Mkuu, karibu sana hospital Tena kitengo cha akina mama ndo utaelewa maana yake
Kuongezeka kwa idadi ya kujifungua kwa kisu ni mambo mengi yanachangia
1. Nimeona wamama wao wenyewe wakitaka kujifungua kwa kisu, ni vle hawataki complications za kusukuma, kutanua uke,...
2. Msukumo (presha) kubwa ambayo serikali inaweka kwenye huduma ya akina mama
Hii nchi ni Bora mgonjwa wa sukari afariki(hata kama imetokana na uzembe) kuliko mama/mtoto afariki wakati wa kujifungua. Kwahyo watu wa afya wanaona ni Bora kufanya operation kuliko kuhatarisha maisha ha mama/mtoto
3. Medical reasons Kwa ajili ya cesarian section kama mtoto kuwa mkubwa, presha/kifafa cha mimba, kisukari cha mimba,
4. Wamama wengi wanabeba mimba katika umri mkubwa ambayo ni risk ya kupata Post partum hemorrhage, Moja Kati ya sababu kubwa ya vifo vya akina mama, kwahyo kuepusha hayo, ni Bora kuzaa kwa kisu
5. Grand multiparity. Unakuta mama amezaa mara 8, misuli ya mji wa mimba imeshachoka. Kwahyo kusukuma inakua ni ngumu
6. Previous scar. Upasuaji wowote katika mji wa mimba mfano, kujifungua kwa operation, kuondolewa uvimbe...unaacha kovu(scar) kwnwye uterus(mji wa mimba) hivyo ni hatari sana mama kuja kujifungua kawaida maana mfuko utakua kwenye hatari ya kupasuka (uterine rupture. Na hvyo njia inayobaki ni kujifungua kwa kisu Tena na Tena