Bukanga
JF-Expert Member
- Dec 13, 2010
- 2,857
- 1,936
M/kiti wa ccm mkoa wa shinyanga Mgeja:
Nataka niseme maneno machache,
Kwanza juzi mpaka saa nne na dk 59 nilikuwa mwenyekiti wa ccm, saa tano na dk nikajitoa ccm, baada ya kugundua ndani ya ccm hakuna hakuna haki, nami nikaona nijiunge na chadema chama chenye haki.
Jana mmemsikia vuvuzela ikipiga kelele kuwa tunamfuata Lowassa, ningekuwa namfuata Lowassa ningeenda Monduli nyumbani kwake.
Nashangaa vuvuzela Nape eti nimehama chama kisa mtoto wangu ameangushwa ubunge, nataka nimwambie Nape kuwa nina uzefu wa kushindwa, nampa Salamu kuwa tutakutana Mtama.
Nimepigiwa simu zaidi ya 800 zote zinanipongeza, simu sita tu zilikuwa zinanisikitia.
Niseme tu nyumba ya ccm inaungua unasubiri nini kuaga?
Nataka niwaambie Nape na wenye akili kama ya Nape kuwa waeleze wale vigogo wanaojihusisha na ujangili(Kinana) Waeleze fedha za escrow ziko wapi, ccm ni kichaka cha waizi, ccm waeleze kwanini shilingi inashuka, ccm mwulizeni Kikwete unatuachaje? Ataacha umaskini, chuki, husda na rushwa.
Pombe mwisho kaunta, mtaani ni Lowassa
Hahahahaha...
Mgeja bana...