumfanya mtu akwepe kutimiza wajibu wake kama yule mzee aliyekwepa kwenda kupambana Uganda?

NAULIZA TU.
Umetumia VPN gani Kufungua Huu Uzi?
 
Umetumia VPN gani Kufungua Huu Uzi?
Ni uzi wa kizalendo tu huu, hauna shida hatuzungumzii Korona tunazungumzia mambo ambayo hata baadhi ya wanaojibu wanatia chumvi tu kwa mboga wasioijua
 
Tungetambua ni kiasi gani hao watu wa TISS wanavyotoil kuhakikisha taifa liko salama, tungefunga na kuwaombea mema kila siku

Hii amani tunayoiona hapa kwetu huku majirani zetu Congo, Burundi na Kenya wakichinjana haipo tu kwa bahati mbaya. Kuna watu wanavuja jasho na damu kuilinda!
TISS wabeba lawama ila jamaa wanapiga kazi nzito sana.

Yaani ktk security layer hawa jamaa ndio layer ya kwanza,kazi yao ni ku-detect hali ya hatari kabla haija lifikia taifa,sio kazi ndogo na ndio maana mda wote wapo macho.
 
Kama hujui majukumu ya TPDF ni bora ukae kimya kuliko kuwadanganya wasomaji, TPDF ina majukumu mengi sana kuliko unavyofikilia kwenye ubongo wako, katika idadi ya vyombo vya ulinzi na usalama tulivyo navyo TPDF ni chombo cha juuu,
TPDF ni takataka mbele ya TISS huwezi mlinganisha afisa na askari wa JWTZ hata huko TPDF wamejaa wanausalama kwa ufupi TISS ni kama damu katika mwili wa binadamu hata TPDF inategemea uwepo wa TISS kuwa hapo ilipo.
 
Kuna mmoja babake mkubwa aliwahi kuwa mkuu wa kitengo pale kijitonyama alivyotoka masomoni babake akampenyeza sehemu pale mjini kwenye kishirika cha serikali jamaa kila siku yeye ni kuchange magari na anatembea na bastora full mashauzi nowdays katupwa huko mbeya nimemkuta juzi na mark2 box kajichokeaaaaa.nikamkumbusha zile misele akaishia kusema wewe acha tuu. Ngosha alivyoingia kapandikiza watu wake ka kanda ya ziwa tu huko wengine tupa kule.
Wewe fala hujui kuficha hata code jamaa yako umemvua nguo zote mchana kweupe 😡😡
 
Zamani nilipokuwa nasikia TISS nilikuwa nafaa kusisimkwa, nikipata fantasy za kina Willy Gamba....baada ya kuwajua baadhi ya watu niliosoma nao na uwezo wao wa kiakili. Nilikuja jua ni upuuzi mtupu. Hata issue ya mishahara hamna lolote la maana. Wanalia njaa tu. Bora kuwa mjeshi mwenye cheo
 
Zamani nilipokuwa nasikia TISS nilikuwa nafaa kusisimkwa, nikipata fantasy za kina Willy Gamba....baada ya kuwajua baadhi ya watu niliosoma nao na uwezo wao wa kiakili. Nilikuja jua ni upuuzi mtupu. Hata issue ya mishahara hamna lolote la maana. Wanalia njaa tu. Bora kuwa mjeshi mwenye cheo
Wale ukiwatoa vibunduki vyao hawana la maana
 
Lakini mara nyingine TISS haiwezi kushughulikia maadui wa taifa bila kuwahusisha TPDF @ JWTZ,
Kuna matukio mengi ya kihatari ambayo yanakuwa militaristic sana na TISS hawawezi kuyamaliza wenyewe. Inahitaji ukusanywaji wa taarifa na mikakati ya kijeshi ili kuweza kukamilisha kazi kwa ufanisi wa hali ya juu sana.

Kikubwa zaidi ni kwamba TISS ina mkono mrefu sana kuliko TPDF @ JWTZ,
Kwasababu ni CIVILIAN INTELLIGENCE na inahusika na raia kwa moja kwa moja.
TPDF @ JWTZ Jurisdiction yao iko very limited kwasababu wao ni Purely Military tofauti kabisa na TISS.

