Sina uwezo wa kubadilisha jina kwa lugha nyingine, Allah ndiye mwenye sifa hizi:
Suratil Israa aya ya 110, “
دْ عُوا فَلَھُ الأَسْمَاءُ الْحُسْنَ ق ىلُ ادْ عوُا للهَّ أوَْ ادْ عُوا الرَّحْمَانَ أَیًّا مَا تَ …
Maana yake, “Sema: “Mwombeni Allah au
mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita.
Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri…”
ALLAAHU LLADHIY LAA ILAAHA ILLA HUWA (Yeye Ndiye
Mwenyezi Mungu Ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye tu),
ARRAHMAANU (Mwingi wa rehema), ARRAHIYMU (Mwenye
kurehemu), AL-MALIKU (Mfalme wa milele), AL-QUDDUWSU
(Mtakatifu, ametakasika na sifa zote chafu), ASSALAAMU (Mwenye
kuleta amani), AL-MU-UMINU (Mtoaji wa amani), AL-MUHAYMINU
(Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo Yake), AL-`AZIYZU (Mshindi
katika mambo Yake), AL-JABBAARU (Anayefanya analolitaka), ALMUTAKABBIRU
(Mkubwa), AL-KHAALIQU (Muumbaji), AL-BAARIU
(Mtengenezaji), AL-MUSAWWIRU (Mtia sura), AL-GHAFFAARU
(Mwenye kusamehe), AL-QAHHAARU (Mwenye nguvu juu ya kila kitu),
AL-WAHHAABU (Mpaji mkuu), ARRAZZAAQU (Mwenye kuruzuku),
AL-FATTAAHU (Hakimu), AL-`ALIYMU (Mjuzi wa kila kitu), ALQAABIDHU
(Mwenye kunyima au kuzuia), AL-BAASITU (Mwenye
kutoa), AL-KHAAFIDHU (Mfedheheshaji waovu), ARRAAFI`U
(Mpandisha daraja), AL-MU`IZZU (Mtoa heshima kwa amtakaye), ALMUDHILLU
(Mnyima heshima kwa amtakaye), ASSAMIY`U (Mwenye
kusikia), AL-BASIYRU (Mwenye kuona), AL-HAKAMU (Mwenye
kuhukumu), AL-`ADLU (Muadilifu), AL-LLATIYFU (Mwenye kujua
yaliyofichikana), AL-KHABIYRU (Mwenye kujua yaliyo dhahiri), ALHALIYMU
(Mpole), AL-`ADHIYMU (Aliye Mkuu), AL-GHAFUWRU
(Mwingi wa kusamehe), ASHAKUWRU (Mwenye kushukuru), AL-
`ALIYYU (Aliye juu), AL-KABIYRU (Aliye mkuu), AL-HAFIYDHU
(Mwenye kuhifadhi), AL-MUQIYTU (Mlinzi), AL-HASIYBU (Mwenye
kuhesabu), AL-JALIYLU (Wa hali ya juu), AL-KARIYMU (Mkarimu wa
hali ya juu), ARRAQIYBU (Mchungaji), AL-MUJIYBU (Mwenye kujibu),
AL-WAASI`U (Mwenye wasaa), AL-HAKIYMU (Mwenye hekima), ALWADUWDU
(Mwenye kupenda waja Wake), AL-MAJIYDU (Mwenye
utukufu), AL-BAA`ITHU (Mfufuaji), ASHAHIYDU (Mwenye kushuhudia
kila kitu), AL-HAQQU (Wa Haki), AL-WAKIYLU (Mtegemewa), ALQAWIYYU
(Mwenye nguvu), AL-MATIYNU (Aliye madhubuti), ALWALIYYU
(Mlinzi na Msaidizi), AL-HAMIYDU (Mwenye kusifika na
kila sifa njema), AL-MUHSIYU (Mwenye kuhesabu), AL-MUBDI-U
(Mwenye kuanzisha), AL-MU`IYDU (Mwenye kurejeza), AL-MUHYIYU
(Mwenye kuhuisha), AL-MUMIYTU (Mwenye kufisha), AL-HAYYU
(Mwenye uhai wa milele), AL-QAYYUWMU (Msimamia kila jambo), ALWAAJIDU
(Mtambuzi), AL-MAAJIDU (Wa kuheshimiwa), ALWAAHIDU
(Mmoja tu), ASSAMADU (Mwenye kukusudiwa kwa
kuabudiwa), AL-QAADIRU (Mwenye uwezo wa kufanya au
kutokufanya), AL-MUQTADIRU (Mwenye uwezo wa pekee juu ya kila
kitu), AL-MUQADDIMU (Mwenye kutanguliza), AL-MU-AKHIRU
(Mwenye kuakhirisha), AL-AWWALU (Wa Mwanzo), AL-AAKHIRU
(Wa Mwisho), ADHAAHIRU (Wa Dhahiri), AL-BAATINU (Wa Siri), ALWAALIYA
(Mpanga mipango ya watu), AL-MUTA`AALI (Mtukufu
Aliye juu), AL-BARRU (Mwema), ATTAWWAABU (Mwenye kupokea
toba za waja Wake), AL-MUNTAQIMU (Mlipa kisasi kwa waovu), AL-
`AFUWWU (Mwenye kusamehe madhambi), ARRAUFU (Mwenye
huruma), MAALIKU L-MULKI DHUL JALAALI WAL IKRAAMI
(Mfalme wa wafalme Mwenye utukufu na heshima), AL-MUQSITU
(Mtoaji haki sawa kwa kila anayestahiki), AL-JAAMI`U (Mkusanyaji
viumbe siku ya Mwisho), AL-GHANIYYU (Tajiri), AL-MUGHNIYU
(Mwenye kutajirisha), AL-MAANI`U (Mwenye kuzuia viumbe
visidhurike), ADHAARRU (Mwenye kudhurisha), ANNAAFI`U (Mwenye
kuleta nafuu), ANNUWRU (Mwenye nuru), AL-HAADIY (Mwongozaji
wa kheri), AL-BADIY`U (Mzuaji), AL-BAAQIYU (Mwenye kubakia
milele), AL-WAARITHU (Mwenye kurithi kila kitu), ARRASHIYDU
(Mwenye kuongoa waja kuiendea njia ya kheri), ASSABUWRU (Mwenye
kusubiri).”
Source /chanzo kutoka……