UPDATE: Mahujaji zaidi ya Elfu Moja wamefariki Makka. Hakuna Mtanzania aliyepoteza Maisha wala kujeruhiwa

UPDATE: Mahujaji zaidi ya Elfu Moja wamefariki Makka. Hakuna Mtanzania aliyepoteza Maisha wala kujeruhiwa

Katika Uislam tunaamini wanaokufa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni mashaheed.

Dua zao zimekubaliwa, hiyo ni one way ticket ya peponi.
Ingekuwa kufa ni ishara ya ushujaa ya kumfanya mtu aende peponi kama unavyosema, basi kusingekuwa na Emergency first aid Centers ambazo zimejengwa kuzunguka maeneo yote inapofanyika hija.

Vituo vya afya ambavyo vipo katika hayo maeneo vilivyowekwa maalumu kwa ajili ya kupigania afya za watu ili wasife vinapingana na kauli yako kuwa kufa eneo hilo ni ticket ya kwenda peponi.

Pengine walioweka hizo hospitali maeneo hayo wanajua ukweli ambao wewe wamekuficha.
 
Ingekuwa kufa ni ishara ya ushujaa ya kumfanya mtu aende peponi kama unavyosema, basi kusingekuwa na Emergency first aid Centers ambazo zimejengwa kuzunguka maeneo yote inapofanyika hija.

Vituo vya afya ambavyo vipo katika hayo maeneo vilivyowekwa maalumu kwa ajili ya kupigania afya za watu ili wasife vinapingana na kauli yako kuwa kufa eneo hilo ni ticket ya kwenda peponi.

Pengine walioweka hizo hospitali maeneo hayo wanajua ukweli ambao wewe wamekuficha.
Unafikiri utaiona pepo bila kuuingia umauti?

Ingekuwa rahisi kama unavyofikiria, watu wasingekufa kwa wingi mahospitalini, wacha vituo vya huduma ya kwanza.
 
Yani nionee wivu watu waliokufa kisa dini??? Nitakuwa sipo serious aisee 😂😂😂
Sasa wewe wanakuhusu nini umeshupalia? Hata unachosoma hukielewi? Unaambiwa waeathoiriwa na "heat wave", unaelewa maana ya "heat wave"?

Sisi tunasema kwa kuwa wamefariki katika njia ya Allah basi wana ujira mkubwa peponi.

Hupendi hilo kwa kuwa wewe haujajisalimisha kwa Muumba wako?

Sikuelewi "argument" yako ni nini? Au ni uoga tu wa Uislam?
 
Labda pepo ya mabwege, wauza unga kibao tu wanajenga misikiti na kwenda Hija.

Hija ni njia ya Saudi Arabia kuingiza pesa kwa utalii wa kidini.
Unawaonea wivu?

Sijuwi kinachokukera nini watu kufariki wakiwa wanatekeleza ibada yao?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Zaidi ya mahujaji Elfu moja wamepoteza maisha katika mji wa Makka walikokuwa wamekwenda kuhiji kama sehemu ya kutimiza nguzo kuu tano kwa muislamu yeyote yule mwenye uwezo walau mara moja tu katika uhai wake kuweza kufika katika mji huo mtakatifu kwa waislamu .

Vifo hivyo inasemekana vimetokana na kuchochewa na joto kali sana lililokuwa limetokea katika Wiki hii na kufikia nyuzi joto 51 ,kwa wale tuliosoma Geography tunaelewa maana ya joto hili kuwa ni la juu sana na hatari kwa maisha mwanadamu.

Nchi mbalimbali zimeripoti vifo vya watu wake,huku Misri ikiongoza kupoteza watu wake ,ambapo mpaka sasa imepoteza watu 658. Tanzania haijapoteza wala kutokea kifo cha mtanzania yeyote yule wala majeruhi .

Tuendelee kuwaombea wenzetu hao warejee salama kabisa hapa Nchini na kuungana na familia zao.

Chanzo cha habari yangu ni Gazeti la Mwananchi la kiswahili.kwa undani zaidi unaweza jipatia nakala yake au kusoma kupitia mtandaoni na kulipia kulingana na uwezo wako wa kifedha. Lakini pia natamani wenye uwezo wa kifedha mliopo humu jukwaani pia mngekuwa mnachangia Jamii forum pesa kidogo ili kuwatia moyo .ikumbukwe hili ni jukwaa linalotukutanisha maelfu ya watanzania na kujadili masuala mbalimbali kwa uhuru sana.

Kazi iendelee.Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

PIA SOMA
- Saudi Arabia: Mahujaji zaidi ya 500 wafariki wakati wa Hija huko Makka
Ulikuwapo huko ama ni msemaji wa watz huko,au wawasaudi
 
Tatizo Kila nikiangalia teuzi Lucas Mwashambwa hayumo sijui kwa nn au ni chawa uchwara????? Pascal Mayalla. Majibu ya jumuiya ya machawa tafadhali.
P hana njaa sikuhizi,mtafute njanjaa nwenzie Luca atakusaidia majibu🤭
 
Back
Top Bottom