Japo sasa,
Majasusi wengi wa TISS ambao ni heavy duty wanatokea JWTZ.
Kwasababu mfano tu, mwanajeshi Special Forces (Marine) anakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi za kijasusi wa kijeshi kama Reconnaissance, Kutegua mabomu, kuchambua na kutafsiri mikakati ya kijeshi ya nchi za adui kuliko jasusi ambaye yuko uraini kila siku . Kikubwa ambacho jasusi wa TISS atamshinda huyu Jasusi aliyetoka jeshi ni "Broad Mind" kwasababu mwisho wa siku kila taarifa za kijasusi ziwe za Kijeshi au Kiraia (Raw Intelligence) ni lazima ichakatwe (Processed) kwa ajili ya matumizi ya Kiutawala(Civilian Administrative Purposes). Wanaochakata ni Analysts ambao ni Think Tanks kutokea TISS kwasababu wanakuwa na mtazamo wa kiraia... ..Hili ndilo linawafanya TISS wawe hatua kumi mbele ya JWTZ @ TPDF kama taasisi.

NB 1: TISS wanafanya kazi bampa tu bampa na JWTZ kwasababu Its the duty of the TISS to make sure the army behaves and remains royal to the government and the state at by and large......!!!! Hivyo contractors wengine wa TISS wanakuwa ni wanajeshi katika asilimia 100% na maisha yao yote ni kwenye Barracks za kule Lugalo au Ngerengere.

Tuseme ukweli,
TISS na JWTZ ni mapacha wasiofanana (Fraternal Twins)
Hakuna anayeweza kufanya kazi bila kumtegemea mwenzake.
TISS IMARA=JWTZ IMARA..........

NB 2: Tusisahau pia kwamba JWTZ nao wana kitengo chao cha Intelijensia.
MILITARY INTELLIGENCE nacho kinafanya kazi na oparesheni kubwa sana za kijeshi.
Kazi yake ni kushughulikia maadui wa taifa covertly/clandestinely ambao ni purely Militaristic of Para-Militaristic in nature........
Mtawala halisi wa dunia nchi yoyote ile ni jeshi. Mkuu wa jeshi akiwaambia vijana wake waingie mtaani na vifaru kila mtu anafyata...mifano mingi, Al Asis, Zimbabwe na sasaiv Maynamar. Wengine mbwembwe tu..Aungurumapo Simba mcheza nani
 
Zamani nilipokuwa nasikia TISS nilikuwa nafaa kusisimkwa, nikipata fantasy za kina Willy Gamba....baada ya kuwajua baadhi ya watu niliosoma nao na uwezo wao wa kiakili. Nilikuja jua ni upuuzi mtupu. Hata issue ya mishahara hamna lolote la maana. Wanalia njaa tu. Bora kuwa mjeshi mwenye cheo
unatala kusema hata salary zao ziko kawaida tu? sio kubwa kama zinavyodhaniwa?
 
TPDF ni takataka mbele ya TISS huwezi mlinganisha afisa na askari wa JWTZ hata huko TPDF wamejaa wanausalama kwa ufupi TISS ni kama damu katika mwili wa binadamu hata TPDF inategemea uwepo wa TISS kuwa hapo ilipo.
hapa nitakupinga. JWTZ wana resources nyingi, na rasilimali watu wengi kuliko TISS.
and JWTZ sio brainless foot soldiers,kuna vitengo ndani yake, moja yao ni MI. officialy wana detachment yao maalum but sitoiweka hapa kwa sasa.
yes TISS mara kadhaa wanafanya recruitment toka jeshini, but it doesnt mean kwa JWTZ hawajui, or they know.
MI wanafanya kazi karibu na TISS.nila sio kwamba ni TISS.
hizi ni taasisi mbili zenye kazi tofauti. na kila mmoja ana umuhimu wake.
 
Back
Top Bottom