Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

Huwezi kuiba pesa ya serikali/umma bila hao wajomba kuwaonjesha mkuu tofauti yake ni kuumbuliwa dk 0 kwa hiyo wapo na wanaona, tusiwalaumu kwa yaliyojuu ya uwezo wao
TATIZO kubwa ni mfumo, kumbuka hata hao tiss hawakujiunda bali, taasisi yao nayo iliundwa, kiongozi wao mkubwa ni mteuliwa wa mwanasiasa mkubwa, nguvu ni mamlaka na mamlaka unapewa na mtu, akiyaondoa una Baki kama ulivyozaliwa SI lolote SI chochote. Nchi yangu Tanzania Kuna mambo makubwa tunatakiwa kubadilika lkn hatuwezi kubadilika kwa urahisi kwa kuwa yeyote anayefikia levo hizo ni faida sana kwake hivyo hawezi kukubali kubadili kitu labda vidogo vidogo.
SI raisi, mkuu wa majeshi, igp, mkurugenzi wa usalama wa taifa jaji mkuu, katibu wa bunge, mawaziri, au mkuu yeyote wa idara anapaswa kulaumiwa kwa rushwa, ufisadi,wizi au UOVU wowote katika taifa hili Bali WA KULAUMIWA NI SISI WANANCHI. KWA UOGA NA UPUMBAVU WETU. ACHENI WANAOPATA FURSA WAPIGE MAISHA NDIO MFUMO ULIVYO.
Hao wakubwa wote wa hizo taasisi kubwa nilizozitaja wanateuliwa na wanaondolewa MDA wowote wakienda kinyume na aliyewateua na Hilo wanalijua, kudumu kwao au kulinda kibarua Chao ni kucheza Ngoma na stepu anazocheza mteuaji.
Tuna ona UOVU tunapokuwa nje ya system lkn ukiwa ndani ya mfumo unaokubeba utafurahia tu.
Nina mengi lkn niishie hapo
 
Hili ndilo neno maana form four failures ndiyo wanaolinda maslahi ya nchi...

Ugumu ni kwamba..
Hao form four failures ndiyo wamejaa jeshini,polisi na kwenye vitengo vinavyotumia silaha kwahiyo mapinduzi ni ngumu kiasi
Hao fomu foo felia walifeli Masomo darasani lkn hawakufeli mafunzo ya kijeshi bwana hebu acha dharau, hata wewe unaweza kufaulu history kwa alama A lkn ukafeli mafunzo ya mgambo. Hapa TATIZO ni mfumo wetu ndio uliofeli, na wakulaumiwa ni sisi WANANCHI ambao hatukui hatua
 
Hao fomu foo felia walifeli Masomo darasani lkn hawakufeli mafunzo ya kijeshi bwana hebu acha dharau, hata wewe unaweza kufaulu history kwa alama A lkn ukafeli mafunzo ya mgambo. Hapa TATIZO ni mfumo wetu ndio uliofeli, na wakulaumiwa ni sisi WANANCHI ambao hatukui hatua
Kwamba hao waliofeli elimu upande wa darasani wakijifunza mbinu za kumlinda raia na mali zake watafaulu...🤔🤔😄😄😄😄.

Kumbuka aliyeleta elimu ya darasani ndiye aliyetuletea elimu na mbinu za jeshini na zote ni written na practical..
 
Kwamba hao waliofeli elimu upande wa darasani wakijifunza mbinu za kumlinda raia na mali zake watafaulu...🤔🤔😄😄😄😄.

Kumbuka aliyeleta elimu ya darasani ndiye aliyetuletea elimu na mbinu za jeshini na zote ni written na practical..
Akiweza kupita tu form 2 atapita popote pale
 
Linaweza kuwa swali lisiloeleweka haraka, Labda nianze na simulizi kwanza

Mwaka 1979 Tanzania iliingia kwenye vita na Uganda maarufu kama vita ya KAGERA. Mwaka 1995 nilikutana na mzee Mkumbi(marehemu) mmoja wa watu ambao walikaribia kabisa kupigana vita hiyo. Miongoni mwa mambo aliyonisimulia ni kuwa yeye alirudia eneo la mwisho ambalo angetoka hapo ilikuwa ni moja kwa moja anaingia uwanja wa vita. Anasema alifurahi sana kwani akiwa kwenye eneo la mwisho ambalo daktari alikuwa anawapima afya ndipo alinusurika, kilichomnusuru ni kukutana na daktari ambaye alikuwa ndugu yake, akamuokoa kwa kueleza kuwa afya yake si mzuri.

Binafsi ingawa sikusema nilimshangaa sana huyu mzee kwa sababu alichokifurahia ni kukwepa majukumu yake ya msingi kama Mwanajeshi, hata huyo daktari kwangu bado hakuwa Mzalendo alitaka mtoto wa nani afe na wa nani abaki? Na hawa ndio wale ambao ni wengi wanaajiriwa kwenye majeshi yetu kwa njia za upendeleo lakini je tumeangalia nini athari yake?

Kuna hii idara maarufu ambayo wengi wanatamani kuajiriwa ambayo ni usalama wa Taifa, Licha ya mshahara na marupurupu yake upande wa pili wa idara hii ukoje(side effect yake ni ipi?) Kuna jamaa waliibuka kwa ahadi za kuajiri watu kwenye Idara hiyo ambapo walikuwa wanahongwa Mil 1 na kuendelea ili kuwapatia watu kazi kwenye Idara hiyo, Hivi ni kweli watu wanaoingia kwa mtindo huo watayaweza hayo majukumu? Au kazi yenyewe ni ile ya kupita kurekodi tu watu wanaomkosoa Rais kwenye vijiwe vya kahawa? Hakuna majukumu ambayo yanamtaka mtu kujitoa ambayo yanaweza kumfanya mtu akwepe kutimiza wajibu wake kama yule mzee aliyekwepa kwenda kupambana Uganda?

NAULIZA TU.
🤔
 
Tiss inaelezwa wapo kila idara kila sekta kila mahali kila wizara but still upigaji upo pale pale reporte ya CAG huwa ina toa upigaji kwenye hizo wizara halmashauri na idara nyinginezo nyingi nawapigaji wanajulikana .hapo ndipo utakapojua kuwa kuku ya bwana juma imeliwa na mbwa wa bwana juma . Ila wakiamua wao kuikomboa nch kiumchumi kisiasa kijamii na nk wanaweza coz kila kitu kipo mikononi mwao———— but unaambiwa wapo everywhere
 
Back
Top Bottom