Update Maandamano Sept 23: Tayari Moshi Huu Unafuka

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Ujomile musani!.


Nilichokiona na kusoma mtandaoni kimepelekea kupeana taarifa jinsi gani jeshi la polisi linajiandaa hasa kwa Jumatatu ya tarehe 23.

Nikiwa njia panda ya Himo hapa moshi naona bus za polisi zikiwa uelekeo wa Dar.

Na kuna mdau kaposti bus za polisi zikitoka Morogoro.

Hebu tupeane taarifa kwa kinachoendelea hapo ulipo, ili na sisi abilia tunaosafiri kuja Dasramu week hii tukae vipi.

Ukipata kapicha kapachike hapa mdau!.

UPDATE:

Katika picha ni mitaa ya jiji la Dasramu mchana wa leo.


KAWE:
Jeshi la Polisi jioni hii wamevamia kikao cha ndani cha viongozi wa kata ya Bunju, Kawe na kuwakamata viongozi zaidi ya 23 waliokuwa kwenye kikao hicho.

Na upande wa pili patrol ya mtaa kwa mtaa inaendelea pichani.



Huku magari, farasi na mbwa.






JUMAPILI HII.
KUTOKA SPACE X:

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasiq na Maendeleo CDM, ndg Freeman Mbowe kasema;
"Natangaza kuwepo kwenye Maandamano yetu ya Amani na Maombolezo kesho Jijini Dar-es-Salaam, tarehe 23 Septemba 2024 na likitokea lolote miongoni mwetu, wengine tusirudi nyuma"

"Na mkisikia Mbowe nimekamatwa msirudi nyuma, mkisikia Mbowe nimepigwa risasi iombeeni roho yangu ipumzike mahali pema peponi"

" Ninyi songeni mbele"
 
mnaandamana wenyewe na halafu mnaweweseka wenyewe 🤣

hii dunia ni hadaa sana dah 🤣
 
Watapata Ajali na watakufa Tu mark my word.....ni Wapumbavu mnooooo wanaoaminishwa kupigana na Ndugu wanaopigania maslahi Yao kwa faida Yao. Kuwa POLISI haimaanishi kuwa mjinga na mpumbavu
 
Wapigwe chenga....

Wao polisi wakaandamane DSM lakini maandamano yafanyikie Arusha kwa Makonda au njooni Mwanza au twendeni Mbeya....!!
 
Jana wametupita sehemu Fulani na king'ora wapo katika defender kama tatu hivi. Wana mikogo balaa,tinted machoni na wengine wamevaa musk nyeusi wanaonekana macho tu.

Kila mtu aliyewaona aliwapuuza na kuwasema vibaya.Hawa jamaa Nina uhakika wanachukiwa na watz sana sasa hivi na siku likiwakuta baya tutashuhudia dhihaka nyingi sana mitandaoni.

Polisi na nyoka,hapa duniani hakuna viumbe vinapenda sifa kuwazidi Hawa wahuni wawili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…