Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

huku kwetu polisi!!!mimi sio polisi mkuu.

unaposema naandika tu,sijajua unakuwa umetumia rejea gani??kwani si kila mtu anaandika tu humu chochote,na watu wanasoma wanafurahi,ila nyuma ya pazia ni ukuta mnene kwa jf au vijiweni.
Kwanini mnakataa kazi zinazowaweka mjini???Punguza ujuaji
 
Upande wa pili wa usalama wa taifa ndyo mdudu gain?
 
Unachosema ni dhahiri mkuu.Kuna baadhi ya watu katika idara nyeti za umma wanapenda kushare baadhi ya vitu vya maofisini as a way to release their grievancies lakini ni busara ya kawaida kuhakikisha haujadili kitu ambacho ni siri ya ofisi/wewe binafsi.Kukaa kimya kwa masuala nyeti ya nchi hasa ya usalama ni UZALENDO pia.So guys tuwe makini

Ukiwa na akili nyingi huwezi kuwa mtumishi wa umma
 
Kuwa polisi,mwanajeshi au afisa wa jeshi hapa nchini ni ujanja na mafanikio, wengi wetu tunachukulia kama ni sehemu ya kazi tu kama zilivyo kazi nyingine. Tunaitaji kupata mshahara kwa wakati na faida kibao ikiwemo heshima mtaani na sio uzarendo kazini katika kulitumikia vyema taifa.
Lakini aina hii ya wanataasisi husika wasiotekeleza majukumu yao vyema ni mavuno ya mazao yaliopandwa na serikali yenyewe. Hapa nikimaanisha unakuta katika kuchagua watu husika wakufanya kazi katika kitengo fulani muhimu ndani ya taifa, watu waliopaswa kusimamia vyema kazi hiyo wanachanganya na maamuzi yao binafsi ikiwa ni kuingiza vitendo vya rushwa ndani yake, kuweka nafasi za upendeleo na undugu huku wakiwaacha Watanzania wengi wenye sifa hizo husika mitaani na kulibebesha taifa wataalamu na watendaji kazi fake.
 
Sio Ishu ya Tetesi ndugu, ndivyo ilivyo kwa uhalisia wake; Kila Idara, Mfumo wa utendaji unapoanzishwa basi lazima jamaa wawekwe.
Hii ilianza zamani toka enzi za nyerere, Kila taasisi ilipoanzishwa aliangalia Mfumo mzuri wa kupenyeza watu wa Usalama ili kuhakikisha Taasisi, Idara au Mfumo husika unafanya kazi Bila kuleta wasiwasi kwenye usalama wa Taifa.

Wakati wa kuanzishwa Mfumo wa Vyama vingi, Nyerere aliigomea hii kitu kabisa (Alikuwa hataki mfumo wa vyama vingi), Lakini ishu ilikuwa atawezaje kuhakiksha usalama wa Taifa kwenye Vyama hivyo (ndani katika utendaje wake), Ilimchukua muda tangu azimio la vyama vingi kutakiwa mpaka jamaa aliporuhusu. Ndipo akaweka Utaratibu kuwa Ukitaka upate usajili wa kudumu basi chama cha siasa basi lazima kipate wanachama japo 200 angalau katika mikoa kumi. Sasa hapa ndipo inakuwaga ndio pale Usalama wa nchi Yetu unaingiza watu wake japo 5, na mara nyingi si watu wa kawaida unakuta ni watu walio very smart kwenye uwezo wa kupambanua mambo, wana mtazamo chanya kabisa kabisa juu ya hicho chama, wanajenga hoja vizuri kiasi kwamba ni rahisi kupewa nyadhifa za juu katika chama, ila Core-business yake ni Undercover; (wako kazini kiusalama na si kichama), Achana na Usalama hawa vijana wa siku izi, anatoa kitambulisho, mara bastola; Usalama makini nawaambia huwezi kumtilia shaka ndugu yangu, Angali comment yangu nyingine hapo juu, kuna mtu nimefanya nae kazi serikali ya awamu ya 3 yotee, same Dept, Tukaenda kusoma ughaibuni tukarudi awamu ya Jk miaka 3+ tuko nae ofisini ila nikamuona amevaa Gwanda anapewa Mkono na Mheshimiwa Rais wa Awamu hii ya 5, Nilistaajabu sana; hawa jamaa mtu anafanya kazi yake kwa ueledi huku akifanya jitihada zote asiweke wasiwasi juu ya walio karibu nae; Katika Idara zote na Taasisi za Serikali Lazima kuwepo watu wa system (ni lazima) BOT, Taasisi za Elimu, Mashirika ya Umma yote, Mamlaka zotee( EWURA,TRA,TRL,TFDA,TPA,MSD,SUMMATRA yaani mamlaka zote) Tena Hao TISS wanakuaga wanapanda taratibu vyeo kutokana na Usmart wao (Refer Mkuu wa Idara ya Usalama wa sasa MK)
Most of high political Leaders hasa wale walionza toka Mfumo wa Vyama vingi umeingia nchini, Believe me ni Under cover, Wako kiusalama zaidi kuliko kichama.

