Update: Mfano wa oda ya mbao kutoka Njombe kupeleka Dar es Salaam yenye mchanganuo wa gharama na vibali vyote

Update: Mfano wa oda ya mbao kutoka Njombe kupeleka Dar es Salaam yenye mchanganuo wa gharama na vibali vyote

Una hela fungua hardware hautajuta.
Bei unapanga wewe na mteja hapindui.
Nitakupa MFANO wakati nauza hard ware.
Unanunia koki Kwa 6,000.wewe unauza 10,000
Unanunia msumeni Kwa 7,000.wewe unauza Kwa 10,000 hadi 12,000.
Unanunua elbow za half inch Kwa 3,00 wewe unauza 1,000 n.k
Yaani faida tu juuu ya faida.we angalia wamiliki wa hardware maisha yao
Msaada kwa maeneo yanayoweza kuwa na mzunguko mzuri kwa mikoa iliyochangamka
 
Habari za muda huu,leo ningependa kutoa mfano wa oda ya mbao ya mteja anaezitoa wilaya ya njombe kuzipeleka Dar es salaam.

Hapo chini nitakuwekea mchanganuo wa gharama na vibali kila kitu,fatiliana na nami:


ENEO LA KUPAKILIA:
Mkoa: Njombe
Wilaya: Njombe
Kijiji: Uwemba

TAARIFA ZA ODA YA MBAO

•Mteja anataka mbao size mbili tu ambazo ni 2×2 na 1×4 kwaajili ya kusambaza kwenye workshop wanazotengeneza bedsofa kule dar es salaam.

•Mteja anataka kupakia gari nzima aina ya semi yenye Tani 30.

•Baada ya kuchanganua ukavu wa mbao ,uzito wa mbao na ukubwa gari tumefanya makadirio gari inaweza kupakia jumla pc 7500 za size 2×2 na 1×4.

•Baada ya makadirio tumekubaliana mbao moja atanunua kwa 1,200/= kwa size zote (2×2 na 1×4).

MCHANGANUO WA GHARAMA YA ODA KUANZIA MANUNUZI HADI VIBALI KILA KITU HADI ZINAFIKA DAR ES SALAAM.

•Manunuzi: 9,000,000/=
•Usafiri: 3,000,000/=
•Kupakia: 200,000/=
•Ushuru (3% ya manunuzi): 270,000/=
•TRA (2% ya manunuzi): 180,000/=
•Transit pass (TP): 15,000/=
•Ushuru wa TP (20% ya TP): 3,000/=
•Ushuru wa magogo: 50,000/=
•Kuhakiki uzito mizani: 15,000/=
•Barua ta serikali ya mtaa: 5,000/=
•Usafiri wakati wa kushughulikia vibali: 12,000/=
•Kukodi leseni ya kufanya biashara bidhaa za misitu: 150,000/=
•Emergency cash: 350,000/=

JUMLA: 13,250,000/=


NYARAKA MUHIMU ZILIZOANDALIWA KABLA GARI HAJAANZA RASMI KWENDA DAR ES SALAAM

•Kibali cha kufanya biashara za bidhaa za misitu (mbao)
•Transit Pass (TP)
•Barua ya serikali ya mtaa
•Risiti ya ushuru wa mbao wa halmashauri
•Risiti ya kodi ya mbao TRA
•Risiti ya ushuru wa magogo ya halmashauri
•Gari tuliyokodisha ina risiti ya EFD kama mtoa huduma


Mpaka hapo gari yenye mzigo inakuwa ipo tayari kuelekea jiji la matapeli kushusha mzigo kama ni mbagala,Gmboto,tegeta,buguruni au kokote kule ataamua mnunuzi.

View attachment 3545247

•Kama unahitaji kuuliza jambo lolote lile kuhusu mbao za njombe usisite kuwasiliana nami.

•Pia kama upo Dar es salaam,Dodoma,Kahama,Simiyu,mtwara,Pwani nk na unataka kununua mbao njombe usisite kunitafuta nitakusaidia kila kitu hadi mzigo unafika eneo husika.

MAWASILIANO

0748874928 (Piga/sms/whatsapp)View attachment 3545247
KWAHIYO KWA KUSEMA HIVO MZIGO WA 9MIL UNAKUPA FAIDA YA AROUND 4MIL UKIUZA KWA 2500/PC. MEANS HAPO NI UKITOA GHARAMA ZOTE ZA AROUND 14MIL
 
Nimeshangaa mmoja anataka auze kwa siku moja kwani hiyo ni nyanya ,mbao hata ukiuza kwa mwezi sawa tu.
 
Somo zuri lkn mbona limekaa kutamanisha hivi kuhusu mtaji na ununuzi vipo Sawa kweli? Maana wanafanya biashara hizo huwa wanatutishia Sana kuhusu mtani
 
Uzi mzuri sana
Kuna wakati unaweza jikuta unashawishika kufanya aina Fulani ya biashara kupitia elimu kama hizi...very interested
 
Mkuu hiyo mbona kidogo? kaulize wanaouza madawa na kemikali wanapata faida kiasi gani... Mtu anaagiza sulphuric acid 2.5lt kwa Tsh 20,000 anakuja kuuza hadi 100,000.. kuna mwingine niliona anauza dawa inatumika kwenye kilimo cha mbogamboga ambapo 1kg aliuza Tsh 1,050,000 huku yeye kaagiza kwa Tsh 156,000. Biashara nyingi zina faida ila ndo upate sasa wateja
Huu ni wizi siyo faida. watanzania tunadidimizana sana tunabski maskini milele maana hakuna regulations.

Wakati wewe unampiga mwezio kwenye biashara yako na wewe utaenda kupigwa sehemu the same that is why tunabaki wote mlemle

Nimeona kwenye mtumba Mtu ananunia balo la nguo waatani wa nguo 600/= per pc yeye anenda kuuza 2000/= mpaka 3000/=.per pc.
 
Back
Top Bottom