NB: Usalama wa Taifa uko katika nyanja nyingi sana, Kiuchumi, Kijamii etc ndio maana watu wanawekwa kwenye hizo Idara, vyama vya siasa, mashirika ya kijamii na Mamlaka zote; Infact Usalama wa Nchi ndio unahakikisha unapata Raisi ambaye hana viashiria vya kuhatarisha Usalama wa Taifa letu (i hope mtanielewa) Huwa wanapropose na kuhakikisha wanatoa Support stahili.
The best comment ever in this thread katika kuwaelezea hawa watu. CEO wa sasa wa eagle wing alikuwa BOT, Then NIDA sidhani kama sisi watu wa kawaida tulifahamu kuwa Mkuu yule ni jasus hadi alipoteuliwa kuwa CEO wa pale kitengo. Kwa maana hiyo wakuu wote wa tasisi nyeti sio RAIA wa kawaida Bali hawa jamaa. Pia ni jambo sahihi katika kulinda maslahi ya nchi na usalama kwa ujumla
 
Ushawahi kumsikia kisa cha Kijana huyu?

Edward Snowden - Wikipedia
1533625377382.png

https://en.wikipedia.org/wiki/Edward_Snowden

Edward Joseph Snowden (born June 21, 1983) is an American computer professional, former Central Intelligence Agency (CIA) employee, and former ...
 
mimi napendekeza badala ya kununua bombadia tuu ,tununue na ndege moja ya kisasa ya kijeshi kama vile F-16
 
The best comment ever in this thread katika kuwaelezea hawa watu. CEO wa sasa wa eagle wing alikuwa BOT, Then NIDA sidhani kama sisi watu wa kawaida tulifahamu kuwa Mkuu yule ni jasus hadi alipoteuliwa kuwa CEO wa pale kitengo. Kwa maana hiyo wakuu wote wa tasisi nyeti sio RAIA wa kawaida Bali hawa jamaa. Pia ni jambo sahihi katika kulinda maslahi ya nchi na usalama kwa ujumla
Sasa kama alikuwa NIDA kivipi alishindwa kuzuia ufisadi uliotokea pale??? Ifike mahala hawa TISS wapewe nguvu kisheria haya mambo ya kushauri shauri tu hayatufikishi popote ndio maana unajiuliza kipindi cha ufisadi wa ESCROW huyo MK alikuwa BOT ila hakuzuia lolote zaidi ya kutoa macho tu Tanzania ikiibiwa Billion 320+ sasa kuna faida gani ya kuwajaza kwenye hizi taasisi kama hawana impact yeyote?? Huko NEC mbona hawazuii wizi wa kura..... Vipi bungeni mbona sioni wakizuia miswada mibovu inayoweza kuweka usalama wa taifa kwenye rehani???

Hapo tu ndio huwa sielewi sheria zetu zimekaaje
 
Tungetambua ni kiasi gani hao watu wa TISS wanavyotoil kuhakikisha taifa liko salama, tungefunga na kuwaombea mema kila siku

Hii amani tunayoiona hapa kwetu huku majirani zetu Congo, Burundi na Kenya wakichinjana haipo tu kwa bahati mbaya. Kuna watu wanavuja jasho na damu kuilinda!
Mbona hawakuzuia wizi wa tembo,vifaru mpaka wameisha kabisa......makinikia tumeibiwa miaka 20 walikuwa wapi hawa TISS..... Kura zinaibwa huko ZEC na NEC,miswada mibovu bungeni ila bado watu mnawapa credit hao TISS wakati sioni la maana wanalolifanya kwenye ngazi ya kitaifa labda mngesema kusaka petty criminals ila wale moguls sioni hata wakibanwa na TISS ingawa ni mafia wa miaka mingi

TISS is overrated
 
Mkuu Unaonekana Una Elimu Na Intelligence Sio Kwa Hayo Mavitabu. Kama Una Hardcopy Nisaidie Naipenda Hii Kazi Nasikia Hawa Jamaa Wanaangalia Pia Watu Wachunguzi Wa Mambo Kupitia Novels Kama Hizo Hapo. Nimeanza Kusoma Kina James Hadley Chase. Novel Ni Tamu Balaa Ndo Maana Mzungu Begi Lake Nguo Mbili The Rest Books.
bas na wewe mkuu naomb hyo copy ya hiki kitabu ulichosoma sote tupate hyo burudan
 
Back
Top Bottom